Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) 2020/21

Nchi ina madudu mengi sana cha ajabu viongozi nao wapo tu hawachukui hatua yoyoye wasubiri siku mi niwe rais ndio watajua sukuma gang ni nini
 
Hao wakaguzi wanaotumwa na CAG wanayoonesha tu maovu Kama ma 3 hivi Kati ya 100, Wana maisha mazuri kwa kupokea Rushwa wakati wa ukaguzi, madudu mengi wanaficha kwakuwa wanapewaga pesa huko wanapoenda kukagua , na pesa wanazolipwa ni hizo hizo Kodi za Wananchi. Hakuna kitu,

Hizo riport Zinazotolewa ni the best you can have, zoezi la ukaguzi ni zoezi la kupiga hela. Nyie mnapagawa na riport , je wakifanya kwa uwazi , wote mtaandamana hayo madudu

Nimemaliza.
Nimekuelewa kuwa inatakiwa kampuni ya kimataifa ije kufanya ukaguzi badala ya Cag
Na Hii itasaidia nchi kuwa na daraja zuri la kimataifa iwe rahisi kupata wawekezaji na mikopo
 
View attachment 2185789
Charles Kichere (CAG)
Hii ndiyo ripoti kamili ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere kwa Mwaka wa Fedha 2020/21, imewekwa hadharani Jumanne Aprili 12, 2022.

Baadhi ya mambo yaliyoguswa:

Mashirika ya Umma kutopeleka michango Sh bilioni 129.33
Mashirika ya umma manne mwaka 2020/21 hayakupeleka michango ya kisheria ya Sh. bilioni 129.33 kwenye mifuko ya pensheni, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kama inavyotakiwa. Hali hii ilichangiwa na ukosefu wa fedha.

Wanaume kupewa huduma za kujifungua
Nilipopitia taarifa za fedha za NHIF, nilibaini taarifa zinaonyesha wanaume wamepewa huduma ya kujifungua kwenye vituo vya afya.

TARURA kutelekeza miradi
Miradi ya barabara yenye thamani ya Sh. bilioni 1.9 imetelekezwa na TARURA.

Manunuzi nje ya mipango ya Serikali
Mamlaka za Serikali za Mitaa 24 zimefanya ununuzi wa bidhaa za Sh. bilioni 3.4 nje ya mpango wa ununuzi wa mwaka.

Mwingiliano majukumu TANROADS na TAA
Katika kufuatilia ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege, nimebaini kuna mwingiliano wa majukumu kati ya TANROADS na TAA kutokana na TANROADS kupewa mamlaka na majukumu yale yale yanayotekelezwa na TAA.

Upungufu wa walimu 16,577 (41%)
Tathmini ya uwiano wa walimu na wanafunzi katika mamlaka 48 za serikali za mitaa, ilibainisha kati ya walimu 40,458 wanaohitajika kwa shule za msingi walikuwepo walimu 23,881 tu ikimaanisha upungufu wa walimu 16,577 sawa na asilimia 41.

Serikai kulipa fedha kwa marehemu, waliofukuzwa
Mamlaka za Serikali za Mitaa 25 zimelipa fedha Sh milioni 556.8 kwa watumishi waliofariki dunia, waliostaafu na wasiostahiki. Ninapendekeza TAMISEMI izisimamie ipasavyo.

ATCL hasara imepungua kutoka Sh bilioni 60 hadi 36
CAG Charles Kichere: Mwenendo wa uendeshaji wa ATCL umeimarika. Kampuni imepunguza hasara kutoka Sh. bilioni 60 mwaka 2019/20 hadi Sh. bilioni 36 katika mwaka wa ukaguzi (2020/21).

Tsh bilioni 7 zimetumika vibaya Benki ya Maendeleo
Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema fedha za Mfuko wa Dhamana kwa Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati Sh bilioni 7 zilizopelekwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo hazikutumika kwa malengo ya kutoa dhamana kwa wahusika, zilitumika kwa matumizi ya kibiashara ya kibenki

#RipotiCAG2022 ya CAG imeonesha Sh milioni 917.342 za Mfuko wa Kilimo Kwanza na Sh 226,758,800 za Mfuko wa Taifa wa Pembejeo zilitumika kwa madhumuni mengine tofauti na yaliyokusudiwa

Amesema mikopo kutumika nje ya malengo ilitokana na mifumo dhaifu ya ufuatiliaji wa matumizi ya mikopo na uchambuzi wa sifa za wateja

Kuna upungufu wa Mawakili wa Serikali kwa 89%
CAG katika #CAGReport2022 amesema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambayo inahusika kusimamia, kudhibiti na kushtaki kesi za jinai Nchini kuna upungufu mkubwa wa idadi ya watumishi kwa asilimia 89, hiyo inachangia ucheleweshaji wa utoaji wa haki.

Kuna watumishi 661 tu badala ya 5890 sawa na upungufu wa asilimia 89 ya mawakili wa Serikali wanaohitajika, pia watumishi waliopo licha ya kuwa hawatoshi lakini hawakupangwa kulingana na uzito wa kazi katika Mahakama mahususi.

CAG: Miradi ya bilioni 7.68 imekamilika lakini haitumiki
Tathmini ya ufanisi wa utoaji wa huduma zilizokusudiwa kwa Miradi iliyokamilika imeonesha katika Halmashauri 30, miradi yenye thamani ya Tsh. Bilioni 7.68 ilikuwa imekamilika lakini haitumiki.

Hii imehusishwa na sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa umeme, kukosekana Wataalamu wa kuendesha Mifumo mbalimbali pamoja na idadi ndogo ya Watumishi.

Kuna upungufu wa mawakili wa Serikali kwa 89%
CAG katika #RipotiCAG2022 amesema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambayo inahusika kusimamia, kudhibiti na kushtaki kesi za jinai Nchini kuna upungufu mkubwa wa idadi ya watumishi kwa asilimia 89, hiyo inachangia ucheleweshaji wa utoaji wa haki.

CAG: Mtu mmoja apimwa damu mara 30 kwa siku
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema alipokagua taarifa za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa mwaka 2020/21 alibaini kuna mtu mmoja imeonekana katika Nyaraka zake za Hospitali kuwa amefanyiwa vipimo vya damu (Full Blood Picture) mara 30 kwa siku moja.

CAG: Iliyokuwa Manispaa ya Ilala haikupeleka bilioni 10.13 benki
Katika kaguzi maalumu 37 katika Halmashauri 36 Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alibaini kuwa jumla ya shilingi bilioni 19.72 zilikusanywa kutoka vyanzo mbalimbali lakini hazikupelekwa benki.

Kati ya fedha hizo , kiasi cha shilingi bilioni 10.13 ( asilimia 51) zinahusiana na iliyokuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ambapo shilingi bilioni 4.64 hakikupelekwa benki na mawakala 20 wakati kiasi cha shilingi bilioni 5.49 hakikupelekwa benki na watumishi 19 waliokuwa wakikusanya mapato.

Malimbikizo mishahara Mashirika ya Umma ni Tsh. Bilioni 2.72
CAG katika #RipotiCAG2022 amesema Malimbikizo ya Shilingi Bilioni 2.72 ya mishahara n madeni ambayo haijalipwa katika na taasisi zingine za umma ni shilingi bilioni 2.72, kuanzia mwaka mmoja hadi miaka saba.

Malimbikizo hayo ya madeni yanatokana na upandishaji vyeo wafanyakazi na mabadiliko ya mishahara, ajira mpya, uhamisho na mabadiliko ya mishahara kutokana na kuhuisha mifumo ya miundo ya utumishi.
CAG: Manispaa ya Temeke ililipa Tsh. Bilioni 2.16 kwa wananchi hewa 94
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ililipa Malipo ya Fidia ya Tsh. Bilioni 2.16 kwa Watu Wasiotambuliwa na Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Halmashauri hiyo kupitia kampuni ya uthamini, ilifanya uthamini wa maeneo kwa ajili ya fidia ya ujenzi wa miradi inayofadhiliwa kwa fedha za Benki ya Dunia.

Hadi Aprili 24, 2021 jumla ya Tsh. Bilioni 18.79 zilikuwa zimelipwa na Halmashauri ambapo wakazi 94 waliolipwa Tsh. Bilioni 2.16 hawakuwa wanatambulika na Viongozi wa Serikali za Mitaa yao.

