Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Jamani eeh. Hili suala ni pana sana nimeisikia ripoti pale bungeni alipokuwa anisoma Mtetezi wa wanyonge Mh. Dk Mwakyembe nimepata na mshtuko na kilio baada ya kugundua kuwa hata TAKUKURU (TAKUKURUNDO taasisi ya kuzuia rushwa ndogondogo) nao wanahusika pamoja na ofisi ya mwanasheria mkuu. Sasa wataweza kweli kushughulikia suala la BoT na mheshimiwa ndiyo hivyo hilo suala ameliweka mikononi mwao

Leo ni Throw Back Tuesday!
 
Ripoti ya time ya mwakyembe kuhusiana Na mchakato wa kampuni ya Richmond ndiyo ilipelekea Mzee lowasa kupewa aka ya fisadi. Kuna madai kwamba Kuna vitu havikusomwa siku Ile Dodoma hili kuficha aibu kwa serikali. Lakini pia,ripoti ilionyesha uhusika wa Mzee lowasa kwenye hili suala. Jana,lilitolewa ufafanuzi Na anayedaiwa kuwa mhusika mkuu
kukata mzizi wa fitina Na kuondoa suala la kutupiana mpira. Mwenye ripoti ya time ya mwakyembe atuwekee hapa,tusome tupate yaliyomo Na ukweli wake.
asante
 
Miaka imepita tangu Skendo ya Richmond ilipoanza kusikika midomoni mwa wengi na mtuhumiwa mkuu akiwa EL, maswali ambayo ninajiuliza na ambayo sijapata majibu hadi sasa ni haya; 1. Kwanini kamati haikumuhoji EL? ilikuwa bahati mbaya au kwa dhumuni fulani? 2. Kwa nini ushahidi wa El aliopewa spika haukuorodheshwa kwenye ripoti ya akina Mwakyembe?
Nini kilikuwa nyuma ya huu mchezo wote?
 
(16) Uhuru mkubwa ambao viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini waliutumia bila wasiwasi katika kuhakikisha kwamba kampuni waliyoitaka, Richmond Development Company LLC, inapewa zabuni ya umeme wa dharura; maelekezo ya mara kwa mara ya Waziri Mkuu kwa Wizara katika kila hatua ya mchakato huo; upendeleo wa dhahiri ambao Richmond Development Company LLC iliupata kutoka taasisi mbalimbali za Serikali k.m Kituo cha uwekezaji (TIC) ambacho kilifikia hatua ya kufumbia macho baadhi ya taratibu zake za msingi ili kuipa kampuni tanzu ya Richmond Development Company LLC cheti cha uwekezaji haraka iwezekanavyo; kutotimiza masharti ya Bodi za Makandarasi na Wahandisi na Wizara ya Nishati na Madini kuikingia kifua kampuni hiyo isichukuliwe hatua za kisheria; uteuzi wa mwisho wa Richmond Development Company LLC kuwa mkandarasi kufanywa na Waziri Mkuu mwenyewe tarehe 21 Juni 2006;

uamuzi wa kuiteua Richmond Development Company LLC kuwa mkandarasi kusafishwa na TAKURU ( sasa TAKUKURU) kuwa ulikuwa wa wazi na wa haki; uamuzi wa Serikali kuizuia TANESCO isivunje mkataba na kampuni hiyo licha ya sababu zote kisheria kuwepo, ni baadhi tu ya viashiria vya nguvu kubwa iliyo juu ya Wizara ya Nishati na Madini kutumika katika suala hili na Kamati Teule kutokana na ushahidi wa kimaandishi, kimazingira na wa mdomo, inaiona nguvu hiyo kuwa ni Waziri Mkuu.

Ibara ya 52 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inatamka wazi kuwa Waziri Mkuu ndiye mwenye madaraka ya juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ndiye Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni.

Kamati Teule haikufurahishwa hata kidogo na taarifa hizo zinazomgusa moja kwa moja Mhe. Waziri Mkuu katika kuipendelea Richmond Development Company LLC. Hata hivyo Kamati Teule imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge letu Tukufu.

Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mhe. Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge. Vile vile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake.
Kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Spika, kwa kumalizia Kamati Teule ya Bunge ilifadhaishwa sana na tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali ya kukaidi amri ya kuwasilisha nyaraka zinazohitajika na Kamati Teule. Kamati Teule inaliomba Bunge litafakari kitendo cha aina hii na kufikiria hatua za kuchukua dhidi ya watendaji wa namna hiyo.

Mhe. Dk. Harrison G. Mwakyembe
MWENYEKITI
KAMATI TEULE YA BUNGE
06 Februari 2008
 
mda si mrefu watu wataachwa uchi hapa..subirini mtaona..hv inaingia akilini kweli eti lowasa ale dili ya richmond peke yake bila mkuu wake kujua!?mwe subirini dondoo tulishapewa
 
(14) Pamoja na dharura iliyokuwa inalikabili Taifa, Serikali haiwezi kuwa kinara wa uvunjaji wa taratibu, kanuni na sheria za nchi kwa makusudi.

Kamati Teule imeanisha katika taarifa hii vitendo vya ubabe, ujeuri na kiburi vilivyofanywa na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini alimradi kampuni waliyoitaka iteuliwe kiasi cha kupindisha hata maamuzi ya Baraza la Mawaziri bila wasiwasi wowote, kukaidi ushauri wa kitaalamu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma mara tatu mfululizo na kinyume na maagizo ya Baraza la Mawaziri lililotaka Sheria ya Ununuzi wa Umma izingatiwe, kukiuka sheria kwa makusudi kwa kuingilia mchakato wa zabuni wa taasisi nyingine ya ununuzi, kuvipuuza vyombo vya ndani vya maamuzi vya TANESCO

(Bodi ya Wakurugenzi, Bodi ya Zabuni n.k), kuilazimisha Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuridhia maamuzi yaliyofanywa na Wizara ya kuibeba Richmond Development Company LLC kinyume cha sheria na taratibu n.k. Wizara hiyo katika kuibeba Richmond Development Company LLC ilifikia hatua ya kupotosha kwa makusudi ushauri wa Wizara ya Fedha uliozuia malipo ya awali ya Dola za Kimarekani Milioni 10 katika Barua ya Dhamana ya Benki ya Richmond Development company LLC. Siku iliyopotosha ilikuwa tarehe 6 Octoba 2006.

Kamati Teule inapendekeza kwamba Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo Mhe. Dk. Ibrahim Msabaha (Mb) na Katibu Mkuu Ndugu Arthur Mwakapugi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kwa makusudi kwenye mkataba na kampuni ya mfukoni ambao umesababisha hasara kubwa kwa nchi. Aidha Kamishna wa Nishati Ndugu Bashir Mrindoko naye achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu mpya wa Wizara kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC ambao ulijulikana dhahiri na Wizara toka mwaka 2004 kwenye mkataba wa Bomba la Mafuta. Ndugu Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua kampuni hiyo kusitisha mkataba wake na Serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa zabuni ya umeme wa dharura haujaanza.

Daaa itakuwa vizuri akamalizia na lile jina alilosema akilitaja ktk kashfa ya RICHMOND inchi itayumba. ..
 
lowassa alionewa sana, huyo Mwakyembe kama aliagiza mabehewa chakavu toka India mchakato ulikiuka sheria ya manunuzi
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom