Ripoti ya Synovate | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti ya Synovate

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mndebile, Oct 12, 2010.

 1. m

  mndebile Senior Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 4, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nimejaribu kuangalia kwa makini hii ripoti ya Synovate na kugundua mambo yafuatayo:
  1: Pamoja na kuwa na wabunge wachache katika bunge lililopita 2005-2010, kutoka vyama vya upinzani, wabunge wawili kutoka Chadema ndo walifanya vizuri zaidi katika kipindi hicho cha miaka mitano, ambao ni Mh. Zitto Kabwe 20% na Mh. Dr. W.Slaa 11% wakifuatiwa kwa mbali na Mh. H. Mwakyembe 3%,
  Hii ina maanisha kuwa CHADEMA kimekubalika zaidi kwa wananchi kwa kipindi hicho cha miaka mitano kwa utendaji wake.
  2: Kati ya wananchi waliohojiwa, 2000, 38% walionesha kuwa walishiriki katika kura za maoni ndani ya vyama vyao, Hii inatoa picha kuwa kati ya watu 2000 waliohojiwa, 700, yaani 35% ni wanachama wa chama cha mapinduzi CCM, kwa sababu, ndo chama ambacho kiliendesha kura ya maoni kwa nchi nzima kwa wanachama wake wakati wa uteuzi wa wagombea ubunge na madiwani, pamoja na kuwa vyama vingine vilifanya kura ya maoni lakini kwa CCM walikuwa na coverage kubwa zaidi, hivyo basi nashawishika kusema kuwa zaidi ya theluthi mbili waliohojiwa walikuwa wanaCCM. Na kama matokeo yanavyoonesha ndani ya hao wana CCM hawatakipa kura chama chao na bdala yake watapigia kura vyama vingine vya siasa.
  3:Kuhusiana na matatizo na kero mbalimbali zinazowasumbua wananchi wa Tanzania kila siku.
  Takwimu za Synovate zinaonesha kama ifuatavyo:
  a) Ajira, asilimia 81 ya watanzania waliohojiwa hawana ajira za kueleweka na kwa maana hiyo hawaridhiki na mwenendo mzima wa ajira Tanzania,chini ya CCM.
  b) Vyakula, ikumbukwe kuwa kila mwananchi anahitaji kula kila siku, takwimu za Synovate zinaonesha 72% hawaridhiki,
  c) Umasikini, 86% hawaridhiki,
  d) Rushwa, 73% hawaridhiki,
  e) Maji safi na salama ya kunywa 51% hawaridhiki,
  f) Kupata huduma za afya 48% hawaridhiki,
  g) Wanapokuwa kwenye vituo vya huduma za afya huduma wanazopata 50% hawaridhiki,
  h) Uhalifu 51% hawaridhiki,
  i) Barabara 57% hawaridhiki,
  j) Reli 62% hawaridhiki,
  k) Umeme 63% hawaridhiki,
  l) Usafiri mijini na vijijini 60% hawaridhiki.

  Pamoja na mapungufu mengi yaliyojitokeza katika hiyo ripoti, kwa upande ambao naamini haujachakachuliwa, mfano kwenye hizo kero zinazowasumbua wananchi walio wengi (maana inavyoonesha ni kuwa wao walitilia maanani zaidi kwenye uchakachuaji wa maoni ya kura ya Urais, ambapo pia kuna udhaifu mkubwa, mfano huwezi kuuliza kama uchaguzi ungefanyika leo nani ungempa kura yako, kati ya Raisi Kikwete, Dr. Slaa, Prof. Lipumba, mie naona kuwa na uwanja ulio sawa walitakiwa kama ni kuita Mh Kikwete, Mh. Dr. Slaa na Mh. Prof. Lipumba, sio kwa JK unatanguliza raisi Kikwete inachanganya watu, wengine watafikiri kuwa ni raisi tayari wa awamu ya tano)

  Takwimu zao zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 62 ya watanzania waliohojiwa (kama wapo) walionesha kuwa kero mabalimbali hawajaridhishwa na jinsi zilivyoshugulikiwa na serikali ya awamu ya nne, ikiongozwa na Mh. Jakaya Kikwete, hii maana yake nini? Kwa hali ya kawaida ni kwamba chini ya asilimia 38 ndo wameridhishwa na utendaji wa serikali ya Mh. JK.

  Swali : Inakuwaje zaidi ya asilimia 62 ya watu waliohojiwa wamesema hizo kero bado zinawasumbua, lakini wakati huohuo eti bado asilimia 61 ya waliohojiwa waseme kuwa wangemchagua Mh JK, ina maana wananchi wanashindwa kuunganisha matukio kuwa hizo kero zipo na hazijapata ufumbuzi ndani ya miaka mitano ya uongozi wa raisi JK anayemaliza muda wake, kwa kutokusimamia kwa makini watendaji walio chini yake au kutokuwa makini kwa serikali ya awamu ya nne kutatua na kushughulikia matatizo ya msingi ya watanzania?
  Hiyo asilimia 62.8 ya waliosema kuwa hawajaridhishwa na jinsi kero zilivyoshughulikiwa inanifanya niamini kuwa ni idadi hiyohiyo ndo iko tayari kupigia kura vyama vya upinzani, na kwa maana hiyo Nashawishika na kuamini vyama vya upinzani kwa ujumla wao watapata kuanzia asilimia 62 na zaidi.
  Tukumbuke kuwa unapofanya analysis za kitafiti, data zilizopo zinahitaji interpretation iliyo sahihi.
  Naomba kuwasilisha ili na nyie wadau mjaribu kuangalia hizo takwimu kwa makini, mtagundua hayo ninayosema.
   
Loading...