Upigaji Tsh. bilioni 3.9 ndani ya BOT katika mfumo noti chakavu
CAG Charles Kichere ameweka wazi kuwa kuna hasara ya Tsh. Bilioni 3.9 ndani ya Beki Kuu Tanzania (BoT) iliyotokana na mchakato wa kubadili noti chakavu ambapo wafanyakazi sita wasio waadilifu ndiyo waliohusika na mchezo huo uliofanyika Januari 2017 hadi Desemba 2019.

Anasema ukaguzi ulitokana na maombi ya Naibu Gavana. “Noti chakavu ni noti halisi yenye kukosa sifa za kufanya malipo halali. BoT ilipokea noti za Tsh. bilioni 4.17 ili zitolewe noti mpya

“Tulibaini noti 1,427 zenye thamani ya Tsh. milioni 14.27 zilikuwa safi na zinafaa, zenye thamani ya Sh. 161.87m kweli zilikuwa chakavu, noti 399,392 zenye thamani ya Sh. bilioni 3.99 hazikuwa na vigezo vya kupewa noti mpya na zilipewa noti mpya kwa njia ya udanganyifu uliofanywa na maofisa wawili na watunza fedha wanne wa BoT,” - CAG

Ikiwemo kukata vipande vya note ya Sh 10,000 ili wapate noti mpya, kutotunza, daftari la wateja waliokuwa wanabadilisha fedha chakavu, na katika kitabu cha mahudhurio ya wateja kuna wateja 24 waliofika beki mara kwa mara kwa ajili ya kufanya miamala ya noti chakavu, wamehusishwa kushirikiana na wafanyakazi wa Benki Kuu kutekeleza mpango huo.

Amependekeza Gavana wa Benki Kuu achukue hatua stahiki za kinidhamu dhidi ya wafanyakazi wa Benki Kuu waliohusika katika ubadhirifu huu.

CAG: Wanafunzi wakopeshwa Tsh, bilioni 2.25 bila kukidhi vigezo
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere katika #CAGReport2022 amebaini udhaifu kwenye mikopo inayotolewa na Serikali kwa makundi tofauti ya kijamii

Kupitia ripoti yake ya ukaguzi wa ufanisi ameonyesha wanafunzi 756 wa elimu ya juu walikopeshwa Tsh. Bilioni 2.25 bila kukidhi vigezo vinavyotakiwa

Pia, Mfuko wa Taifa wa Pembejeo ukiwadhamini wajasiriamali 21 wasiokuwa na sifa kukopa Tsh bilioni 9.1, ambapo pia mfuko huo ulikopesha Tsh bilioni 4.6 kwa wateja wenye kumbukumbu zisizoridhisha
CAG anakuwa kama mganga wa kienyeji; “kuna mtu anakuroga” hakutajii ni nani anayrkuroga, kuna haja ya CAG kubainisha wahusika wa ubadhirifu wa fedha za umma kuliko kusema tu, “watumishi sita waliiba kiasi fulani cha pesa”. Funguka ili wachukuliwe hatua
 
CAG: WATAALAMU 320 WA AFYA HAWANA LESENI HAI HOSPITALI ZA RUFAA
CAG Charles Kichere amebaini kuwa wataalamu wa afya 320 kutoka hospitali tano za rufaa wanafanya taaluma yao bila kuwa na leseni hai za kitaaluma.

Hospitali hizo na idadi ya watumishi ambao hawana leseni ni Amana ya Dar es Salaam (71), Mbeya (25), Mbeya-Kanda (104), Temeke ya Dar (72), Tumbi ya Pwani (27) na Sekou Toure ya Mwanza (21).

Kichere amesema sehemu ya 16 (1) ya Sheria ya Famasia ya mwaka 2011 inatamka 'mtu hatastahiki kutoa huduma kama mfamasia isipokuwa kama amesajiliwa ipasavyo.
Hizi ni kawaida sana. Tz tumezizoea. Tunapeana machungu tu, hakuna lolote litakolofanyika. Mwakani tutasikia mengine zaidi.
 
Back
Top Bottom