Ripoti ya Mrundikano wa watoto wa vigogo BoT (Benki Kuu) yatua mezani kwa Magufuli

Huyo Pamella Lowassa ameingia kwa sifa zake. Aliandika barua ya maombi ya kazi akaambatanisha na vyeti vyake. Kosa lake nini?
Tuwe na subira, report ya wafanyakazi wote wa BOT ipo mezani kwa rais , ataitolea maamuzi,,,, so stop worrying about her.
 
Hakuna jipya hapo..watu katika vyama wanawekana watoto,mahawara sembuse kazini,WATZ karibuni wote ndio tabia tuliyo nayo.
 
Sie tunataka maendeleo . Hao watoto wa wakubwa kama wana vigezo Kuna tatizo gani. Hayo majipu yametusaidia nini mpaka sasa . Hali mbaya mtaani watu wanatafuta ajira yeye anasema wapunguzwe.
Fisadi anapokamuliwa wengi hali zetu lazima ziwe mbaya.
 
Ukweli ni kwamba hao watoto wa vigogo wapo BOT kutokana na wazazi wao kushika nafasi mbali mbali serikalini. Hata kama wote wana sifa kwa nini wote wajazane BOT na agency nyingine nyeti za serikali?? Nna uhakika pia kwa hao watoto kuna ambao hawana sifa ya kuwepo hapo. Ila ngoja tuone mkuu wa kaya atakavyo-deal nao.
Ni kweli mkuu , yaan hao watoto wa vigogo ndio wanasifa za kufanya kazi BOT ????????????. watumbue tu Mkuu wa nchi.
 
BOT ina watumishi 1,391..balaaaaaaa tupu na ina matawi 5 tu... ni shida sana sana... NMB ina 150 Branches and is operated by 2,800 employees...!!! Cheki hiyo ratio sasa...!!

BOT ni jipu kubwa sanaaaa... wafanyakazi wamezidi hadi mara 3 zaidi...nadhani hadi aibu... FOR ME, JPM awapige chini hadi wabaki 500 tu...!! 500 bankers kwa 5 branches wanatosha sana tena ni wengi bado... so awafukuze hao 891...!! ❌❌❌❌❌⁉❌❌❌ tumbua kabisa 891..!!

ni wengi kupindukia..!! Kama SISIMIZI...!! KAZI KUTAFUNA FEDHA TU...!! ❌❌❌❌

Yaani nchi yetu imelemewa sana sana...!!
 
Hata yeye mbona amegawa madaraka kwa watoto wa kishua, John Mongela ambae ni mkuu wa mkoa wa Mwanza, vipi kuhusu Makonda, sio hisani ile? Hussein Mwinyi, January Makamba
Ongezea Vita Kawawa (mkuu wa wilaya)
 
Watanzania wamechoka kurukiwa na usaha....ni wakati sasa rais arushe maziwa na Asali.....tulimtuma atuletee Maisha bora....yeye kila siku anatuimbia kavumbua jipu.....majipu yake yametuchosha ...mbona wakati majipu yapo Maisha yalikuwa mazuri tu
kweli chief maisha skuiz yamekuwa yakusononeka tu
 
Watanzania wamechoka kurukiwa na usaha....ni wakati sasa rais arushe maziwa na Asali.....tulimtuma atuletee Maisha bora....yeye kila siku anatuimbia kavumbua jipu.....majipu yake yametuchosha ...mbona wakati majipu yapo Maisha yalikuwa mazuri tu
Ulikuwa una maisha mazuri kwakuwa ulikuwa unaishi maisha ya kuigiza ya kuiba pesa iliyopaswa kununua dawa ya mtoto aliyechini ya miaka mitano, wewe ukaikwapua. Sasa hivi kwanini maisha yabadilke wakati mshahara wako ni ulele?
 
Ukweli ni kwamba hao watoto wa vigogo wapo BOT kutokana na wazazi wao kushika nafasi mbali mbali serikalini. Hata kama wote wana sifa kwa nini wote wajazane BOT na agency nyingine nyeti za serikali?? Nna uhakika pia kwa hao watoto kuna ambao hawana sifa ya kuwepo hapo. Ila ngoja tuone mkuu wa kaya atakavyo-deal nao.


Mnasema tuu sababu hamjapata nafasi...ukipata nafasi utatamani mwanao awe sehemu nzuri...
 
Kila mzazi lazima amuandalie mtoto wake mazingira mazuri ya kusoma na kupata kazi so kama wanasifa sio tatizo tuache wivu je mzazi wako atakubali wewe usiwe na kazi nzuri wakati ana uwezo huo? Kama wamepata kazi hizo kihalali hskuna shida ila kama hawana sifa fagia woteeeeee
 
Mzee wa kuhamisha goli kazini, lakini hajui anachokifanya ni sawa na mtu Una matatizo unaona suluhisho ni kunywa pombe lakini pombe ikiisha shida iko palepale, anaweza kuhamisha goli kwa sasa kutoka ligumi hadi sukari kutoka sukari hadi ulevi wa kitwanga kutoka kitwanga hadi UDOM kutoka UDOM hadi BoT, haya yote tunayahifadhi ukifika muda muafaka tutachambua skendo moja hadi nyingine na iliisha vipi?

Ishu ya Lugumi inakufa pole pole
 
Ukiona Mkuu wa nchi anaitisha majina ya wafanyakazi ili ajue nani yupo na anafanya nini baada ya malalamiko ujue kuna walakini mkubwa hapo. Hiyo ndio kazi ya kupoteza muda wa rais wa nchi yenye matatizo lukuki hata sukari haipo madukani?
Kama anamwamini Gavana anashindwa nini kumuagiza atumie wataalamu waangalie establishment ya watumishi na kuondoa wasio hitajika kwa elimu zao na utendaji wao? Au hamuamini? Na kama hamuamini katika jambo kama hilo hayo makubwa ya BOT atamuaminije?
BOT watu washichunguzwe kwa majina yao kwa sasa bali kwa sifa za elimu na record za utendaji, makosa ya huyu mtoto wa nani hayana maana tena ila yasirudiwe.
Huwezi sema tunamfukuza fulani kwa sababu ni mtoto wa Kawawa wakati elimu yake inafit post aliyo nayo na utendaji wake ni mfano wa kuigwa, ila kasoro yake ni mtoto wa mkubwa.

Umeongea safi kabisa. Imekaa kulipiza visasi na wivu sijui.... kuna mengi ya kuangalia kwenye nchi hii zaidi ya kuhangaika na ajira za watu kisa watoto wa wakubwa. bora atumie neno lingine aachane na hili la watoto wa wakubwa maana linaleta matabaka. Mpaka 2025 kutakua kuna kazi sana. kufanya kazi kwa kutokuamini watendaji wako ni kujichosha na kujisababishia pressure zisizotakinana.
 
Aanze na ufisadi wa elimu kwanza, hasa suala la kilaza aliyethibitishwa jeska. Kutingisha kila taasisi kwa muda mfupi hakuongezi tija bali hofu na kuyumba kwa uchumi.

Najaribu kupitia comment za kipuuzi puuzi hivi ;hakika hii ni ya kwanza.
Hivi kichwa chako kina ubongo au kinyesi? samahani lakini
 
Tunataka ripoti ya kurudishwa wanafunzi wa UDOM na ile ya jesi-khaa!! Hii ina dharura kuliko hao unaowafata fata kwa kuhisi wana mishahara mizuri....badala ufatilie uchumi unafatilia majina ya watu....
Hii ni ya pili!!!
 
Blasia William Mkapa sio mtoto wa Mkapa namfahamu sana, ni majina tu kufanana hao wengine sijui lakini!
 
Hivi unamfukuza mtu kazi kwasababu ni mtoto wa fulani, amekosa vigezo au hajafuata utaratibu kupata ajira?

Mambo mengine yamekaa kijesi-kha jesi-kha tu.

Huyu naye!!! ................................//Team Vilaza
 
Back
Top Bottom