Ripoti ya Mrundikano wa watoto wa vigogo BoT (Benki Kuu) yatua mezani kwa Magufuli

Unajua hata kama kweli watu hao wana sifa na vigezo vya kufanya kazi ambazo wanadaiwa kuzifanya hapo Benki Kuu, kwa idadi yao hapo na unyeti wa sehemu yenyewe pamoja na nafasi za hao wazazi wao lazima tu kutasababisha watu waangalie uwepo wao hapo kwa jicho la shaka na kuhoji kama wapo hapo kutokana na ushawishi wa hao wazazi/ jamaa zao au la.

'Watoto wa vigogo' uwa wanasoma vizuri kuliko sisi ilo ni dhairi na kama umebahatika utajua wengi wanafwata nyayo za wazazi wao na uwa outstanding sasa mimi kama baba angu aliexcel mimi nisiexcel kisa baba angu ana jina tuache chuki tukaze na sisi tufike wanasiasa wasitugeuze viini macho ili tuwe upande wao.
 
Tunataka ripoti ya kurudishwa wanafunzi wa UDOM na ile ya jesi-khaa!! Hii ina dharura kuliko hao unaowafata fata kwa kuhisi wana mishahara mizuri....badala ufatilie uchumi unafatilia majina ya watu....

ilibidi nigonge like
 
Akiwafukuza hao, ile mishahara itatumika kuwalipa walimu ili wale wanafunzi 7000 warudi chuo, huwezi jua, yeye ni binadamu na anawashauri wake, pengine upo uwezekano wa kuwafikiria upya wale waototo, mana ukiangalia chanzo cha yote mpaka watoto wakafukuzwa kimeanzia kwenye malipo n.k. (ukosefu wa pesa), kwahiyo wacha serikali ipunguze matumizi kusaka pesa Zaidi na pengine wakafikiriwa upya wale watoto.[/Q
Wafanyakazi 1391 kwa BOT ni wengi sana, no wonder wengine hawaeleweki wanafanya kazi gani hapo. NMB tu yenye matawi nchi nzima haina idadi hiyo ya wafanyakazi

Commercial bank sio sawa na central bank am beginning to think wametumia reasoning kama yako
 
Ngabu kaka!!
Hili la BOT nadhani halijaja wakati muafaka!
Mkuu anapaswa amalizane na boliti lake kwanza! Hiki kibanzi hakipe muda, legitimacy ya kusimamia uadilifu inampotea kwa kuwa hajaweka sawa la kwake! Kila mmoja wetu hapa si mtakatifu na kwa mapungufu yetu tunaomba msamaha au tunaomba Mungu tupate kusitiriwa! Lakini si kwa viongozi wa nchi hii, wao likitokea soo, wana divert kwa hoja nyingine na sio kumaliza shida iliyopo!
No, not this time, yampasa ajue kuwa anapaswa kufanya jambo moja at a time! Sasa tumalizane na elimu kwanza, akimaliza hili ndio twende kwingineko!
KUTI KAVU TUMEKALIA,KADRI SIKU ZINAVYOZIDI KWENDA MIOYO YA WATU NA FIKRA ZINA HIFADHI HAYA,NA TUKIANZA NA WALE 7000?WAIT AND SEE AFTER 4YRS.
 
Mkuu, hi ishu ya kuwabaini hao wasiotumia majina ya ukoo sio ishu kubwa sana kwa TISS.

Wakiamua kuingia mzigoni ni siku mbili tu wanakuja na data za mpaka rangi ya bati la babu yako ikoje.

Na ninavyojua Magufuli hii ishu ya BoT lazima awahusihe TISS kwa 100%

Nafasi nyeti hazina budi kupatiwa vijana waliosomea nchini na isijalishe ni mtoto /watoto WA nani.
Vijana/watoto wa vigogo waliosomea nje us nchi ni mzigo mzito usio na tija,kinachofanyika ni kukopi na kupest procedures zinazorigharimu taifa.
 
Mzee wa kuhamisha goli kazini, lakini hajui anachokifanya ni sawa na mtu Una matatizo unaona suluhisho ni kunywa pombe lakini pombe ikiisha shida iko palepale, anaweza kuhamisha goli kwa sasa kutoka ligumi hadi sukari kutoka sukari hadi ulevi wa kitwanga kutoka kitwanga hadi UDOM kutoka UDOM hadi BoT, haya yote tunayahifadhi ukifika muda muafaka tutachambua skendo moja hadi nyingine na iliisha vipi?

Well said
 
Nilitaka nipitee tuu lakini nimeona kuna utata ktk maelezo ya mwandishi Wa Nipashe..John Nchimbi hajawai hakuwai kuwa Kigogo Wa Police..labda alitaka kumaanisha Emmanuel Nchimbi. Aliyewai kuwa Waziri Wa Mambo ya ndani na waziri..Hata ivyoo huyoo Kenneth ana sifa hajabebwaa...na kwa kumalizia Maguu afanyee yoote ila Pamela Amuwachee kwani Itaibua visa juu ya visasi.Pia Filbert amwache..Asijifanye kila jambo yy ndo Man Of the Show...Atakuja kunikumbuka maneno yangu si kila watu wanatumbuliwaa kirahisirahisi..kama waana Siifa!mbaya wawe Vilaza kama Jeeesikha!!!
 
Ila kweli, Hv ingekua ni wew uko juu alafu una watoto usingeweza kuwapachika hapo,. Tuongeeni ukweli, Tusione wengine ni malaika hawakosei, alafu sis ndo binadamu tunaweza kosea............

Ila hata hvo wamefanya vbaya naunga hoja
 
Sasa kama watu walikuwa na sifa za kuajiriwa? Yaani kuwa mtoto wa kigogo ni dhambi? Tunaelekea wapi hii nchi?
Sawa madam, lakini inapoonekana ni wao tu inatia Shaka.
Fursa za ajira hasa zile nyeti ni kwa ajiri ya Wote na si vinginevyo.
 
Hao watoto wa wanasiasa hapo hujaingia private sector, mimi ni field engineer upande wa power kwenye minara ya simu, ila nachoka ninapomshuhudia mtu ana elimu ya FORM 6 HGK anapiga drive test tena ktk kampuni kubwa ya simu, yote tisa kumi Kuna sista mmoja nae ktk kampuni hiyo hiyo ana certificate ya full secretarial service anapiga kazi za NOC engineer. Si shangai sana kwani ni nchi yetu ila nikiwafikiria jamaa zangu niliosota nao wengine wapo kitaa, wengine kazi mikataba yao haieleweki alafu unasikia mtu ambaye hana sifa anapewa kazi ROHO INAUMA nikifikiria msuli wa ENGINERING uliyokuwa tafu we acha tu. Alafu baadaye utawasikia maCEO wa makampuni wanalalamika wasomi wa Tanzania hawaajiriki, kumbe wamewaweka watoto zao na ndugu zao.
 
Hatimaye ile ripoti iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu inayotishia hatima ya ajira za watoto kadhaa wa vigogo ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imekamilika na kuwasilishwa mezani kwa Rais John Magufuli, Ikulu.

Inasemekana kwa sasa hali si shwari BoT, baada ya kuwepo tetesi za kupunguza watumishi ambao wengi ni watoto wa vigogo waliongia kwa migongo ya wazazi wao.
==========================

ib1.jpg

Akizungumza na Nipashe jana, Gavana wa BoT, Prof. Benno Ndulu, alisema maagizo ya Rais Magufuli juu ya kupitia upya ajira za watumishi wote wa taasisi hiyo yameshafanyiwa kazi na ripoti yake imekamilika.

Machi 10 mwaka huu, Rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza Makao Makuu ya BoT na kutoa maelekezo mbalimbali kwa menejimenti ya taasisi hiyo nyeti kwa mustakabali wa taifa kiuchumi.

Rais Magufuli alimuagiza Gavana wa BoT (Prof. Ndulu) kupitia upya ajira za watumishi wa taasisi hiyo na kupunguza idadi ya watumishi hao hasa ikibainika kuwa kazi zao zinaweza kufanywa na watu wengine.

Katika mazungumzo yake hayo na uongozi wa BoT, ilibainika kuwa benki hiyo ina watumishi takriban 1,391; idadi ambayo ilionekana kuwa ni ya juu kulinganisha na ukubwa wa taasisi hiyo na hivyo kumshangaza Rais Magufuli.

Wakati akizungumza na Nipashe jana, Prof. Ndulu alisema kazi hiyo (ya kupitia ajira za watumishi) ilishafanyika na ripoti yake imeshawasilishwa kwenye vyombo husika.

"Hiyo kazi ilishafanyika kama alivyoagiza Mheshimiwa Rais na tayari vyombo vinavyohusika vimeshapewa taarifa hiyo," alisema Prof. Ndulu na kuongeza:

"Hatutoi taarifa kama hizo magazetini bali kwenye vyombo husika--sisi tukishakamilisha kazi tunapeleka ripoti kwenye mamlaka husika na ndivyo tulivyofanya."

 AJIRA ZA WATOTO WA VIGOGO

Alipotembelea benki hiyo Machi, Rais Magufuli alisema anashangazwa kuwapo kwa wafanyakazi wengi ndani ya BoT ambao baadhi hata kazi wanazofanya hazijulikani wazi.

"Haiwezekani tukawa na kundi kubwa la wafanyakazi, wanalipwa mishahara wakati hata kazi wanazofanya hazijulikani," alinukuliwa Rais Magufuli.

Kabla ya ziara ya Rais Magufuli, majina kadhaa ya watumishi wa BoT yalikuwa yakiibua mijadala mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii kwa madai kuwa ajira zao zimetokana na kubebwa na wazazi ama ndugu zao ambao wana ushawishi mkubwa serikalini kutokana na nafasi mbalimbali walizo nazo au kuwahi kuwa nazo.

Orodha ya watu wanaodaiwa kuwa ni ya watoto wa vigogo, na ambayo Prof. Ndulu alisema siyo mpya kwani ilishaandikwa na kujadiliwa sana hapo kabla ni pamoja na Pamela Lowasa, anayedaiwa kuwa ni mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowasa.

Wegine ni Filbert Sumaye anayedaiwa kuwa ni mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu katika serikali ya awamu ya tatu, Fredrick Sumaye na Zaria Kawawa, anayedaiwa ni mtoto wa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya kwanza, Marehemu Rashid Mfaume Kawawa.

Mwingine ni Harriet Lumbanga anayedaiwa ni mtoto wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya tatu, Marten Lumbanga.

Aidha, orodha hiyo pia ina jina la Salama Ali Hassan Mwinyi anayedaiwa ni mtoto wa aliyekuwa Rais wa awamu ya pili, Alhaji Hassan Mwinyi; Rachel Muganda anayedaiwa ni mtoto wa aliyekuwa Balozi katika serikali ya awamu ya nne, Alexender Muganda. Salma Omar Mahita, katika orodha hiyo anadaiwa kuwa ni mtoto wa aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wakati wa utawala wa awamu ya tatu, IGP mstaafu Omar Mahita.

Wengine ni Justina Joseph Mungai anayedaiwa kuwa ni mtoto wa aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu na Utamaduni katika serikali ya awamu ya tatu, Joseph Mungai. Pia yumo Keneth Nchimbi anayehusishwa na kada wa CCM aliyewahi kuwa kigogo wa Jeshi la Polisi John Nchimbi. Blasia William Mkapa, anadaiwa kuwa ni mtoto wa Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkpa katika orodha hiyo yenye pia jina la Violet Phillemon Luhanjo, ambaye anadaiwa kuwa mtoto wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu kiongozi wakati wa serikali ya awamu ya tatu na nne, Phillemon Luhanjo. Liku Kamba anadaiwa kuwa mtoto wa aliyekuwa kada wa CCM wa muda mrefu, Kate Kamba.

Wengine wanaotajwa katika orodha hiyo ni Thomas Mongela anayedaiwa kuwa mtoto wa kada mashuhuri ndani ya CCM; aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwamo za ubunge, Getrude Mongela. Jina la Jabir Abdalah Kigoda linadaiwa kuwa ni mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika serikali ya awamu ya nne, marehemu Abdalah Kigoda.

Machi mwaka huu, mara baada ya agizo la Rais Magufuli kuhusiana na ajira za watumishi wa taasisi hiyo, Nipashe ilizungumza na Prof. Ndulu kwa njia ya simu kutaka kujua kama kweli orodha ya watoto hao ni miongoni mwa watumishi wa BOT na majibu yake kwa mwandishi, ambaye alimsomea majina hayo kuanzia mwanzo hadi mwisho, ni kwamba orodha hiyo 'haina jipya'. Prof.

Ndulu alieleza zaidi kuwa hakuna ubaya wowote kwa mtu mwenye sifa kuajiriwa na BoT, bila kujali jina lake. "Hayo majina kwani kwako wewe ni mapya? Mbona yameshaandikwa na kujadiliwa sana hayo--mimi nasema hakuna jipya hapo," alisema Profesa Ndulu na kuongeza:

"Hivi ukiwa na jina kubwa halafu ukiwa na akili ama sifa za kufanya kazi fulani, unataka kuniambia usipewe hiyo kazi kwa sababu una jina kubwa?"

 HOFU YATANDA

Licha ya ufafanuzi wa Prof. Ndulu kuhusiana na madai ya kuwapo kwa watumishi walioajiriwa kwa sababu ya ushawishi wa wazazi wao ambao ni vigogo serikali, bado mijadala mbalimbali iliendelea kutawala katika mitandao ya kijamii kuhusiana na orodha hiyo.

Aidha, imedaiwa kuwa hofu imetanda miongoni mwa watumishi hao na wengine wengi kutokana na kile kinachoelezwa kuwa huenda kukawa na punguzo kubwa la watumishi kutoka idadi iliyopo sasa ya wafanyakazi 1,391; jambo ambalo linaweza kutekelezwa wakati wowote kulingana na kile kilichomo ndani ya ripoti na kumfikia Rais Magufuli.

Wengi wa wachangiaji katika mitandao ya kijamii kuhusiana na majina ya watoto wa vigogo ni madai kwamba ajira zao zilitokana na ushawishi wa majina makubwa ya wazazi wao katika medani za uongozi nchini na siyo sifa za kuajiriwa kwenye taasisi hiyo na hivyo, upo uwezekano kuwa wengi miongoni mwao hawatasalimika pindi kazi ya kuwapunguza watumishi (wa BoT).

Source: Nipashe

NB: Mjadala kuhusu Ajira za Watoto wa Vigogo BoT ulijadiliwa kwa kina hapa JamiiForums mnamo mwaka 2008 | Soma: Watoto wa Vigogo na Ajira BoT

Kama waliajiriwa kihalali wana haki ya kuendelea kuwa kazini. Watanzania tumekuwa wa ajabu sana, ivi nchi hii baba/mam yako akiwa na cheo huruhusiwi kuomba/kupata kazi serikalini?
 
Kwingine na kwenye private sector pakoje?!
 
Back
Top Bottom