'Ripoti' ya Mziray na Mabadiliko ya Chadema kuelekea 2010

Hapa sasa ndio patamu, hoja zije kujibiwa kwa hoja. Hoja hizi ni nzito na binafsi ningependa sana kufanya mahojiano na Bw. Mziray kwani yawezekana amefungua macho ya watu wengi sana, nikiwemo mimi.
 
Unaweza Kudanganya Watu Wachache Wakati Wote, Lakini Huwezi Kudanganya Watu Wote Wakati Wote (you Can Fool Some People Some Time But You Cant Fool All People All The Time), Mbowe Anapaswa Kujua Hilo.
 
Chadema kunani paleeee...........au ni annex ya CCM??sielewi..naona ukabila ukabila.....tuu kwenye nafasi zote zenye ulaji...hivi Tz tuna chama pinzani kwelii ambacho kikipewa uraisi kesho kinaweza kutuongoza.......kwelii nina mashaka..sana na ubinafsi....
 
Hapa sasa ndio patamu, hoja zije kujibiwa kwa hoja. Hoja hizi ni nzito na binafsi ningependa sana kufanya mahojiano na Bw. Mziray kwani yawezekana amefungua macho ya watu wengi sana, nikiwemo mimi.

Ala!!! kumbe nawewe hawavumi lakini wamo kwa usanii
 
Unaweza Kudanganya Watu Wachache Wakati Wote, Lakini Huwezi Kudanganya Watu Wote Wakati Wote (you Can Fool Some People Some Time But You Cant Fool All People All The Time), Mbowe Anapaswa Kujua Hilo.

And Yu kan not boili ani empti poti ekspekting supu!!!!!!!!!!!!!!!(yani huwezi chemsha chungu kitupu ukitegemea kupata mchuzi mrua)
 
Haya machaceh hapa chini so far ni maneno mazito sana kuhusiana na na hii ishu ya Chadema, na matatizo yake na Wangwe, kwa hiy hivi majuzi Wangwe alipoyasema haikuwa ni mara ya kwanza, yalishsemwa huko nyuma mpaka kuundiwa kamati liyotoa mapendekezo, lakini hayakufanyiwa kazi, unless kuna something I am missing hapa, au?

Kamati ilipewa hadidu za rejea zifuatazo:

i) Kuchunguza tuhuma za kuwepo ubaguzi ndani ya makao makuu ya chama.

2.0 MATATIZO NA MAFANIKIO

1. Kamati inashauri swala la uteuzi wa wabunge wa viti maalum katika siku za usoni uwepo umakini wa hali ya juu katika uteuzi wa viti hivyo kwa kuzingatia matakwa ya katiba ya chama na pia uwepo utaratibu wa ukomo wa vipindi vya mbele vya kuwa mbunge wa viti maalum.

3.0 Uteuzi wa nafasi za Wakurugenzi

Katika swala la uteuzi wa wakurugenzi waliohojiwa waliirifu kamati kuwa katika nafasi 8 za wakurugenzi, nne zinashikiliwa na watu wa mkoa mmoja wa Kilimanjaro (wachaga) kitu ambacho kamati katika uchunguzi wake imethibitisha.

Katika hili kamati inatoa maoni na mapendekezo kwamba nafasi zote za kazi katika chama zitangazwe ndani ya chama katika ngazi zote. Hii itasaidia kuweka wigo mpana katika uwiano wa kikabila, dini na jinsia miongoni mwa watendaji na kukifanya chama kuwa na sura ya kitaifa.

Pia kwa kufanya hivyo tutaweza kuwa na uhakika wa muombaji wa nafasi ya uongozi kama ni mwanachama mwenzetu, maana kamati imegundua katika uchunguzi wake yupo mtu aliyependekezwa na kuajiriwa ndani ya chama kabla ya kuwa mwanachama (Bi Regina Mrema) ambaye ni Mchaga kabila analotoka Mwenyekiti wa chama, FREEMAN MBOWE.
 
Kweli Mbowe alikuwa anahitajika kwenda kusoma na I hope kuna kitu amejifunza ambacho kitamfanya awe kiongozi bora na kuweza kukabiliana na matatizo ya uongozi.

Ila kama ameenda kusomea uongozi na bado anafanya haya madudu basi hapo kazi ipo kweli kweli.

Hivi CHADEMA mnahitaji kurundika wafanyakazi makao makuu? Huo ni mtindo wa CCM ambao wana mapesa ya kuiba BOT. Sioni umuhimu wa hizo kurugenzi na badala yake mungepeleka nguvu wilayani na mikoani.

Dawa hapa ni kushughulikia haya malalamiko kisha akina Wangwe watakosa cha kuongea. Mpaka sasa inaonekana anachosema Wangwe kinaungwa mkono na watu wengi tu ndani ya CHADEMA, sasa sijui mtafukuza wangapi?

Hata siku moja usije ukaficha report maana kuna siku itatoka nje tu, ni bora uitoe kwa muda unaoona unafaa, vinginevyo wajanja wataitoa kwa muda ambao ni pigo kwa chama.
 
Siku ya mbwa kufa pua zote zinaziba ,wao badala ya kushughurikia ripoti ya Mziray wao mhimu kwao wameikataa na atakayeendelea kuyasema kama Wangwe na apigwe chini.

Harafu kila anayetimka chama kwa namna moja ama nyingine tatizo ni Mbowe kunani Mbowe??
 
Baada ya kusoma tena na kuirudia ripoti hii, nimeona matatizo makubwa zaidi ndani ya ripoti yenyewe. Nina maswali yangu machache kwa Mziray au mjumbe yoyote yule aliyehusika kwa sababu kupokea tu na kuikumbatia siyo hekima bali kwanza kujiridhisha kuhusu masuala fulani. Mwitikio wetu usiwe wa hisia na vionjo bali wa mantiki na akili.

Madai yanayotolewa ni mazito sana na makubwa sana. Sasa ni wakati wa kuyachekecha kwa makini.
 
yes mkjj, hata mie ningependa kusikia maneno machache kutoka kinywani mwa bwana Mziray,,Otherwise hii issue ni nzito kwa chama kinachokua,
 
Watanzania wana akili bwana... walijua hawa jamaa inabidi wajifunze utawala kwanza... Mambo yanayotokea kwenye ofisi ya CHADEMA kiongozi mwenye uzoefu mdogo sana... anaweza kuya-sort out easily....

Hawa ndio wanaoona wengine hawajui, wazembe etc...
 
Baada ya kusoma tena na kuirudia ripoti hii, nimeona matatizo makubwa zaidi ndani ya ripoti yenyewe. Nina maswali yangu machache kwa Mziray au mjumbe yoyote yule aliyehusika kwa sababu kupokea tu na kuikumbatia siyo hekima bali kwanza kujiridhisha kuhusu masuala fulani. Mwitikio wetu usiwe wa hisia na vionjo bali wa mantiki na akili.

Madai yanayotolewa ni mazito sana na makubwa sana. Sasa ni wakati wa kuyachekecha kwa makini.

Mwanakijiji,

Mambo yote yaliyoandikwa kwenye hiyo report yamejadiliwa hapa kwa muda mrefu. Tofauti tu kwasasa ni kwamba yameanishwa na kamati ya CHADEMA yenyewe.

Swala la wabunge wa viti maalumu liko wazi mno, hapo ndipo palipoanzia matatizo mengi.

CHADEMA wangeshughulikia haya matatizo mwaka jana effect yake ingelikuwa ndogo sana kuliko hizi tuhuma za kila siku zinazozagaa sasa. Nina uhakika uchaguzi wa desemba una nafasi kwenye huu mgogoro wa sasa, ingawaje si ajabu hata CCM nao wako pembeni wakishangilia.
 
Baada ya kusoma tena na kuirudia ripoti hii, nimeona matatizo makubwa zaidi ndani ya ripoti yenyewe. Nina maswali yangu machache kwa Mziray au mjumbe yoyote yule aliyehusika kwa sababu kupokea tu na kuikumbatia siyo hekima bali kwanza kujiridhisha kuhusu masuala fulani. Mwitikio wetu usiwe wa hisia na vionjo bali wa mantiki na akili.

Madai yanayotolewa ni mazito sana na makubwa sana. Sasa ni wakati wa kuyachekecha kwa makini.

Kwi kwi kwi,

Nakuaminia mkuu... unajiandaa ku-spin... i wish hii report ingetoka CCM,,, najua ungekuwa mbogo... haya mkuu... yetu macho na masikio...

Wewe kama binadamu kama binadamu wengine... una-double standard sana mkuu!!!

Suala sio kumtafuta Mziray... issue iko rahisi... hiyo ripoti watakuwa wameiona viongozi wote. wa CHADEMA walioko hapa...

Swali ni moja tu... waulize waliiona hii ripoti? Kama wameiona basi waachie wanajamvi waijadili... badala ya kuleta za kuletwa mzee wangu.
 
last time watu tumeongea sana kuhusu kufukuzwa kwa wangwe na hoja zilizokua zikitolewa na wangwe,,,duh tulishambuliwa kama watoto,,sasa leo mambo hadharani na mie ninawahakikishia chadema kama hawatatatua matatizo na vikwazo vilivyopo basi chadema hakitenda popote,,,na mbowe atakua hana tofauti na Mrema
 
Watanzania wenzangu, matatizo ya uongozi tulionao ni ya jamii nzima... tukifikiri ni ya CCM, ya CHADEMA ya NCCR-Mageuzi tunajidanganya sana...

Viongozi wengi wa kisiasa ni wa kuchaguliwa ukiacha viongozi wachache wa wakutelewa! na hawa viongozi wanachaguliwa na wananchi...

Turudi nyuma tuchambue jamii yetu vizuri... badala ya kutumia muda mwingi kujadili vitu visivyokuwa na tija!!!
 
last time watu tumeongea sana kuhusu kufukuzwa kwa wangwe na hoja zilizokua zikitolewa na wangwe,,,duh tulishambuliwa kama watoto,,sasa leo mambo hadharani na mie ninawahakikishia chadema kama hawatatatua matatizo na vikwazo vilivyopo basi chadema hakitenda popote,,,na mbowe atakua hana tofauti na Mrema

Niambie baada ya uchaguzi wamefanya nini kama chama!!! ukiachilia mbali initiatives za viongozi wa CHADEMA binafsi (Zitto, Slaa etc)

Chama kimeimarishwa vipi!!!

Kibaya zaidi... mwandishi wa ripoti amesema hivi:

Pia palitolewa malalamiko kuwa ofisi ya Katibu Mkuu inatumiwa na watendaji isivyostahili kwa mfano watendaji huingia ndani ya ofisi hiyo ambapo wanatuhumiwa kufanya maongezi binafsi na marafiki zao wa kike.

Hii sio ishara nzuri hata kidogo... I'm sure Mzee Makamba hawezi ruhusu huu upuuuzi.
 
Baada ya kusoma tena na kuirudia ripoti hii, nimeona matatizo makubwa zaidi ndani ya ripoti yenyewe. Nina maswali yangu machache kwa Mziray au mjumbe yoyote yule aliyehusika kwa sababu kupokea tu na kuikumbatia siyo hekima bali kwanza kujiridhisha kuhusu masuala fulani. Mwitikio wetu usiwe wa hisia na vionjo bali wa mantiki na akili.

Madai yanayotolewa ni mazito sana na makubwa sana. Sasa ni wakati wa kuyachekecha kwa makini.

Ningekushauri kabla ya kumuuliza Mziray Ungeuliza kwanza ni nini na malengo yapi na kwanini na kwasababu zipi zilizowasukuma hao walioiunda hiyo kamati.Yani anza kuwauliza kwanza hao walioiunda kamati maswali hayo.
 
