Tangia kuanza kwa swala mchanga wa dhahabu maarufu kama makinikia, tumeona makundi mbali mbali na watu tofauti tofauti wakialikwa pale Mh.Raisi anapokabidhiwa ripoti ya uchunguzi.
Kwenye ripoti ya pili kama ilivyokua ripoti ya kwanza, viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa dini, wazee,wanasiasa chama tawala na wale wa upinzani vuguvugu, wasanii wa muziki na Bongo Movie walialikwa.
Swali langu ni je Ikulu kupitia kamati yake ya mwaliko haijaona umuhimu wa kuwalika viongozi wastaafu hasa marais na mawaziri wakuu wastaafu hawa wa awamu ya tatu(3) na ya nne( 4) kuja kuungana na watanzania kusikitika pamoja juu ya upotevu wa rasilimali za nchi uliotipotiwa na hizi kamati mbili alizounda Rais??
Kilichojionesha wazi katika uwasilishaji wa hizo ripoti mbili ni masikitiko yaliooneshwa na Mh Rais, wajumbe wa kamati na (hasa wawasilishaji wa ripot), wageni waalikwa pale ukumbini na hata huku mtaani.
Hata kama itakua ni machozi ya Mamba lkn uwepo wao ungeongeza uzito sana na kuonesha tuko pamoja nao.