Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

mkuu kweli unaamini failure ya TANESCO ni IPTL & Richmond..whatever it is still sikubaliani na hizo community/public property na ndio mwanzo wa unrealiable & poor services,unaongea failure ya City water ambayo tunajua ilikuwa kampuni ya briefcase iliyoingia kwa kifua cha hao mafisadi lakini kumbuka DAWASA ni disaster nyingine ambayo badala ya kusaidia ni mzigo tuu na Dar ni kama yote haina maji sasa sijui wanafanya nini?...mbona husemi TBL chini ya serikali iligeuza Tanzania kuwa 100% market ya wakenya with zero tax...free market rules monopoly ya Tanesco lazima iishe.
 
Imefika mahali nadhani wabunge wazuri wameanza kuachana na woga. Fanyeni kazi mliyotumwa na wananchi walio wachagua, bila ya kuweka maslahi yenu mbele kwanza. Mkifanya hivyo tutawapongeza na kuwaheshimu.

Koba, nadhani hukuwaelewa wanachokilalamikia wabunge hawa. Hawakatai kubinafsisha, but it has to be done the right way, na kwa utaratibu wenye kuleta manufaa. Sote tumechoka kuyashirikisha mashirika yetu, kwa mfano Shirika la ndege na lile la Afrika ya kusini. Sioni kama hapo palikuwepo na maandalizi mazuri, na ndio maana ikashindikana.

Tanesco ni shirika nyeti sana; hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kujitoa moja kwa moja katika mashirika kama hayo, hata kama kazi hiyo inafanywa na wafanyabishara.

Wabunge wanayo haki sana kuhoji utaratibu mzima wa kuyabinafsisha mashirika nyeti kama hili.
 
Posted Date::2/4/2008
Bunge: Fukuto la Richmond,Spika aahirisha ziara ya Marekani
* Waziri Mkuu, Makamba wateta kwa saa tatu
* Wabunge CCM kukutana leokuweka mkakati

* Yadaiwa kuna mpango wa kuzuia mjadala

Na Tausi Mbowe, Dodoma
Mwananchi

SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta ameahirisha safari yake ya kwenda Marekani.

Taarifa ya kusitishwa kwa ziara hiyo ilitolewa jana na Naibu Spika, Anna Makinda na kufahamisha kwamba leo Spika atakuwepo Bungeni kuendelea na shughuli za Bunge.

Hata hivyo katika tangazo hilo la Naibu Spika Makinda hakutaja sababu ya Spika kuahirisha safari hiyo.

"Wabunge kama mnakumbuka, Spika alitangaza kuwa atasafiri leo na kurudi siku ya Alhamisi, ameniagiza kutangaza kuwa amesitisha safari hiyo ya Marekani na kwamba kesho (leo) atakuwepo bungeni kuendelea na shughuli za Bunge kama kawaida," alisema Makinda.

Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa Spika amefikia uamuzi huo ili kuokoa jahazi kutokana na hali ya kisiasa kuchafuka kufuatia msimamo ulionyeshwa na wabunge kutaka ripoti ya Richmond iletwe bungeni kwanza kwaajili ya kujadiliwa.

Wakati anawaaga wabunge, Spika Sitta alimuagiza Naibu Spika, Anna
Makinda asije akakurupuka na kuyavamia mambo yote nyeti na kuyazungumza au kuyatolea maamuzi katika bunge hilo wakati yeye hayupo.

Sitta alisema kuwa mambo yote 'nyeti' yatasubiri mpaka atakapokuwepo na kwamba Naibu Spika asije akarudhusa kujadili mambo makubwa wakati hayupo.

Spika alitolea mfano wa sakata la ufisadi la Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na la Richmond na kusisitiza kuwa ili kujadili masuala hayo lazima yeye awepo.

Kauli hiyo ya Spika ina maana kuwa ripoti hiyo isingejadiliwa mpaka yeye yaani wiki ya mwisho ya kikao cha 10 cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma.

Juzi wabunge walisusia semina iliyoandaliwa na na Wizara ya Nishati na Madin ikwa lengo la kuwaelimisha kuhusu muswaada wa Sheria za Umeme na Biashara ya mafuta ya Petrol wakidai wapewe kwanza ripoti ya Kamati ya Richmond ili waijadili kabla ya kuupitisha muswada huo.

Wabunge hao pia walisema kuwa hawana imani na wizara hiyo pamoja na Shirika lake la Umeme Tanesco kwa kuwa taasisi hizo zimejaa uchafu na kwamba hawawezi kujadili masuala ya mikataba mengine mpaka wajisafishe.

Taarifa zilizopatikana kutoka miongoni mwa wabunge mjini hapa, zilieleza kuwa ili kuua mjadala bungeni, serikali inataka kutumia Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (Takukuru), kukamata baadhi ya maafisa na kuwafikisha mahakamani.

Chanzo chetu cha habari kilisema, juhudi zilikuwa zikifanyika tangu mwishoni mwa wiki kwa viongozi wakuu wa serikali kuwasiliana na Takukuru kwa ajili ya kuchukua hatua hizo.

Inadaiwa kuwa, kupelekwa kwa maafisa hao kuwatanyima haki wabunge kujadili suala hilo kwasababu ya utaratibu wa kuheshimu utawala wa sheria, lengo likiwa ni kuwaziba midomo wabunge hasa kutokana na cheche walizoonyesha mwishoni mwa wiki.

"Viongozi wanahaha kuhusu Richmond. Zimeenea habari kuwa viongozi wanaotaka kuua hoja hiyo bungeni wataitumia Takukuru kuwafungulia kesi maafisa kadhaa wa serikali kuwa walikula njama za kuihujumu Tanesco, iliwa na lengo la kuzuia mjadala bungeni," alisema Mbunge mmoja wa CCM na kuongeza:

"Upo uwezekano mkubwa watu hao watakamatwa kabla ya kikao cha wabunge wa CCM kinachofanyika leo."

Hata hivyo, Takukuru iliwahi kutoa taarifa za kuwasafisha maafisa waliohusika na kwamba hakuna rushwa iliyotumika kwenye mchakato mzima wa kufikia utoaji wa zabuni yenye mashaka ya Richmond.

Taarifa hiyo ya Takukuru ilipingwa na wananchi, huku Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Edward Hosea akisimama kidete kuwa hisia za rushwa ni juu ya mkataba huo ni majungu.

Kwa mujibu wa maelezo ya awali ya Spika, safari ya nchini Marekani ilikuwa na lengo la kuliongezea Bunge uwezo katika masuala mbalimbali yanayohusu shughuli zake na kwamba ingekuwa ya muda mfupi na kuahidi kurudi siku ya Alhamisi na kuendelea na shughuli kama kawaida na kujadili mambo hayo nyeti.

Siku hiyo pia Spika aliliambia Bunge kuwa bado mashauriano baina ya ofisi yake na serikali yanaendelea kuhusu ripoti nzima ya Mahesabu ya Akaunti ya Nje ya Nchi (EPA), kupelekwa bungeni kwaajili ya kujadiliwa.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Yussuf Makamba jana walikutana kwa dharura kuweka mikakati itakayowezesha Wabunge wa CCM kuwa na kauli moja kutokana kuwepo kwa mgawanyiko mkubwa kwa wabunge hao dhidi ya ripoti ya Richmond.

Viongozi hao wajuu wa chama hicho walikutana jana kwa zaidi ya saa tatu katika Ofisi za Bunge ili kuokoa jahazi kutokana na mgawanyiko huo unaonekana kutokea wazi wazi.

Habari zaidi zinasema kuwa wabunge wote wa CCM watakutana leo kwa ajili ya kuweka mkakati kabambe ikiwa ni pamoja na kuwa na kauli moja katika sakata hilo lilosababisha Spika Sitta kukatisha safari yake ya Marekani.

Kwa upande wa wabunge wengi walionekana kuwa na shauku kubwa kutaka ripoti hiyo ifikishwe bungeni kwanza ili wapate fursa ya kuijadili kwa undani ripoti hiyo.

 
napiga muluzi... nimeanza kuimba pambio ya "neema neema, neema imefunuliwa"...

tik tak tik tak

Mwanakijiji this is too early, unajua hao jamaa ni wasanii wakubwa, unaweza kushangaa tunapigwa bao lingine la kisigino litakalo tikisa nyavu ndogo, na atakayeshangilia zaidi ni EL. Hii ndio chance pekee ya kuitisha vote of confidence kama alivyosignal JK lakini sidhani kama wanaweza kufanya lolote!
Wabunge wetu na hata baadhi ya mawaziri wanamuogopa sana EL huenda atakachosema wote watanywea..............
Jumatano utaniambia......
 
Na mimi naona hivyo hawa jamaa wanabuy time ili kuendeleza usanii wao.
 
Huu ndio wakati umefika wa Mhe.JK...ku dump yale majitu ambayo ni liability ktk cabinet yake...i've feeling that mkuu wa mafisadi ambaye hata mzee JKN alimtema atakuwa wa kwanza akifunga virago...i bet JK atafanya cabinet reshuffle after kikao hiki cha bunge.
 
Huu ndio wakati umefika wa Mhe.JK...ku dump yale majitu ambayo ni liability ktk cabinet yake...i've feeling that mkuu wa mafisadi ambaye hata mzee JKN alimtema atakuwa wa kwanza akifunga virago...i bet JK atafanya cabinet reshuffle after kikao hiki cha bunge.

Mwanatanu:
1. Hiyo sio bendera ya Tanu.

2. Sina uhakika, hata kama ikitokea hiyo reshuffle ndio itakuwa dawa ya 'systemic ufisadi' uliokidhiri katika serikali ya huyu bwana. Kubwa zaidi ninaloliona ni kuweka mikakati ya kufunika mambo na kupoza chungu kinachoelekea kuchemka. Kazi ya kusafisha serikali itahitaji kufumua karibu serikali nzima; jambo ambalo haliwezekani.
Nadhani jambo analoweza kufanya Kikwete ili kurudisha imani yake kwa wananchi kwa kiasi fulani, ni kujinasua moja kwa moja na kundi hili lililomteka tokea wakati wa uchaguzi. Atuonyesha kwa vitendo thabiti kuwa mambo haya ya kuwaibia wananchi hataweza kuyavumilia. Atuonyeshe kwa vitendo, na isiwe kwa maneno tu kila mara, hata pale ushahidi unapoonekana kuwa upo kuchukua hatua. Asikubali mambo ya kulindana yamteke.
 
Sasa huyu jamaa Si angezuia kabisa kuundwa kwa tume? maana hela zetu zimeshatumika kisha ripoti inafanyiwa manyang'a nyang'au. Hii sio fair kabisa!

Tuweni na sense of responsibility mzee Lowassa!
 
ndio maana wenzetu walisema "njia ya kwenda jehanamu imetengenezwa kwa nia njema".

Ndio maana maneno ya "ni nia ya serikali", "lengo la serikali" n.k ni porojo, tumechoka na nia na makusudio kama yale ya kuleta sheria ya maadili (ambayo tayari ipo!)...
 
Ila msiwe na shaka siamini kama Lowassa anakwenda kokote ni aibu tu kidogo na kujeruhiwa kwa mpiganaji.. ila wa kumuonea huruma ni Msabaha...

tic tak tic tak...
 
mwulizeni dr spin Campbell na babake Tony Blair...wako wapi sasa..itachukua muda lakini hao wajanja watamwagika..my bet is on karamagi na Meghji
 
Hii shida yote ni ya jk mimi simwelewi kabisa ni nani alimwambia kwamba kazi yake ni kuteua tu? Akijuwa kuteua ajuwe na kufukuza anawaogopa nini jamani huyu mtu? TANESCO bila richmond ni mzigo mkubwa kwa wananchi sababu ya IPTL na Songas mnakuja kutuongezea machungu mengine ninyi watu mbona mmekosa huruma kiasi hicho mwogopeni Mungu!!?

JK jamani inabidi akumbuke kuwa katiba yetu inasema rais wetu ni mtendaji si mwenezi au msemaji kama anavyofanya yeye kama ameshindwa a step down tuweke rais mtendaji TUMECHOKA.
 
FD, nadhani wanaliandaa TAifa kisaikolojia... na wanajaribu kujenga very high expectations... lakini mchezo waweza kuwa hivi.

a. Hoja ya Richmond italetwa (ya BoT wala haitajadiliwa sasa kwani Kamati ile nyinginee bado inafanya kazi zake, kwa hekima za spika hilo litawekwa kiporo)

b. Wabunge kadhaa wa CCM watapiga kelele na kutaka kichwa cha mtu kwenye sahani. Wabunge hao ambao tayari wametiwa alama watasimama na kuzungumza kwa ukali wote kiasi cha kufanya tuamini na tushindwe kutofautisha kipi ni maigizo na kipi ni kitu halisi.

c. Vyombo vya habari vitadaka hivyo na kama vila walivyotangaza "Balali Ajiuzulu" watakambilia kutangaza "Wabunge Wacharuka" bla bla bla.. Wananchi waimba sifa za JK na timu yake.

d. Waziri Mkuu atasimama na kuelezea jinsi hali ilivyokuwa na jinsi alivyojaribu kuingilia kati kwa nia njema na si kwa nia mbaya. Atawaomba radhi wabunge wenzie na kusema ndio wamejifunza bla bla bla.. Wabunge watapiga makofi kwa uungwana wa Lowassa..

e. Kwa vile bado kichwa kinatakiwa basi Msabaha na timu yake watawekwa kiti moto. HIli hata hivyo linaweza kutokea masaa machache kabla ya ripoti kuanza kujadiliwa na hivyo it will mirror the resignations of Simba and Ngasongwa some years back.

Njia pekee ya kupush wana CCM wamchukulie hatua WM ni kwa mbunge kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu..
 
Hakuna Jipya litakalofanyika....

Alau G55 ingelikuwepo tungesema lipo litakalofanyika...Lkn G55 wote wakapewa madaraka basi. Ukiona Mbunge analeta chochoko au maneno mengi dawa yake kumpa Cheo nae ale akae Kimya.

Wakati Fulan Jamaa yangu mmoja alikuwa anazungumza na Mmoja waliokuwa wanaBodi ya ATCL..enzi za Ben..anasema yaani wazir hajasoma hata huo mkataba, mkataba kawaambia wazungu wandike kila kitu nae atie sign. Kwa mazingira kama hayo unategemea Nini....Mawazir hata Content ya Mkataba hawaijui...unless ifike kipindi cha Mabomu kulipuliwa...

Mawazir wetu hawapo serious na uchumi wa NCHI. Wakati Marehem Malima akiwa wazir wa Mipango wakati wa Mwalim Nyerere. Serikali ilitangaza tender ya MV BUKOBA. Ndugu yake mmoja Mwalim Nyerere alimfuata Malima kuwa yeye ana rafiki zake wapo Nje ya NCHi wanaweza leta Meli itakayohudumia Ziwa Victoria. Marehem Malima akamwambia afuate Masharti ya serikali ktk tender, hao marafiki zake waombe kama kawaida na uchaguzi utategemea nani ana uwezo na si urafiki/kujuana. Yule Ndugu ya Mwalim akaona mpango wake ushashindwa au unaelekea kushindwa. Akaenda Kumuona Mwalim Nyerere akamueleza juu ya mpango mzima. Nyerere akamwita Malima kumuhoji ilikuwaje. Marehem Malima alimwambia LIVE mwalim kuwa Taratibu za kiserikali zifuatwe.

Mwalim Nyerere akamuambia Malima, kuwa Malkia wa Uingereza pamoja na kuwa anaWazir wa Fedha, lkn bado Malkia ndie Mwamuzi wa Hazina nzima ya Uingereza. kwa statement hio ni kuwa ikiwa Nyerere ana wazir wa Fedha/Mipango, bado yeye ndie Mwamuzi wa mwisho wa Mipango/Hazina ya nchi
na Malima, akamwambia ikiwa wewe Rais unanitaka nichukue uamuzi wa kuwapa Tender Rafiki wa Ndugu yako, basi niandikie MEMO, ili nikichukua uamuzi niwe na ushahidi kuwa nilifanya as per direction na Order of Mr. President. Mwalim Nyerere akamwambia basi kesho ntakupa hio Memo.

MEMO iliyofuata ilikuwa Malima kuondoshwa W/Mipango na kurudishwa UDSM kufundisha...

Kama Balali nae angefanya namna hii, basi hii kesi yake ingekuwa ndogo sana leo hii. lkn Mawazir/Wabunge na watendaji wengine wa serikali wamekuwa si Walinzi wa hazina zetu za NCHI.

Mawazir wengi wa Serikali yetu wanahisi nafasi walizopewa si HAKI yao,bali ni favor ya RAIS means uwezo wa kuongoza wizara hawana nao. na Hata kujituma wafanye basi wameshindwa. Sifikirii kwa Bunge hili na Mawazir hawa kutafanyika JIPYA. Ukichunguza CCM kuanzia M/Kiti wa Serikali ya Mtaa hadi KILELENI, asilimia 90 au wote wameingia KIFISADI.
 
Kumekucha. Yalianza ya Slaa wakafikiri utani,sasa haya ya Richmonduli,tutasemaje. Nilisema mwanzo hizi sera za msimamo wa chama zitawatokea watu puani,kama walivyodai CCM kuwa yeyote atakayehusika kwenye sakata la BOT na ni mwanaCCM huo mzigo ataubeba mwenyewe. Hili la richmond mbona Lowassa lamuwasha. PM subiri kivumbi
 
Chuma acha ungo lete data hapa.

kwa nini mnapenda kupakazia hivi, hivi kweli wewe untuambia eti mwalimu alimkubalia ndugu yake na akamtalia Malima!

Hivi kweli mwalimu alikuwa hivyo!
 

MEMO iliyofuata ilikuwa Malima kuondoshwa W/Mipango na kurudishwa UDSM kufundisha...


Na 'hao ndugu zake' Mwlm walipata hiyo zabuni ya Mv Bukoba?
Put in some flesh please, or withdraw the statement.
 
Chuma acha ungo lete data hapa.

Chuma kaeleza kadri ya data alizonazo na kwa kiwango alichoamua kutoa, kuthibitisha kama kaongopa wewe unayejua otherwise ndio unapaswa kuonyesha upande wa pili. Vinginevyo maneno yake bado yanasimama!
 
Back
Top Bottom