Tz mbongo
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 12,273
- 6,432
Ukiacha hizo takwimu huko kwa wenzetu tulikuwa tunasikia hospitali zimezidiwa kwa wagonjwa na wengine mpaka wakajenga hospitali za dharura na tulikuwa tunasikia hadi sehemu za kuhifadhi maiti zilijaa. Hiyo ndio athari za corona mbali na kujua takwimu.Hoja ya kuwa "kwani wewe una korona au unamjua aliyekufa kwa korona?" ni hoja isiyo na mashiko kwa sababu wakati Watu wanakufa kule Wuhan au Marekani haikumaanisha kuwa lazima kila mtu aambukizwe hiyo korona au afiwe na jirani ndo imaanishe kuwa korona ipo!
Hoja ya maana ni vipimo kwa wengi, uwazi wa kutangaza takwimu ndo tutajua picha nzima ya hali ya korona nchini.
Hii habari ya kuwa sijawahi kung'atwa na nyoka na sijamuona nyoka maeneo haya kwa hiyo nyoka hawapo ni logical fallacy ya kutisha sana!