Haya machaceh hapa chini so far ni maneno mazito sana kuhusiana na na hii ishu ya Chadema, na matatizo yake na Wangwe, kwa hiy hivi majuzi Wangwe alipoyasema haikuwa ni mara ya kwanza, yalishsemwa huko nyuma mpaka kuundiwa kamati liyotoa mapendekezo, lakini hayakufanyiwa kazi, unless kuna something I am missing hapa, au?

Kamati ilipewa hadidu za rejea zifuatazo:

i) Kuchunguza tuhuma za kuwepo ubaguzi ndani ya makao makuu ya chama.

2.0 MATATIZO NA MAFANIKIO

1. Kamati inashauri swala la uteuzi wa wabunge wa viti maalum katika siku za usoni uwepo umakini wa hali ya juu katika uteuzi wa viti hivyo kwa kuzingatia matakwa ya katiba ya chama na pia uwepo utaratibu wa ukomo wa vipindi vya mbele vya kuwa mbunge wa viti maalum.

3.0 Uteuzi wa nafasi za Wakurugenzi

Katika swala la uteuzi wa wakurugenzi waliohojiwa waliirifu kamati kuwa katika nafasi 8 za wakurugenzi, nne zinashikiliwa na watu wa mkoa mmoja wa Kilimanjaro (wachaga) kitu ambacho kamati katika uchunguzi wake imethibitisha.

Katika hili kamati inatoa maoni na mapendekezo kwamba nafasi zote za kazi katika chama zitangazwe ndani ya chama katika ngazi zote. Hii itasaidia kuweka wigo mpana katika uwiano wa kikabila, dini na jinsia miongoni mwa watendaji na kukifanya chama kuwa na sura ya kitaifa.

Pia kwa kufanya hivyo tutaweza kuwa na uhakika wa muombaji wa nafasi ya uongozi kama ni mwanachama mwenzetu, maana kamati imegundua katika uchunguzi wake yupo mtu aliyependekezwa na kuajiriwa ndani ya chama kabla ya kuwa mwanachama (Bi Regina Mrema) ambaye ni Mchaga kabila analotoka Mwenyekiti wa chama, FREEMAN MBOWE.

Field Marshal

Angalia jinsi hawa jamaa walivyo wazushi na wazandiki. CHADEMA makao makuu hakuna afisa yoyote anayeitwa Regina Mrema. Sasa hii ni sehemu moja tu yenye uwongo wa dhahiri wenye kuchochea ukabila. Mnakumbuka hapa niliwahi kumzungumzia dada mmoja aliyekuja kwetu Zanzibar akiitwa Regia Mtema, huyu ndiye wanayemsema. Na masikini binti wawatu mwenye ulemavu lakini mchapa kazi kweli wala sio mchagga. Ni mtu wakutoka Morogoro. Hana asili yoyote ya uchagga. Mimi nimepata nafasi ya kuonana nae. Alikuja kwenye Kongamano la Wanavyuo na Vijana katika siku ya Muungano 26 Aprili ambapo CHADEMA waliliandaa hapa Zanzibar. Ni afisa mwandamizi ya vijana, ndiye anayefanya kazi badala ya John Mnyika.

Kuna mwenye ule mchango wa Paparazi Muwazi kuhusu hii ripoti? Maana aliichambua kweli kweli na kueleza asili yake. Mwenye link atuwekee. Sasa inaonyesha wameamua kujitokeza tena wazima wazima

Asha

Dada Asha, saidia wananchi wa Tanzania.

Je tume iliundwa? Je Mziray alikuwa kiongozi? Je ripoti hii iliwahi kutolewa? na Je kama sio hii hiyo tume ilitoa ripoti ya namna gani? Iko wapi? unaweza kuiweka hapa?

Je Madereva wanaotajwa wapo? Je upungufu wa komputa upo? Je wakurugenzi wanateuliwa? etc. etc. etc. etc....
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom