Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Kuna kitu kimoja sikielewi labda wakuu mnaweza kunisaidia. Nimeipitia juu juu ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Mwakyembe. Naona watu wameongelea sana kutaka watu kujiuzulu, na wanaohusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

Pia Dk. Mwakyembe amelalamika kuwa watu waliohojiwa hawakutoa ushahidi wa kutosha "officially" katika kiapo.Na wengine wametoa ushahidi nje ya kiapo.Sasa kama mtu hatoi ushahidi katika kiapo na anakuja kutoa ushahidi nje ya kiapo hapo hamna kesi ya "obstruction of justice" ili kuweza ku uphold rule of law?

Inawezekana hili ni swala dogo in the grand scheme of things na watu walifocus kumtoa Simba ndani ya nyumba kabla ya kupanga vikombe kwenye kabati, lakini inabidi tuweke standards za juu kuhusu utawala wa sheria ili kesho watu wajue kuwa ukiitwa na tume yenye mamlaka ya kisheria, inabidi utoe ushahid, utoe ushahidi wa kweli, na utoe ushahidi wote. Siyo mambo ya ma deal na ushahidi wa vichochoroni ambao unakosa nguvu.

[ame]https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=9687[/ame]
 
Pundit,
Mimi sio mwanasheria, lakini nijuavyo ni kwamba kutosema kila kitu si obstruction of justice. Obstruction of justice has to do with doing something that obstructs the pursuit of justice. It is not about not doing something. For instance, by not going to testify, Edward Lowasa did not obstruct justice. Gumzo nje ya mahojiano, hata kama lina ukweli, halitii vizuizi kweye kutafuta haki.

Dr. Mwakyembe ni msomi wa sheria. Nafahamu masters yake alisoma Queen's Univesrity, Canada, lakini PhD sijui aliisotea wapi. Kama kungekuwa na obstruction of justice angesema hivyo.

Ni maoni yangu kwamba ilikuwa unethical kutoa gumzo la akina Msabaha la nje ya mahojiano rasmi, katika ripoti. Sielewi kama katika mipango yao kabla ya kutoa ripoti bungeni, Mwakyembe, JK na hata Sitta, waliona umuhimu mkubwa wa kumvaa Lowasa kiasi hata cha kukiuka miiko ya kwaida. Hakuna shaka Mwakyembe alipata go ahead ya JK kabla hajakamilisha ripoti yake. Ni wazi kwamba ripoti ya Mwakyembe ilimsaidia JK kwenye siasa zake. Ni siku nyingi alitaka kumweka Mizengo Pinda nafasi hiyo.

Itabidi makosa yaliyofanywa sasa yasirudiwe na kamati teule za baadaye. Baada ya kamati kupokea ushahidi unaoweza hata kumfunga Lowasa, ilibidi wamwite ajitetete. Hii ni kawaida kabisa.

Kiini cha matatizo haya ya wakubwa wachache kuuza nchi ni msimamo wa serikali kwamba si lazima Bunge lijadili na kuridhia mikataba mikubwa kati ya serikali na wawekezaji. Kama ukiukwaji huu wa katiba utaendelea (ninimeonyesha, mahali pengine hapa JF, kwamba ni ukiukwaji wa katiba), basi hata Mizengo Pinda na mawaziri wapya wakipenda wataweza kuendelea kuuza tu nchi.
 
Itabidi makosa yaliyofanywa sasa yasirudiwe na kamati teule za baadaye. Baada ya kamati kupokea ushahidi unaoweza hata kumfunga Lowasa, ilibidi wamwite ajitetete. Hii ni kawaida kabisa.

Ni kweli mkuu juu ya feelings hizi, lakini baadhi ya wanasheria wanasema kwa kuwa ripoti ya kamati haijatoa adhabu, bali imeshauri hatua zaidi zichukuliwe baada ya kupima matokeo ya ripoti hii, basi hakuna umuhimu wa kufikiria kuwa kwa kweli EL angehojiwa kujitetea.

Bado ana uwanja mpana sana wa kujitetea akifikishwa mahakamani.

Kuna wakati EL alikuwa implicated kwenye uchunguzi wa zogo la Malima na Mengi, na kamati husika ikaomba aitwe...Spika, kinara wa Kamati ile, akasema kuwa kwa kutumia busara, kuzingatia uzitito wa nafasi ya EL kitaifa, asiitwe. Na ikawa hivyo, na EL hakulalamika kwa nini hakuitwa. Sasa juzi alipouliza kwa nini hakuitwa kutoa ushahidi, kamati ikatoa incident hii hii kama reference ya uamuzi huo.

Si hivyo tu, bali pia walimwambia kuwa hawakuwa na haja ya ushahidi zaidi, kwa kuwa ushahidi wa maandishi, mdomo na ki hali ulijitosheleza na kamati iliridhika nao.
 
Wengi wameshasema mengi na hakukuwa na ulazima wa kumuita Waziri Mkuu. Halikuwa suala la Edward Lowassa kama mtu bali Waziri Mkuu kama ofisi.

Ndio maana utaona kuwa ripoti inataja "Waziri Mkuu" badala ya Lowassa. Sababu ni kuwa ushahidi wote wa kuhusika kwa ofisi ya Waziri Mkuu upo na ni sehemu ya vielelezo.

Unapofanya uchunguzi na kukuta barua halisi inayosema "mwambie fulani akupatie kitu hiki, kama nilivyoagiza" na barua hiyo ina jina sahihi na cheo cha mhusika hauhitaji kumuuliza Mhusika uliandika barua hii. Ni wazi ingekuwa vizuri kuuliza kwwanini?

Lakini overwhelming evidence ni zaidi ya mfano huo. Pindi vielelezo vikikamilika kuwa scanned vitawekwa mbele yetu ili tuweze kuona na kuamua kwaninin kesi dhidi ya Lowassa ilikuwa kubwa hivyo.

Kamati hii si Mahakama ambapo kuna Mlalamikaji na Mlalamikiwa. Lowassa kama anaona hakutendewa haki anaweza kwenda mahakamani. Vinginevyo angegoma kujiuzulu na kukubali kufukuzwa na Rais na kusimamia innocence yake.

Lowasa hakuonewa, yeye anajua hivyo na Wabunge wenzie wanajua hivyo. Tafadhali pitieni ile thread ya "Lowassa awatisha Mawaziri"
 
Kwani wakina Mwakyembe walikataa kumsikiliza?Yeye akijua kuwa ofisi yake itatajwa ali'offer' kutoa upande wake akakataliwa? Nakumbuka wakati Madiba ni rais palikuwa na kesi mahakamani iliyomhusu. Wakati watu wanajiuliza kama aitwe yeye akatangaza kuwa yuko tayari kwenda mahakamani kutoa ushahidi na alipoitwa alifanya hivyo. Tatizo nyumbani viongozi wanakuwa kwenye ivory tower na wanangoja kubembelezwa. Safari hii Mkuu alifanya strategic mistake.
 
Wengi wameshasema mengi na hakukuwa na ulazima wa kumuita Waziri Mkuu. Halikuwa suala la Edward Lowassa kama mtu bali Waziri Mkuu kama ofisi.

Ndio maana utaona kuwa ripoti inataja "Waziri Mkuu" badala ya Lowassa. Sababu ni kuwa ushahidi wote wa kuhusika kwa ofisi ya Waziri Mkuu upo na ni sehemu ya vielelezo.

Unapofanya uchunguzi na kukuta barua halisi inayosema "mwambie fulani akupatie kitu hiki, kama nilivyoagiza" na barua hiyo ina jina sahihi na cheo cha mhusika hauhitaji kumuuliza Mhusika uliandika barua hii. Ni wazi ingekuwa vizuri kuuliza kwwanini?

Lakini overwhelming evidence ni zaidi ya mfano huo. Pindi vielelezo vikikamilika kuwa scanned vitawekwa mbele yetu ili tuweze kuona na kuamua kwaninin kesi dhidi ya Lowassa ilikuwa kubwa hivyo.

Kamati hii si Mahakama ambapo kuna Mlalamikaji na Mlalamikiwa. Lowassa kama anaona hakutendewa haki anaweza kwenda mahakamani. Vinginevyo angegoma kujiuzulu na kukubali kufukuzwa na Rais na kusimamia innocence yake.

Lowasa hakuonewa, yeye anajua hivyo na Wabunge wenzie wanajua hivyo. Tafadhali pitieni ile thread ya "Lowassa awatisha Mawaziri"

Nakubaliana nawe Mkuu, ni kweli tupu. Huyu angekuja kuwa kinara wa mafioso nchini kwa kutumia pesa zake na madaraka. Tamaa na over-ambitious vilimfanya ajisahau kuwa ni mtumishi wa umma.

Mtu wa hadhi yake analalamikaje kuwa barua yake aliyompa spika 28January 2008 haikuwa sehemu ya ushahidi wa ripoti ya kamati iliyowasilishwa kwa spika 31 Dec 2007? Hakuwa na lolote la kujitetea, afadhali mara 10 Dr Msabaha aliyelenga kuboresha ripoti ile akakubali yaishe.
 
Mtu ukisema uongo chini ya kiapo si 'perjury' hiyo? Kama Bill, mumewe Hillary,aliposema " I did NOT have sexual relations with that woman" Si alinyang'anywa leseni yake ya uwakili ktokana na hili? Au hawa wakuu hawakusema uongo bali walikataa kuji'commit one way or another'? Kwa vyovyote vile ni serious issue.

Fundi labda hukupata habari kamili, Bill hakusema uongo, isipokuwa hakusema ukweli. It was not sex it was a BJ, the two are not same so Bill did not lie.
Lakini hawa watu wa kwetu kuna sababu iliyowafanya waseme kwa namna walivyosema, kama wangesema wazi chini ya kiapo, basi hatua ambazo zingechukuliwa immediateley zingekuwa na side effect mbaya kwa taifa.
Lakini sasa ex PM yuko nje, naona mengi yanaweza kuzungumzwa ili jamaa na wahusi9ka wengine wafikishwe wanapostahili!
 
Bill ni maarufu kwa ku'split hairs'. Alikuwa notorius kwa kusema alivuta bangi lakini hakumeza moshi. BJ ni sehemu ya sexual relations ndiyo maana alitoswa. Alijaribu kutumia semantics lakini haikusaidia. Kipimo ni jee mtu akimkuta mke wake anatoa hiyo huduma kwa jamaa,mkewe ataweza kujitetea kuwa hakuwa na uhusiano wa kimapenzi?

Kwa nini unasema kama hawa waliohusika wangesema wazi chini ya kiapo pangekuwa na athari kwa taifa? Kwa kutokuwa wazi wamesaidia nini kwa taifa? Hatua isingeweza kuchukuliwa immeadiately maana yote yangeingizwa kwenye taarifa! Au mwenzangu ni mwanasheria kwa hiyo kuna kitu unachojua nisichokijua?
 
Kama kungekuwa na ushahidi wa wazi na wa kutosha kuwafikisha hawa mafisadi kwenye mkono wa sheria, ingekuwa ni mara ya kwanza kwa PM kuingia kwenye njia kama hiyo, na ambayo yangefuata kutona na proceeding yangeweza kuwa na negative effect kubwa, huenda na yeye kwa hasira au kwa ile ya "tufe wote", basi angewaingiza mkenge wengi. That means hata serikali ingeyumbishwa kidogo, kitu ambaco kwa sasa hatukihitaji. For sure EL pale alipo anajua mengi sana yanayohusu ufusadi ndani ya serikali na anaweza kuwasambaratisha watu vibaya sana, kama hii issue at this moment haitaishia kwenye kujiuzulu tu. Kwa hiyo siyo suala la sheria, ni suala la kuangalia tu jinsi serikali yetu ilivyo, na hali yake tete ya sasa, kuna mabomu mengine yanasubiriwa, sasa ni vema yakalipuka taratibu ili liwe handled moja moja, na siyo yalipuke yote at a time, itakuwa kzungumkuti!
 
Balozi Kazaura, aliandika barua hiyo Februari 7 mwaka huu kuelezea malalamiko yake ambayo yanahusu ukurasa wa 37 na 38 wa taarifa hiyo iliyowasilishwa bungeni Februari 6 mwaka huu na Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge ya Uchunguzi wa Mchakato wa Zabuni ya Richmond, Dkt. Harrison Mwakyembe.

Katika barua hiyo, Balozi Kazaura analalamikia aya mbili katika taarifa hiyo, ya kwanza ikisema: "...Balozi akatoa maelezo ya ziada kuwa Richmond ilikuwa mradi wa 'Bwana Mkubwa' na 'mshirika wake mkubwa kibiashara' akimaanisha Waziri Mkuu na Bw. Rostam Aziz (MB)".

Ya pili ni inayosema: "Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Balozi Kazaura kuushusisha uteuzi wa Richmond Development Company LLC na mkono wa Waziri Mkuu. Mara ya kwanza ilikuwa Januari 2007 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Biashara."

Akifafanua kuhusiana na aya hizo, Balozi Kazaura, alisema katika barua yake hiyo yenye kumbukumbu namba SEC.216/2/2008, kwamba kwa mujibu wa kumbukumbu zake ambazo anaamini ni sahihi, hakumbuki kutamka bayana maneno kama yalivyonukuliwa na kama yanavyosomeka katika taarifa hiyo.

"Kama kuna maelezo yoyote ya ziada nje ya kiapo kama ilivyowasilishwa, sikumbuki niliyatolea wapi, mbele ya nani na wakati gani...na hata kama nilitamka au kutoa maelezo ya ziada nje ya kiapo kama ilivyowasilishwa, naamini nisingeweza kutaja wahusika hao wawili kama ilivyotafsiriwa katika taarifa," alisema Balozi.

source: Majira
 
Huyo Balozi Kazaura ni mwoga anaogopa mafisadi.Akikataa kuwa hajatamka ataletewa tape,watanzania wamechoka..Unaogopa nini ,Lowassa sasa ni mbunge tu,RA hana nguvu,maana tushakata tawi lake moja.
 
Balozi Kazaura hana haja ya kutoka hadharani kukubali au kukataa hoja hiyo kwa sababu its too late and mtu ameshakuwa executed. In fact, he can reverse a lot of nothing!
He remains with psychological upheaval and that the price of democracy. Watanzania wameridhika na yote yaliyotokea. Mungu ndio anayajua ya sirini na atamlinda kama alisema au hakusema ukweli ili demakrasia na haki vitimie. Hakuna shaka yoyote kuwa watanzania walidhulumiwa mali zao na wakalalamika kwa Mungu, Mungu nae aka-expose the reality because the voice of people is the voice of God!Dont blame Mwakyembe et al, that was "THE VOICE OF GOD"
 
Mzee Mwanakijiji,
Sasa huyu Kazaura ndiye mwenye point kwa sababu maneno hayo aliyasema nje ya kiapo na off the record imekuwaje yatumike?...Hivi kweli sisi Wadanganyika bado tunafikiria kuwa Tanzania hakuna Mafia?
Hakuna kati yetu anayefahamu hofu iliyomfanya akatae kusema under oarth, leo habari hizo zimekuwa wazi tena kitu ambacho alikuwa akikiogopa toka mwanzo. Lowassa na Rostam Aziz wote wako huru nje na hatufahamu marefu ya mikono yao..
Nina hakika kabisa kama tutajaribu kuwasimamisha hawa wa tu mahakamani basi Kazaura ni mtu wa kwanza kuondolewa...
 
Ni jukumu la serikali sasa kuwapa onyo akina RA na EL juua ya tabia hizi za kulipiza visasi kama kwa akia Kubenea ili kuijenga Nchi .Mzee ni muoga lakini nina ushahidi mwingi kwamba alisema hata mwanae mmoja yuko Japan anasema issue si ndogo na hata mkuu wa kaya anahusika watu hawakusema tu .Ndiyo wanaogopa isijadiliwe Bungeni sasa .
 
inamaana RDC=APSON=KAGODA?

RDC ime shake Nchi na utawala wake kama Zitto kutolewa Bungeni pia .Lakini makubwa bado yamelala chini ya RDC na walicho kifanya kwa uharaka ni kumwambia Lowasa ondoka kufa wewe mmoja tubakie madarakani .Leo issue RDC bungeni inaanza kupangia chenga , bado BoT ambayo inaweza kuona Rais anaomba kujiondoa .Naamini BoT hawatataka ifike Bungeni kwa kweli .Nasema Polisi take over upelelezi ufanywe na ripoti iwe wazi isije ikawa kama mambo ya ujambazi na madawa ya kulevya hadi sasa hayujui nini kinaendelea .

Kosa la Lowasa na wenzake ni kosa la kuhujumu Uchumi wa Nchi .Kujiondoa pekee hakutoshi bali Mahakama ijue na iamue swala hili .

Kazaura tupe nafasi tumalize moja hili kwanza then tutakuja kukuchambua na kukueleza ni wapi umeibia Tanzania vya kutosha.
 
Huyu mzee nae! Sasa kwani angesema nini zaidi ya hapo,ndio maana aliwauma sikio,ili wakisema abishe! Lakini sidhani kama kamati nzima itasema uwongo.
 
Back
Top Bottom