Ripoti ya Sky News kuhusu Magufuli na COVID-19

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,061
2,000
Hiki ni kipande cha ripoti ya Sky News, moja ya shirika la habari la binafsi huko Uingereza.

Ni kipande kilichorushwa tarehe 8 mwezi Juni mwaka huu.

Ni kipande kinachozungumzia jinsi ambavyo Rais Magufuli na serikali yake ilivyoamua kukabiliana na huo ugonjwa wa Coronavirus.

Ni karibu miezi miwili sasa tokea Sky News wairushe hiyo ripoti yao.

Sky News waliirejea hofu ya shirika la afya duniani [WHO] kwamba Tanzania iko juu kwenye orodha ya nchi ambazo shirika hilo la afya lilikuwa na hofu nazo sana.

Miezi miwili kasoro juma moja, maisha bado yanaendelea tu kama kawaida!

Maiti hazijatapakaa mabarabarani. Hakuna makaburi ya halaiki. Spitali hazijajaa wagonjwa. Nikijizungumzia mimi binafsi, hakuna ndugu, jamaa, jirani, wala rafiki ambaye nimempoteza kutokana na hiyo Corona.

Kwa muktadha wa kinachoendelea sasa hivi baina ya Tanzania na Kenya, nadhani kuna kitu ambacho Wakenya wanaweza kujifunza kutoka Tanzania ya Magufuli.

Wameamua kukata sijui ndege toka Tanzania. Kuna kipindi sijui walifunga mpaka na Tanzania, na mengineyo.

Ninachokiona toka huko Kenya ni [1] uoga wa viongozi wao na [2] ukosefu wa uthabiti katika maamuzi yao.

Ni kama vile Kenya inaiga mataifa ya Ulaya na Marekani, kwa jinsi ilivyoamua kukabiliana na hiyo Coronavirus.

Tokea dunia ikumbwe na hilo janga, ni karibu miezi 6 sasa au hata na zaidi.

Kama yangekuwepo madhara makubwa sana basi yasingeweza kufichika kabisa.

Haiwezekani kuficha vifo na maradhi. Watanzania tulio wengi hatujaathirika na hiyo Corona. Maisha yetu yanaenda kama kawaida.

Hofu ya WHO haijatimizika. Natamani hao Sky News warudi tena Tanzania baada ya miezi miwili tokea warushe hicho kipande cha habari yao. Natamani warudi waje kufanya ‘follow-up’.

Sijui wakirudi watasemaje tu!!?

NB: Baadhi ya tafsiri zao za watu walioongea Kiswahili katika hii video yao Naona ni kama hazipo sahihi.....

 

Bungua

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
579
500
Wewe una Corona au ndugu zako wangapi ni wahanga wa Corona?
Kuuliza si ujinga lakini kuna swali la kijinga kama lako. Wewe na sampuli za aina yako mna tatizo kubwa sana la uelewa. Nchini Tanzania ugonjwa unaoongoza kwa kuua ni malaria. Au hata na hilo utabisha? Sasa nifahamishe ni nani kati ya vilaza wenzio kafa kwa malaria? Nani kafa mtaani au katani kwa malaria? Acha kuparamia usoyajua. Praise n worship team kwa hili ni usiku wa giza!
 

Papushikashi

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
8,143
2,000
Wanafahamika kuwa "ni wenye kukaanga mbuyu na kuwaachia we meno watafune."

Waliko wao mabarakoa hadharani si hiari. Kwao maisha ya waliopo 'ikungu lya bashashi' hayana thamani. Ila huko waliko kwenye black lives matter wako mstari wa mbele. Wanataka kuishi.

Hao ndiyo mangedere ngabu, kuona wanaona ya wenzao. Siyo ya kwao.

Jana wilayani Kahama abiria mmoja tokea Dar amefariki njiani jirani na nyumbani kwake. Night kali ya kwenye Saba Saba muda mfupi baada ya kushuka kwenye basi (rip).

Kisa na mkasa? Zile changamoto za zetu.

Kwenye Corona free country, Corona hsipo kabisa. Ila zile changamoto zetu.
Duh!
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,440
2,000
Ndugu zako wangapi wamekufa na corona?
Nyani Ngabu achana na hawa wanaokubeza, Mimi kama mpenda starehe nimeuzuria viunga vyoote vya starehe, tegeta KB, tegeta club 78, tegeta whatsap pub, baa za acculco bay, kinondoni the governors wamepiga siku ya ijumaa skylite band watu full nyomi,sura za wapenda starehe bado zipo fit na viunga vyotebvya tabatabbado wanakula bata kama kawaida
 

