Ripoti ya Sky News kuhusu Magufuli na COVID-19

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,061
2,000
Hiki ni kipande cha ripoti ya Sky News, moja ya shirika la habari la binafsi huko Uingereza.

Ni kipande kilichorushwa tarehe 8 mwezi Juni mwaka huu.

Ni kipande kinachozungumzia jinsi ambavyo Rais Magufuli na serikali yake ilivyoamua kukabiliana na huo ugonjwa wa Coronavirus.

Ni karibu miezi miwili sasa tokea Sky News wairushe hiyo ripoti yao.

Sky News waliirejea hofu ya shirika la afya duniani [WHO] kwamba Tanzania iko juu kwenye orodha ya nchi ambazo shirika hilo la afya lilikuwa na hofu nazo sana.

Miezi miwili kasoro juma moja, maisha bado yanaendelea tu kama kawaida!

Maiti hazijatapakaa mabarabarani. Hakuna makaburi ya halaiki. Spitali hazijajaa wagonjwa. Nikijizungumzia mimi binafsi, hakuna ndugu, jamaa, jirani, wala rafiki ambaye nimempoteza kutokana na hiyo Corona.

Kwa muktadha wa kinachoendelea sasa hivi baina ya Tanzania na Kenya, nadhani kuna kitu ambacho Wakenya wanaweza kujifunza kutoka Tanzania ya Magufuli.

Wameamua kukata sijui ndege toka Tanzania. Kuna kipindi sijui walifunga mpaka na Tanzania, na mengineyo.

Ninachokiona toka huko Kenya ni [1] uoga wa viongozi wao na [2] ukosefu wa uthabiti katika maamuzi yao.

Ni kama vile Kenya inaiga mataifa ya Ulaya na Marekani, kwa jinsi ilivyoamua kukabiliana na hiyo Coronavirus.

Tokea dunia ikumbwe na hilo janga, ni karibu miezi 6 sasa au hata na zaidi.

Kama yangekuwepo madhara makubwa sana basi yasingeweza kufichika kabisa.

Haiwezekani kuficha vifo na maradhi. Watanzania tulio wengi hatujaathirika na hiyo Corona. Maisha yetu yanaenda kama kawaida.

Hofu ya WHO haijatimizika. Natamani hao Sky News warudi tena Tanzania baada ya miezi miwili tokea warushe hicho kipande cha habari yao. Natamani warudi waje kufanya ‘follow-up’.

Sijui wakirudi watasemaje tu!!?

NB: Baadhi ya tafsiri zao za watu walioongea Kiswahili katika hii video yao Naona ni kama hazipo sahihi.....

Valuhwanoswela

JF-Expert Member
Jun 27, 2019
451
500

UKIMWI una miaka zaidi 40 nchini toka ujulikane na Malaki ya watu kote duniani kufariki lakini Tanzania hakuna mtu hata mmoja aliyekufa kwa ugonjwa huo ila kifua kikuu, saratani na magonjwa mengine yaliua watu wengi sana kipindi hicho. Covid-19 kwa muda mfupi imeua malaki ya watu, mamilioni wakiugua kote duniani ikiwa pamoja na nchi zote zinazotuzunguka lakini kwetu ni watu 4 tu walioambukizwa wakifariki kwa magonjwa ya kawaidà kusitukiza ikiwa ni pamoja ugonjwa wa moyo, cancer nk
 
Uongo!

Nina ndugu kibao tu na wa karibu kabisa ambao wamekufa kwa upungufu wa kinga mwilini.

Ninao wengine ambao hivi sasa ni waathirika wa huo upungufu.

Na hakuna ugonjwa uitwao UKIMWI.

Hivyo, UKIMWI hauui. Kinachoua ni yale magonjwa nyemelezi kama kifua kikuu, saratani, malaria ya kwenye ubongo, n.k.

Jifunze....
 
Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
14,334
2,000
Serikali ilijitoa, sasa hivi korona ni ishu ya kila familia kujijua kivyakevyake
Hatuna takwimu halisi za kiwango cha korona nchini
Kwa hiyo kwa sababu wewe hujui takwimu basi kila familia ina Covid-19. Tuonyeshe makaburi basi? Au na kuko mmekatazwa kwenda kupiga picha za makaburi mapya?
 
Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
14,334
2,000
Kwamba Jiwe kwako ndio Muumba wa Mbingu na Nchi sio ?
Hiyo Bangi sasa, nani amekwambia JPM ni mungu? Ndio majungu yenyewe hayo naona hoja zinakushinda. Then unajimwambafy kwamba wewe unafanya kazi huko kwenye hospitali?
 
muheza2007

JF-Expert Member
Mar 19, 2010
414
1,000
Mimi naishi nchi ambayo wamekufa watu zaidi ya elfu 60 kwa Corona.
Lakini sio kazini kwangu ambako tuko zaidi ya elfu moja au mtaani kwangu ambako namjua hata. Mtu mmoja tu aliyekufa.

Kwahiyo niamini hii nchi haina Corona?

wewe mwenyewe huko uliko unawajua wangapi waliokufa?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom