Ripoti ya Mauaji ya Mwangosi yakera; Kamati ya Nchimbi hoi!

Communist

JF-Expert Member
Jun 1, 2012
5,400
1,181
  • MHADHIRI ASEMA SERIKALI IMEJIVUA NGUO

na Edson Kamukara

SIKU moja baada ya kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, kutoa ripoti ya uchunguzi wa mauaji ya mwanahabari, Daudi Mwangosi, huku ikikwama kuweka bayana kiini cha kifo hicho kutokana na kesi inayoendelea mahakamani, wasomi, wanaharakati, wanasiasa na wananchi wamepinga hatua hiyo.

Baadhi ya waliozungumza na gazeti hili waliiponda ripoti hiyo ya Kamati ya Dk. Nchimbi wakidai imeidhalilisha serikali na kuonesha mkanganyiko uliopo wa kujaribu kuwalinda polisi wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya raia.

Wadau hao pia walilisifu Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri (TEF) kutoka ripoti yao iliyojaa kila aina ya ukweli kuwa Mwangosi aliuawa na polisi kama picha za video na mnato zilizopigwa siku ya tukio zinavyojieleza wazi.

Wakati kamati ya Dk. Nchimbi katika uchunguzi wake ikidai kuwa nguvu iliyotumiwa na Jeshi la Polisi kutawanya wafuasi wa CHADEMA haikuwa sababu ya kifo cha mwanahabari huyo, wadau hao wameiponda wakisema ni aibu na kwamba hata wajumbe wake walionesha bayana kuwa walikuwa na aibu ya kuisoma.

Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Azavery Lwaitama, alisema kuwa ripoti hizo mbili ni nzuri kwani kwa mtu mwenye akili zake timamu anaweza kuona jinsi serikali ya Tanzania ilivyofika mbali katika mambo ya ajabu.

"Waziri Nchimbi ni bora asingeitoa ripoti hiyo maana inajichanganya kwa sababu haina maelezo ya kutosha kuhusu kile alichoahidi mapema kuwa hatua zingechukuliwa baada ya kamati hiyo kumaliza uchunguzi wake," alisema.

Alisema ripoti hiyo ni ya kijinga maana inaishia kauli tata za viongozi wasio na hatia badala ya kutaja bayana kuwa kiini cha mauaji hayo ni kuwazuia waandishi wa habari wasiwe wanaripoti mikutano ya CHADEMA na kuwadhibiti CHADEMA wenyewe.

Dk. Lwaitama alibainisha kuwa baada ya Waziri Nchimbi kupokea ripoti zote mbili, ni bora angekaa kimya na kuchukua hatua zaidi ya kuunda kamati nyingine ya kuwachunguza polisi.

"Polisi wameumbuka, maana hawakujua kama kuna picha zilikuwa zinapigwa na ripoti zote zimethibitisha ukweli kuwa lengo lilikuwa ni kuwazuia waandishi ili kuficha kile ambacho kingetokea kwa CHADEMA pale Nyololo," alisisitiza.

Alishauri kuwa Waziri Nchimbi angejijengea heshima kubwa kama angejiegemeza kwenye ripoti ya MCT, lakini katika kulinda vigogo wa polisi wasiumbuliwe ndiyo maana ikaandaliwa ripoti ya kuwasafisha.

"Kama si Mwangosi basi angeuawa Dk. Slaa maana hata TBC1 walishaanza kupotosha kuwa alikuwepo eneo la tukio ili kuhalalisha mambo ya ajabu ambayo polisi wangeyafanya. Sasa baada ya kuona mlengwa hayupo wakamgeukia Mwangosi wakielewa kabisa amerekodi mipango yao yote," alisema.

Dk. Lwaitama alifafanua kuwa kabla ya Mwangosi kuuawa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, alinukuliwa akimwambia kuwa ana kiherehere na askari mwingine akamwambia atakufa.

Alisema picha zinawaonesha watu saba wakimpiga Mwangosi na kisha kuuawa, lakini mahakamani kafikishwa mmoja tena anafichwa sura na kwamba Kamanda Kamuhanda bado hajaguswa wakati alishuhudia mpango mzima wa mauaji.

"Kuhangaika na ripoti ya Nchimbi ni kujipotezea muda, walifanya hivyo ili baadaye watoe sababu za kijinga za kupigwa na kitu chenye ncha kali, lakini picha zikawaumbua. Kama hawakuwa tayari kuyasema yaliyomo wangekaa na ripoti yao," alisema.

Naye mwanaharakati Deus Kibamba, aliliambia gazeti hili kuwa ameisoma ripoti ya MCT, lakini ya Waziri Nchimbi hakuhangaika nayo kwani waliipinga tangu mwanzo wakijua si halali kisheria.

Alisema kuwa Waziri Nchimbi alikuwa mtuhumiwa katika tukio hilo, na hivyo hakuwa na mamlaka kisheria kuunda kamati hiyo na kuongeza kuwa wajumbe wa kamati hiyo licha ya kuheshimika sana kwenye jamii, lakini kwa ripoti hiyo wamejitia doa kubwa.

"Watu wanakubali uteuzi kwenye tume na kamati hizo bila kuhoji maana wanatafuta maslahi kifedha. Kisheria Nchimbi hakupaswa kuunda kamati hiyo na hata MCT wao waliiunda kamati ya kimaadili si kisheria ndiyo maana tunaisifu ya kwao. Tulishasema tunahitaji tume ya kimahakama kuchunguza matukio haya wakatupinga," alisema.

Alisema kuwa Jeshi la Polisi walikwishaonesha kupishana kwa kauli kutokana na tukio hilo, kwamba Waziri Nchimbi alisema hawatamshtaki mtu hadi kamati imalize kazi, lakini wakati ikiendelea askari mmoja alifikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Mtatiro Julius, alisema kuwa Nchimbi aliunda kamati ya kuendelea kujilinda yeye, serikali na CCM kwani kusema polisi hawakutumia nguvu kumuua Mwangosi si kweli.

"Mimi ukiachilia ripoti hizo nimetazama video ya mauaji hayo na inaonesha wazi kabisa kuwa polisi walimuua Mwangosi kwa makusudi kwa kutumia nguvu nyingi ambazo hazikuwa na sababu," alisema. Aliongeza kuwa ripoti ya Kamati ya Nchimbi ni ya kupikwa, kuwalinda polisi kwani hata kumshtaki askari mmoja ni mkakati wa kukwepa wengine wasijekutajwa wakawajibishwa.

Naye Katibu Mkuu wa chama kipya cha ADC, Limbu Kadawi, alisema kwa ujumla ripoti hiyo ni aibu kwa taifa na Nchimbi mwenyewe, kwamba hata Jaji Ihema wakati anaisoma alikuwa akiona aibu.

Alisema wakati umefika kwa wananchi kujifunza kukasirika wanapoletewa mambo ya kijinga na aibu kama hayo. Kidawi alifafanua kuwa, hata waandishi walianza kugawanyika mapema tangu tukio hilo kutokea kwani katika maandamano yao pale Jangwani, baadhi walionekana kujikomba kwa Waziri Nchimbi wakati ndiye alikuwa akilaaniwa kwa askari wake kuua.

"Mauji ya Mwangosi yalikuwa wazi wala hayakuhitaji kamati hiyo kuchunguza maana askari wote walioonekana kwenye picha pamoja na kamanda wao Kamuhanda walipaswa kuwa wamekamatwa na kushtakiwa.
 
Nchi hii inaongozwa kwa miujiza tu! Ila ipo siku hawa akina Nchimbi watajilaumu kwa haya matendo. Hawana hata chembe ndogo ya kimaadili, yes you are trying to protect the government by any means but you should know how. Siyo kukurupuka hovyo!!
 
Hizi kamati/Tume ni chanzo cha ufisadi! zinatumia fedha za walalahoi! zinaleta output za hovyo hovyo!
 
Duhhh, hapa kodi yetu inaliwa na wajanja. Na haki sijui?
Hakuna siku nilijisikia kufedheheka kama siku ile nilipomuona Muheshimiwa Jaji na Nchimbi wakisoma report ile,kwa kweli nilijiuliza sana kuhusu uwezo wa Jaji yule na kamati nzima kwa ujumla.Ile kitu hata mimi wangeniambia nikachunguze ningeandika report nzuri na ya ukweli.Lile tukio lilikuwa wazi sana na facts zake ziko open,to be honest ile tume wamejidhalilisha na wamedhalilisha taaluma,walipokuwa wanaisoma nilikuwa na disgusting feelings as if namsikiliza mtu anayejaribu kushawishi audience kuwa kinyeshi ni mkate .
 
yani ni upuuzi mtu nacho washauri wa andishi wa habari juu ya hili nikuacha mara moja kuandika habari za jeshi la polisi, na nguvu zao nyingi wazipeleke kwa wapinzani na kuandika habari zao na kuiponda ccm iwe ni chukizo machoni pa wenye mwili,
 
Kwa matumizi mabaya ya madaraka na fedha za umma(kuunda kamati feki ya mwangosi),waziri nchimbi anastahili awafuate akina basil mramba na yona pale kisutu!
 
Huyu Nchimbi ndie aliesema hatutapata waziri kama yeye. katika ukurasa huuhuu niliandika ni kweli hatutapata waziri mpumbafu kama huyu si mmeona. bila aibu anasema eti ile ni ripoti. Sisi wananchitunayo ripoti yetu

  • :focus:

 
Kumbuka Nchimbi PHD yake ni ya ujanjaujanja sasa anataka kufanya ujanjaujanja ule ule katika mamabo serious,what a shame on CCM minister!!!
 
kaz ipo kwel kwel. REPORT; Polis hawakutumia nguvu kubwa kumuua Mwangos, kwahyo kutumia nguvu kias/ndogo inaruhusiwa?? REPORT; Polis hawakuhusika moja kwa moja, kwahyo aliyehusika moja kwa moja ni nan?? Picha zinaonyesha nin au zile ni fek.!?
 
Lengo la elimu ni kumkomboa mtu ili aweze kuepukana na utumwa ikiwemo utumwa wa kifikra. Lakini sielewi ni kwanini wanaojiita (au kuitwa) wasomi wa Kitanzania wanakubali kuwa watumwa wa wanasiasa.

Inawezekana vipi kwa msomi aliyebobea katika elimu ya sheria hadi kufikia hatua ya kupewa cheo cha Ujaji, afanywe mtumwa wa kifikra kwa kukubali kuuficha ukweli uliowazi kwa lengo la kulinda maslahi ya mabwana zake? Aibu kwake yeye mwenyewe na taaluma yake amefanywa mjinga naye akakubali kuwa mjinga, akatoa ripoti ya kijinga!
 
Watu wapumbavu kawaida hufanya mambo ya kipumbavu, nilikuwa natamani hata nisisikie hata huo ugoro wao
 
Kuuwa mwandishi kuna uhusiano gani na CHADEMA?Picha zinaonyesha polisi walimzingira na kuumuua mwandishi wakati wafuasi wa Chadema wamekwisha tawanyika, hivyo ni dhahiri kwamba polisi walimkusudia na hawakuwa na haja na wafuasi au viongozi wa CHADEMA.
 
Nchimbi + Duni+ ( )= CCM.
Guess who or what is in bracket.
.
 
hiv tangu lini mtuhumiwa akajichunguza afu yeye mwenyewe akaja akatoa majibu ya uchunguzi afu yawe fair?Nchmb alikua anacheza mchezo wa kuigiza ambao watazamaji wake wana akili kuliko anavofkir!shame on his report.
 
hatuna serikali tuna matatizo
hatuna waziri wa ulinzi tuna uwalo
nyama na wauaji wakubwa kikwete unaridhika na hili?
Ina maana tanzania haidhamini raia wake?
Kikwete unatakiwa ufunguke ripoti haina maana......
 
Back
Top Bottom