Bungua

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
579
500
hakuna korona bongo hata wew mi shahidi na ndiomaana huvai barakoa. Ni vyema kufurahia ushndi kwa
viongoz we2 dhidi ye2
Ushindi kwa viongozi wetu! Walitumia nini kufuta covid-19? Nilimsikia ajiitaye mwanasayansi bila sayansi akisema covid-19 tumeimaliza! Tulifanyaje tukaimaliza? Kwa nini tusiuze hiyo recipe USA, RSA, Spain na kwingineko tukawa matajiri wa kupindukia katika zama hizi za covid-19? Watu walimiminika kutoka kila pembe ya dunia kwenda kwa Babu wa Loliondo! Sipati picha wangapi watakuja kwa JPM kupata recipe? Ukiona hiki kimya na madongo ya rejareja kwake elewa kabisa si yeye wala hao viongozi wengine mwenye hiyo recipe! Na angekuwa nayo enzi za Iddi Amin kubebwa mabegani na mabeberu zingetua kwake. Angewakoga hatari. Mwenye recipe yupo. Aliye mwingi wa rehema na amejaa neema. Umrehemu amtakaye. Neema ummwagia ampendaye. Alimpenda Yakobo na kumchukia Esau bado mimba!
 

X-bar

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
624
1,000
Nyani Ngabu naona unaendelea kutoa mfululizo wa mada kuonesha kwamba COVID-19 "si kitu" kwa Tanzania bali tulijengewa hofu na "mabeberu" na kwamba utabiri (matarajio) juu ya ukubwa wa maambukizi ya C19 yalikuzwa kuliko hali halisi. Bali unajaribu kuonesha kuwa Rais Magufuli na serikali yake walikuwa sahihi kutofuata njia za "kimataifa" za kuzuia maambukizi kwa jamii (lockdown). Labda nikuulize.

1. Marekani ilitabiriwa idadi ya maambukizi ingezidi 1.5M na vifo 200K. Je, hao mabeberu walitabiri hali ya maambukizi na vifo kwa Tanzania ingekuwa kubwa kwa kiasi gani?

2. Serikali ya Tanzania iliacha kutoa takwimu za hali ya C19 wakati ambapo takwimu hizo zilikuwa zikionesha mwenendo wa maambukizi na vifo kuendelea kuongezeka kwa zaidi ya 100%. Je, unawezaje kupinga utabiri wa hao mabeberu wakati hakuna takwimu za kutuweesha kupima ukubwa wa tatizo?

3. Je, kwa kutumia maabara moja tu kupima C19 unadhani ilitosha kupata takwimu halisi za maambukizi na vifo kwa taifa lenye idadi ya watu zaidi ya mil. 50?
 

Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
6,330
2,000
Mada inazungushwa zungushwa na maneno mengi, lakini haisemi alichofanya Magufuli ambacho ni tofauti na walichofanya wengine wote kinachosababisha pawepo na tofauti kati ya Tanzania na hizo nchi nyingine..
Kiufupi, ni mipasho tu ya mapambio yasiyokuwa na maelezo.

Kenya kama ameigiza nchi nyingine, na huko Afrika ya kusini nako hivyo hivyo, na Rwanda je, kamwigiza nani. Uganda kamuiga nani?

Corona haipo Tanzania?

Watu Tanzania hawafi, unajua vifo vinavyotokea vinasababishwa na nini?
Kwahyo wew unajua vifo vinayotokea vinasababishwa na nini!!!
 

zanga

Senior Member
Dec 8, 2011
183
250
Mimi naishi nchi ambayo wamekufa watu zaidi ya elfu 60 kwa Corona.
Lakini sio kazini kwangu ambako tuko zaidi ya elfu moja au mtaani kwangu ambako namjua hata. Mtu mmoja tu aliyekufa.

Kwahiyo niamini hii nchi haina Corona?

wewe mwenyewe huko uliko unawajua wangapi waliokufa?
Ndugu,huko ulipo ni ugenini, sidhani kama huko Una ndugu, au marafiki wengi kama huku,katika hao watu 60,000 waliokufa humjui hata mmoja,unadhani ingekua bongo huku usingekosa hata jirani?.kuna nchi zina Corona hatujakataa, ndio maana vifo ni vingi, uliza huku kwenu ulipo na ndugu na marafiki na majirani wengi unaowafahamu, unaweza kuficha hivyo vifo 60,000???.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
6,441
2,000
Hoja ya kuwa "kwani wewe una korona au unamjua aliyekufa kwa korona?" ni hoja isiyo na mashiko kwa sababu wakati Watu wanakufa kule Wuhan au Marekani haikumaanisha kuwa lazima kila mtu aambukizwe hiyo korona au afiwe na jirani ndo imaanishe kuwa korona ipo!

Hoja ya maana ni vipimo kwa wengi, uwazi wa kutangaza takwimu ndo tutajua picha nzima ya hali ya korona nchini.

Hii habari ya kuwa sijawahi kung'atwa na nyoka na sijamuona nyoka maeneo haya kwa hiyo nyoka hawapo ni logical fallacy ya kutisha sana!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom