Ripoti ya Pentagon 2020 kwenye Bunge la Marekani: Uchina ina jeshi kubwa la maji kuliko Marekani, Tanzania yatajwa

Huo utafiti na hiyo ripoti vimefanywa na Marekani wenyewe, unadhani baada ya kugundua hayo watakaa nayo tu bila kuifanyia kazi? Unadhani wao wenyewe hawajifanyii assessment ili ku improve?
Pamoja na yote, bado dunia inaitegemea sana Marekani ili kujua ukweli kuhusu yanayoendelea duniani. Maana wamewwkeza katika kuutafuta na kuujua ukweli hata uwe mzuri au mbaya kwao, mchungu au mtamu.
Unadhani taarifa hizi ungeweza kuzijua kupitia China?
Akili kama hii haipo ccm
 
Mkuu jana sio leo kila jambo na nyakati zake!
"We chose to go to the moon and do other things in this decade, not because they are easy but because they are hard" JF Kennedy speech Sept 12 1962 .
Given the two options Americans have a tendency to chose the hardest route over the simplest one ,it is ,in their spirit.
 
Tatizo mchina ni mchina tu ... mpaka kesho huko China magorofa yanaporomoka sasa sielewi hizo nguvu za kijeshi zinatoka wapi

Ni kweli Wachina ni Wachina ndio maana wamefakiniwa kuunda hypersonic missiles na glide vehicle wakati Marekani bado wanahaha ie hawana makombora hatari kama hayo, Uchina inefanikiwa kurusha roving vehicle mwezini yenye uwezo wa kupiga still colour pictures na video na kuzituma aridhini na cha kushangaza zaidi chombo hicho kilitua the other side of the moon ambayo hainekani Duniani - sasa swali ni: Wachina walifanikiwa vipi kuwezesha chombo hicho kutuma mawasiliano Duniani in real time wakati surface ya Mwezi ina block radio communucation! Miaka ya zamani Urusi iliwahi kutuma chombo chao kwenye orbit ya Mwezi kikazunguka na kupiga picha sehemu ya pili ya Mwezi lakini mawasiliano yalikatika mpaka chombo kilipo rudi upande ambao unaonekana Duniani - zoezi hilo LA Urusi ndilo liliwawezesha Wamerikani baadae na wao kutuma chombo chao kwenye moon orbit lakini hakikuwahi kutuma mawasiliano from the other side of the Moon - the questions is: how did Chinese succeed to maintain seamless communication na chombo Chao wakati kilipo tuwa kwenye other side of the moon? Halafu MTU anakuja na kejeri hapa eti Wachina ni Wachina!! China ndio Taifa pekee Duniani an independent orbiting station kwenye outer space, juzi juzi hapa Wachina wamerusha chombo cha kwenda kwenye Sayari ya Mars kinategemewa kufika katikati ya mwaka ujao, Wachina ndilo lilikuwa Taifa la tatu Duniani kulipuwa thermonuclear bombs in early 1960s - hivi sasa wanamiliki thermonuclear laden ICBM zenye uwezo wa kushambulia bara la Merikani pake itakapo bidi, wanamiliki vile vile aircraft carrier killer anti ship missiles zenye uwezo mkubwa wa kuzamisha carrier group nzima na hii haijarishi kama meli zenyewe zipo pwani ya Uchina au katikati ya bahari ya Pacific , in case war breaks out Amerika itapata hali ngumu sana kuwadhibiti Wachina na marafiki wake wa siri watakao wapatia Wachina a 200MT thermonuclear laden submarine drones za kumaliza kabisa Navy nzima ya Merikani na kuwakata ngebe, ukweli huo Uncle SAM anaujuwa sana we sema sikio LA kufa huwa halisikii dawa.
 
Pentagon wamepeleka ripoti yao ya mwaka 2020 kwenye bunge la Marekani kuhusu nguvu ya kijeshi ya taifa la Uchina.

Uchambuzi huo umezungumzia ukuaji wa kasi wa nguvu ya kijeshi ya taifa la Uchina tokea mwaka 2000 hadi 2020: Kuna mambo ambayo yameshangaza wataalamu wengi wa Marekani kwasababu wengi hawakutegemea kama yangetokea hivi karibuni tena kwa taifa ambalo miaka 70 nyuma lilikuwa ni masikini sana.

Ukisoma kurasa za mwanzo kabisa imethibitika kwamba taifa la Uchina ndiyo taifa lenye jeshi kubwa la majini kuliko Marekani, ambapo Uchina ana meli zisizopungua 350 (Ukijumlisha manowari za vita na nyambizi) huku Marekani akiwa ana meli zisizopungua 293 (Ukijumlisha manowari za vita na nyambizi).

Ikumbukwe tangu vita ya dunia iishe Marekani ndiyo taifa lilikokuwa na jeshi kubwa sana la majini ambapo hadi kufika mwaka 1985 alikuwa ana meli zisizopungua 600 kule bahari ya Pasifiki, hasahasa ukanda wa Mashariki ya mbali.

Upande mwingine ripoti inasema Uchina ana makombora aina ya (Ground Launched Ballistic Missiles) na (Ground Launched Conventional Missiles) zaidi ya 1,250 yenye kufika umbali wa kilomita 500 hadi 5,500.

Huku Marekani akiwa ana makombora aina ya (Ground Launched Ballistic Missiles) pekee yenye kufika umbali wa kilomita 70 hadi 300. Sambamba na hili Uchina ndiyo taifa lenye mfumo mkubwa na ulio bora wa makombora ya kujihami dhidi ya mashambulio ya angani (Surface to Air Missiles) ambapo wanasema mfumo huo umejumuisha mifumo ya kisasa ya Urusi aina ya S-300 na S-400.

Miaka sita nyuma niliwahi kusoma jarida moja likisema kwamba hadi kufika mwaka 2020 Uchina atakuwa na meli nyingi kuliko Marekani wengi walipinga na kusema kwamba hata kama Uchina atakuwa na meli nyingi basi haziwezi kuwa za kisasa kama za Marekani.

Hata kwenye hii ripoti naona bado wanasema kwamba Uchina ana manowari za kubebea ndege (Air-Craft Carrier) moja tu huku Marekani akiwa nazo kumi. Lakini nadhani hili halitasaidia kwasababu tofauti kabisa na Marekani, mkakati wa ulinzi wa Uchina uko tofauti kabisa.

Mpaka sasa sehemu nyeti kwa Uchina ni eneo la Bahari ya Uchina Kusini (South China Sea) ambako kuna visiwa anavyogombania na nchi kama Ufilipino, Vietnam, Malaysia na Brunei.

Na eneo la Bahari ya Uchina Mashariki (East China Sea) ambako kuna Taiwan ambayo Uchina anasema ni sehemu yake, pia na visiwa vya Diaoyu/Senkaku ambavyo wanagombania na Japani.

Kwasasa haya ndiyo maeneo nyeti sana kwa ulinzi wa Uchina, tofauti na Marekani ambaye maeneo yake nyeti kiulinzi ni kama Bara lote la Marekani (Western Hemisphere), Ulaya (Europe), Ghuba ya Uajemi (Persian Gulf) na Mashariki ya mbali/Ukanda wa Pasifiki (South-East Asia).

KWANINI UCHINA ANAWEKEZA SANA KWENYE JESHI LA MAJINI ???
Kwa hii nguvu aliyonayo Uchina sasa, kama siku ataamua kutanua misuli kwenye lile eneo au hata kuvamia Taiwan kijeshi sidhani kama Marekani na NATO watakuwa na uwezo wa kufanya lolote kumzuia Uchina.

Mwaka 1996 (Third aiwan Strait Crisis) Uchina chini ya JIANG ZEMIN walipewa somo gumu sana na Marekani pale alipotaka kuwafanyia fujo Taiwani kwa kuanza kulipua bandari zao.

Uchina alifyatua makombora na kupeleka manowari zake za kivita, lakini bahati mbaya uongozi wa Bill Clinton ulijibu mapigo kwa kupeleka manowari mbili kubwa za kubebea ndege (Aircraft Carriers) pamoja na meli kubwa za vita kule eneo la Pasifiki ili kumtishia Uchina kwamba hawezi kuvamia Taiwan kijeshi.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani wa wakati huo William Perry alimuita moja ya maafisa wa Ulinzi wa Uchina (Liu Huaqui) kumwambia kama wakiendelea hivyo basi watapata madhara makubwa sana kwamba "there would be grave consequences".

Uchina alidhalilika na alijifunza somo gumu sana kwamba kama akiendelea kuwa kwenye hali ile basi kile alichofanyiwa na Muingereza mwaka 1839 (The Opium Wars) au alichofanyiwa na Japan mwaka 1931 (The Invasion) of Manchuria kinaweza kujirudia.

Ukimsikiliza Raisi wa Uchina XI JINPING aliwahi kusema dhahiri kwamba Uchina lilikuwa taifa kubwa sana ambalo lilidhalilishwa na mataifa ya Magharibi hivyo hawatakubali tena.

Chama Cha Kikomunisti kimewekeza rasilimali nyingi sana kwenye mambo ya Ulinzi na wakiwa wazi kabisa kwamba adui yao mkubwa ni Marekani.

KUHUSU UHUSIANO BAINA YA TANZANIA NA UCHINA:
Ukisoma hii ripoti kuna sehemu wanasema Uchina anataka kutumia maeneo kama Tanzania, Pakistan, Sri-Lanka na Kenya kuwekeza kambi kubwa za kijeshi ili kupambana na Marekani.

Ina maana ile bandari ya Bagamoyo mbali na kuwa na faida za kiraia na kiuchumi ingekuwa na manufaa kiulinzi pia: Huu mkakati Chama Cha Kikomunisti kimeuita THE MILITARY-CIVIL FUSION STRATEGY, ambapo miundombinu ya kijeshi inaweza kutumika kwenye shughuli za kiraia za kiuchumi, pia vivyo hivyo kwa miundombinu ya kiraia (Dual Use).

Lakini ukisoma mwishoni kabisa mwa Ripoti utagundua kwamba jeshi la Uchina limekuwa likifanya mazoezi na mataifa mbalimbali dunia, ili kutekeleza mkakati wa Chama Cha Kikomunisti unaotaka hadi kufika mwaka 2049 Uchina liwe taifa lenye nguvu kuweza kupambana popote duniani huku likiwa na nguvu kubwa ya ushawishi kwenye siasa za dunia.

Katika mazoezi hayo ni nchi mbili tu za Afrika zilihusika mwaka 2019, Afrika Kusini na Tanzania. Huku jina la Mazoezi na Tanzania yakiitwa SINCERE PARTNERS-2019. Sasa kama hili ni jambo zuri au baya kwa Tanzania mimi binafsi sifahamu.

Ripoti: https://media.defense.gov/2020/Sep/...020-DOD-CHINA-MILITARY-POWER-REPORT-FINAL.PDF
Asee hata mm niliona aljazeera wakizungumzia hilo.
China ni taifa pekee mpinzani wa USA.
Nilikua natizama kipindi cha aljazeera kinaitwa "the coming war in china" ikielezea namna China kuanzia miaka ya 1930 alivyovunja utawala wa USA Asia mdogo mdogo mpaka sasa anaendelea kuvunja utawala wa dunia wa USA.
Ndio maana USA anamuundia tume ya makombora mazito China katika visiwa vya marshall island.
 
lakini tukumbuke wanasiasa wengi sana wa US wamepeleka technolojia yao uchina, hata viwanda vyao vingi wameviacha viende uchina hivyo kuipa china nafuu na nguvu ya kiuchumi............

pia, kulikua na taarifa kwamba kuna wanasiasa na wana usalama wa US walikua wanauza taarifa nyeti uchina, either direct au kwa kupitia 'wanafunzi' wa uchina waliokuepo US........

that being said, hii ripoti inawezekana ina malengo ya kisiasa..... a vote for biden is a vote for china!
 
Mkuu hizo porojo tu mbabe wa vita mbabe wa Majeshi ni Japan 🇯🇵 Asia yote. UN marekani mwenyewe wanalijua hilo hata jeshi lako JWT wanalijua hilo tafuta hii movies pearl harbor.huyo Mchina wako anaeweza kuwa na jeshi kubwa Lakin wanajeshi wake wengi wao ni vilaza
 
Ni kweli Wachina ni Wachina ndio maana wamefakiniwa kuunda hypersonic missiles na glide vehicle wakati Marekani bado wanahaha ie hawana makombora hatari kama hayo, Uchina inefanikiwa kurusha roving vehicle mwezini yenye uwezo wa kupiga still colour pictures na video na kuzituma aridhini na cha kushangaza zaidi chombo hicho kilitua the other side of the moon ambayo hainekani Duniani - sasa swali ni: Wachina walifanikiwa vipi kuwezesha chombo hicho kutuma mawasiliano Duniani in real time wakati surface ya Mwezi ina block radio communucation! Miaka ya zamani Urusi iliwahi kutuma chombo chao kwenye orbit ya Mwezi kikazunguka na kupiga picha sehemu ya pili ya Mwezi lakini mawasiliano yalikatika mpaka chombo kilipo rudi upande ambao unaonekana Duniani - zoezi hilo LA Urusi ndilo liliwawezesha Wamerikani baadae na wao kutuma chombo chao kwenye moon orbit lakini hakikuwahi kutuma mawasiliano from the other side of the Moon - the questions is: how did Chinese succeed to maintain seamless communication na chombo Chao wakati kilipo tuwa kwenye other side of the moon? Halafu MTU anakuja na kejeri hapa eti Wachina ni Wachina!! China ndio Taifa pekee Duniani an independent orbiting station kwenye outer space, juzi juzi hapa Wachina wamerusha chombo cha kwenda kwenye Sayari ya Mars kinategemewa kufika katikati ya mwaka ujao, Wachina ndilo lilikuwa Taifa la tatu Duniani kulipuwa thermonuclear bombs in early 1960s - hivi sasa wanamiliki thermonuclear laden ICBM zenye uwezo wa kushambulia bara la Merikani pake itakapo bidi, wanamiliki vile vile aircraft carrier killer anti ship missiles zenye uwezo mkubwa wa kuzamisha carrier group nzima na hii haijarishi kama meli zenyewe zipo pwani ya Uchina au katikati ya bahari ya Pacific , in case war breaks out Amerika itapata hali ngumu sana kuwadhibiti Wachina na marafiki wake wa siri watakao wapatia Wachina a 200MT thermonuclear laden submarine drones za kumaliza kabisa Navy nzima ya Merikani na kuwakata ngebe, ukweli huo Uncle SAM anaujuwa sana we sema sikio LA kufa huwa halisikii dawa.

Basically China has overtaken America militarily.
 
Kama unakumbuka ya Saddam ndo hayo hayo , pengine mchina anaundiwa zengwe kwa kuambiwa ana vitu ambavyo pengine kiuhalisia hata hana,
China haina nguvu kubwa Kama ilivyo Marekani au Russia kijeshi lakini China ni yenye nguvu kubwa Sana na NI dhambi kuifansnisha no na Iraq ya sadam
 
Pentagon wamepeleka ripoti yao ya mwaka 2020 kwenye bunge la Marekani kuhusu nguvu ya kijeshi ya taifa la Uchina.

Uchambuzi huo umezungumzia ukuaji wa kasi wa nguvu ya kijeshi ya taifa la Uchina tokea mwaka 2000 hadi 2020: Kuna mambo ambayo yameshangaza wataalamu wengi wa Marekani kwasababu wengi hawakutegemea kama yangetokea hivi karibuni tena kwa taifa ambalo miaka 70 nyuma lilikuwa ni masikini sana.

Ukisoma kurasa za mwanzo kabisa imethibitika kwamba taifa la Uchina ndiyo taifa lenye jeshi kubwa la majini kuliko Marekani, ambapo Uchina ana meli zisizopungua 350 (Ukijumlisha manowari za vita na nyambizi) huku Marekani akiwa ana meli zisizopungua 293 (Ukijumlisha manowari za vita na nyambizi).

Ikumbukwe tangu vita ya dunia iishe Marekani ndiyo taifa lilikokuwa na jeshi kubwa sana la majini ambapo hadi kufika mwaka 1985 alikuwa ana meli zisizopungua 600 kule bahari ya Pasifiki, hasahasa ukanda wa Mashariki ya mbali.

Upande mwingine ripoti inasema Uchina ana makombora aina ya (Ground Launched Ballistic Missiles) na (Ground Launched Conventional Missiles) zaidi ya 1,250 yenye kufika umbali wa kilomita 500 hadi 5,500.

Huku Marekani akiwa ana makombora aina ya (Ground Launched Ballistic Missiles) pekee yenye kufika umbali wa kilomita 70 hadi 300. Sambamba na hili Uchina ndiyo taifa lenye mfumo mkubwa na ulio bora wa makombora ya kujihami dhidi ya mashambulio ya angani (Surface to Air Missiles) ambapo wanasema mfumo huo umejumuisha mifumo ya kisasa ya Urusi aina ya S-300 na S-400.

Miaka sita nyuma niliwahi kusoma jarida moja likisema kwamba hadi kufika mwaka 2020 Uchina atakuwa na meli nyingi kuliko Marekani wengi walipinga na kusema kwamba hata kama Uchina atakuwa na meli nyingi basi haziwezi kuwa za kisasa kama za Marekani.

Hata kwenye hii ripoti naona bado wanasema kwamba Uchina ana manowari za kubebea ndege (Air-Craft Carrier) moja tu huku Marekani akiwa nazo kumi. Lakini nadhani hili halitasaidia kwasababu tofauti kabisa na Marekani, mkakati wa ulinzi wa Uchina uko tofauti kabisa.

Mpaka sasa sehemu nyeti kwa Uchina ni eneo la Bahari ya Uchina Kusini (South China Sea) ambako kuna visiwa anavyogombania na nchi kama Ufilipino, Vietnam, Malaysia na Brunei.

Na eneo la Bahari ya Uchina Mashariki (East China Sea) ambako kuna Taiwan ambayo Uchina anasema ni sehemu yake, pia na visiwa vya Diaoyu/Senkaku ambavyo wanagombania na Japani.

Kwasasa haya ndiyo maeneo nyeti sana kwa ulinzi wa Uchina, tofauti na Marekani ambaye maeneo yake nyeti kiulinzi ni kama Bara lote la Marekani (Western Hemisphere), Ulaya (Europe), Ghuba ya Uajemi (Persian Gulf) na Mashariki ya mbali/Ukanda wa Pasifiki (South-East Asia).

KWANINI UCHINA ANAWEKEZA SANA KWENYE JESHI LA MAJINI ???
Kwa hii nguvu aliyonayo Uchina sasa, kama siku ataamua kutanua misuli kwenye lile eneo au hata kuvamia Taiwan kijeshi sidhani kama Marekani na NATO watakuwa na uwezo wa kufanya lolote kumzuia Uchina.

Mwaka 1996 (Third aiwan Strait Crisis) Uchina chini ya JIANG ZEMIN walipewa somo gumu sana na Marekani pale alipotaka kuwafanyia fujo Taiwani kwa kuanza kulipua bandari zao.

Uchina alifyatua makombora na kupeleka manowari zake za kivita, lakini bahati mbaya uongozi wa Bill Clinton ulijibu mapigo kwa kupeleka manowari mbili kubwa za kubebea ndege (Aircraft Carriers) pamoja na meli kubwa za vita kule eneo la Pasifiki ili kumtishia Uchina kwamba hawezi kuvamia Taiwan kijeshi.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani wa wakati huo William Perry alimuita moja ya maafisa wa Ulinzi wa Uchina (Liu Huaqui) kumwambia kama wakiendelea hivyo basi watapata madhara makubwa sana kwamba "there would be grave consequences".

Uchina alidhalilika na alijifunza somo gumu sana kwamba kama akiendelea kuwa kwenye hali ile basi kile alichofanyiwa na Muingereza mwaka 1839 (The Opium Wars) au alichofanyiwa na Japan mwaka 1931 (The Invasion) of Manchuria kinaweza kujirudia.

Ukimsikiliza Raisi wa Uchina XI JINPING aliwahi kusema dhahiri kwamba Uchina lilikuwa taifa kubwa sana ambalo lilidhalilishwa na mataifa ya Magharibi hivyo hawatakubali tena.

Chama Cha Kikomunisti kimewekeza rasilimali nyingi sana kwenye mambo ya Ulinzi na wakiwa wazi kabisa kwamba adui yao mkubwa ni Marekani.

KUHUSU UHUSIANO BAINA YA TANZANIA NA UCHINA:
Ukisoma hii ripoti kuna sehemu wanasema Uchina anataka kutumia maeneo kama Tanzania, Pakistan, Sri-Lanka na Kenya kuwekeza kambi kubwa za kijeshi ili kupambana na Marekani.

Ina maana ile bandari ya Bagamoyo mbali na kuwa na faida za kiraia na kiuchumi ingekuwa na manufaa kiulinzi pia: Huu mkakati Chama Cha Kikomunisti kimeuita THE MILITARY-CIVIL FUSION STRATEGY, ambapo miundombinu ya kijeshi inaweza kutumika kwenye shughuli za kiraia za kiuchumi, pia vivyo hivyo kwa miundombinu ya kiraia (Dual Use).

Lakini ukisoma mwishoni kabisa mwa Ripoti utagundua kwamba jeshi la Uchina limekuwa likifanya mazoezi na mataifa mbalimbali dunia, ili kutekeleza mkakati wa Chama Cha Kikomunisti unaotaka hadi kufika mwaka 2049 Uchina liwe taifa lenye nguvu kuweza kupambana popote duniani huku likiwa na nguvu kubwa ya ushawishi kwenye siasa za dunia.

Katika mazoezi hayo ni nchi mbili tu za Afrika zilihusika mwaka 2019, Afrika Kusini na Tanzania. Huku jina la Mazoezi na Tanzania yakiitwa SINCERE PARTNERS-2019. Sasa kama hili ni jambo zuri au baya kwa Tanzania mimi binafsi sifahamu.

Ripoti: https://media.defense.gov/2020/Sep/...020-DOD-CHINA-MILITARY-POWER-REPORT-FINAL.PDF
Mkuu habari...
Nimeupitia tena huu uzi...
Je Uchina ina jipanga bado, maana kwa kitu kilichotokea wakati spika wa bunge la Marekani alivyo enda Taiwan Kwa nguvu ijapokuwa China ilikataa...
 
Dah!...uzi mzuri Sana wa mwaka huo....nadhani uvamizi wa Urusi huko Ukraine umezipa muda China, Taiwan na US kujitathmini kipi kitatokea iwapo mgogoro utazuka kati yao.
T14 Armata Mag3 dudus Yoda
 
China ina quantity ila haina quality. Uwezo wa jeshi la maji huwa tunaupima kwa displacement sio kwa idadi ya vessels. Iran ina speed boats na missile boats nyingi sana, unaweza jumlisha boats zaidi ya 100 ila ukijumlisha displacement yake ni sawa na Ticonderoga class cruiser moja ya Marekani.

Marekani inaunda meli kubwa chache, China inaunda meli ndogo ndogo nyingi hivyo lazima iwe na idadi kubwa. Na tulinganishe doctrines zao, wakati Marekani inaunda meli ziweze kutoka kwake kwenda kutunishiana misuli kona zote za dunia, China inaunda meli kulinda straits zake pale South China sea na Indian ocean. Hutoona meli za China karibu na Marekani ila kukuta meli za Marekani karibu na South Africa, Iran, Pakistan, Australia au popote duniani ni kawaida sana. Sasa huwezi kuwa na meli za kazi kama hiyo kisha ziwe ndogo. Linganisha aircraft carriers za Marekani na latest ya China.

Ila Navy ya China inakua haraka sana, tena hiyo report ni ya 2020 na niliisoma ila kwa mwaka huu speed ya ukuaji ni kubwa kuliko. Kuna destroyers tano zinaundwa kwa wakati mmoja sasa hivi kwenye shipyards za China.

Mkuu MALCOM LUMUMBA kesho Zhuhai Airshow inaanza ifuatilie. Kuna silaha mpya za China zitaonyeshwa na ndio nataka once and for all niamini nani mkubwa kati ya jeshi la Urusi na China
20221107_194205.jpg
 
Back
Top Bottom