Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Hatimaye ripoti ya ya CAG ya miradi inayosimamiwa na NSSF, imepelekwa kwa Rais Dk. John Magufuli kwa ajili ya kuipitia.
Awali ripoti hiyo ilitakiwa kuwasilishwa juzi kwenye Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge, baada ya wajumbe wa kamati hiyo kuiomba, lakini ilishindwa kuwasilishwa na viongozi wa NSSF kutokana na kuwepo tuhuma za ufisadi katika miradi mbalimbali ya NSSF.
Wajumbe wa kamati ya bunge ya Katiba na Sheria ilionekana wakiiulizia ripoti hiyo lakini, Waziri Jenister Mhagama, aliwaambia ripoti hiyo imetua mikononi mwa Rais Magufuli, hivyo hawawezi kuipata hadi aisome na kuiwasilisha bungeni.
“Kutokana na hali hii, kamati haiwezi kuipata ripoti hii hadi rais mwenyewe atakapoamua kuiwasilisha,”
Waziri Mugama amedokeza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Rais kuishughulikia ripoti kabla ya kupelekwa Bungeni kujadiliwa.
Wajumbe wa kamati walipinga na kuwataka watendaji wa NSSF waiwasilishe kwenye kamati hiyo kwa sababu wao ndio walioiomba ili waweze kuipitia na kuangalia utekelezaji wa majukumu ya NSSF.
Baada ya mvutano huo, Waziri Jenister alisisitiza taarifa alizonazo ripoti ipo kwa Rais, hivyo hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuipata hadi ipelekwe bungeni au atoe maelekezo mengine kwa kuwa yeye ndie mwenye kibali hicho kwa mujibu wa sheria.
Dau jiandae, Magufuli ameamua kuchukua ripoti aishughulikie yeye mwenyewe, badala ya kupitisha kwenye kamati za Bunge.
Chanzo: Mtanzania