Ripoti ya uchunguzi Moto Soko la Kariakoo utawekwa wazi Lini??

Vyura99tu

JF-Expert Member
Jan 14, 2017
266
500
Wadau kama taarifa hii ilishatolewa/kuwekwa wazi huenda mie sikuiona.
Waliopewa dhamana hii kwa wiki 2 nadhani ni miezi sasa imepita! Je? Nini kimeikumba timu hii au posho ya mkao ilishapita kama ilivyo desturi za kamati! Mheshimiwa Waziri Mkuu na Mkuu wa Mkoa tuwaombeni kujulishwa hili na huko ndiko kuwajibika kwa wananchi wenu.
Tanzania isiendelee kwa shamba la bibi!!.

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,983
2,000
Wanasubiri moto mwingine uwake,watangaze au kusoma pamoja...kua mtulivu ndugu mwananchi.
 
Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
7,204
2,000
Wadau kama taarifa hii ilishatolewa/kuwekwa wazi huenda mie sikuiona.
Waliopewa dhamana hii kwa wiki 2 nadhani ni miezi sasa imepita! Je? Nini kimeikumba timu hii au posho ya mkao ilishapita kama ilivyo desturi za kamati! Mheshimiwa Waziri Mkuu na Mkuu wa Mkoa tuwaombeni kujulishwa hili na huko ndiko kuwajibika kwa wananchi wenu.
Tanzania isiendelee kwa shamba la bibi!!.

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
Bado wako shule
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,447
2,000
Inapata vumbi kama ripoti zingine zilizoundiwa tume but watu wameshachukua mgao wao wa kuchunguza!kilichotakiwa pale ni fire brigade na police kuchunguza sio tume
 
Baraka21

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
1,282
2,000
Ripoti inasema hivi:

1. Miundombinu mibovu ya tangu enzi za mkoloni.

2.Hakuna chemba za maji

3.Magari ya zimamoto ilibidi yafuate maji airport

4. Moto ulidumu kwa masaa 6 hadi ukazimika wenyewe.

5. Vifaa duni vya zimamoto

6. Maji yaliyokuwa yanarushwa na magari ya zimamoto yalikuwa yanaishia njiani, hayafiki ghorofani

7.Wanasiasa kuja kuuza sura eneo la tukio wakati zoezi la kuzima moto likiendelea
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
43,543
2,000
Toka siku ile waziri mkuu amesema ripoti ya soko la kariakoo itatoka nilijua ni uongo. Waziri mkuu huyu alisema atatoa ripoti ya ajali ya lori la mafuta huko Morogoro mpaka leo kimya. Alisema atatoa ripoti ya aliyejiunganishia bomba la mafuta hapa Dar, mpaka leo yuko kimya. Inshort ni muongo wa wazi.
Wadau kama taarifa hii ilishatolewa/kuwekwa wazi huenda mie sikuiona.
Waliopewa dhamana hii kwa wiki 2 nadhani ni miezi sasa imepita! Je? Nini kimeikumba timu hii au posho ya mkao ilishapita kama ilivyo desturi za kamati! Mheshimiwa Waziri Mkuu na Mkuu wa Mkoa tuwaombeni kujulishwa hili na huko ndiko kuwajibika kwa wananchi wenu.
Tanzania isiendelee kwa shamba la bibi!!.

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom