Ripoti ya maandamano ya Chadema wilayani Kahama mkoani Shinyanga.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti ya maandamano ya Chadema wilayani Kahama mkoani Shinyanga..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sexologist, Mar 1, 2011.

 1. sexologist

  sexologist JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 2,296
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 135
  Ndg wana jamvi.. Salam nyng kutoka Shinyanga..

  Leo nilikuwa mmoja wa maelfu ya waandamanaji waliojitokeza mjini Kahama.

  Watu walikuwa ni wengi haijawahi tokea.. Hali ya usalama ilikuwa tulivu sana, ilikuwa ni amani tu.. Viongozi wa CDM waliokuwepo ni Mh. Mbowe, Ndg. Mwita Waitara, M/kiti wa chama mkoa na wa wilaya, Mbunge viti maalum Manyara, Mweka hazina wa chama taifa na wengne sikuwatambua.


  Mabango yalikuwa ni mengi sana, na baadhi yake yalisomeka kama ifuatavyo:-
  "BORA UKIMWI KULIKO KIKWETE".. "TUNATAKA UMEME WA BUZWAGI".. "JK NA NGELEJA UZENI WAKE ZENU MUILIPE DOWANS".. "TUNATAKA KATIBA MPYA"... "TUNAPINGA KUPANDA KWA BEI YA BIDHAA" nk..

  Viongozi wote wa CDM waliokuwepo waliongea.. Mambo makubwa ni pamoja na kukubaliana kufanya maandamano mpaka Buzwagi kuwaambia wawekezaji waisaidie Kahama kimaendeleo.. Mh. Mbowe alitumia muda mwing kujibu hotuba ya JK ya jana.. Kikubwa alichosema ni kwamba maandamo ndio silaha pekee ya CDM kutumia nguvu ya umma kuikumbusha serikali wajibu wake kwa wananchi.

  Nashukuru.
  Naomba kutoa hoja.
   
 2. U

  Uswe JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  kila kitu nimekipenda, lazima tuwakumbushe. . .isipokua pale kwenye kuuza wake hapajanibariki sana
   
 3. j

  jerry monny Member

  #3
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks kwa ripoti ndugu,nguvu ya umma sio mchezo mpaka kieleweke.
   
 4. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,949
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  Safi mbumbumbu tuko pamoja. Hata lami ya jk ni ya hovyo
   
 5. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145

  Mabango mengine hayana maani na ni matusi kwa mkuu wa nchi, huwezi kusema JK auze mkewe ili alipe DOWANS huko ni kudhalilishana. Mbona maneno bado yalikuwepo ya kuandika katika mabango. Tukiendelea na mabango ya namna hii viongozi wa CDM watapunguza credibility yao kidogo.
  Sijafurahishwa na maneno niliyobold.

   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  ni kweli kwamba ni maneno makali sana lakini yote hiyo ni dalili za watanzania kumchoka jk, acha na yeye akereke kama wapambe wake mnavyo kereka...mbona yeye anatukana akina mama/watanzani kwa kuwaahidi bajaj..wakati serikali yake ina tenga mil 90 kwa kila mbunge na bil 94 za kuwalipa dowans wakati kwenye huduma za jamii hali ni mbaya kuliko unavyo weza kuielezea
   
 7. n

  nyantella JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mzee wa Rula,
  Nakubaliana nawe kabisa yaani Slaa ana simama jukwaani huku kuna matusi ya aina hiyo mbele yake, nahisi amekubali kwamba hatakaa awe rais wa nchi hii maana rais ni statesman, mstaarabu hata kama humpendi mtu kumtukana hadharani si ustaarabu!! mtu kasoma dini namna tulivyoona kwenye cv yake jana? ila upeo wake wa elimu kama ndio ule sijui kwanini aitwe Dr. anatakiwa aitwe Dkt na sii Dr. hana Phd hata ya dini according to the CV we saw jana, anaye bisha ailete! na kama ni kusoma phylosophy si lazima uwe Phd!!!. Mbowe tunaweza msamehe maana ndiyo lugha ya Bills. na Mh. Regia Mtema, wanawake wenzie wanatukana anaona poa tu, sawa pipoz pawa!!.
   
 8. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Cha kutafakari ni nini kimepelekea mpaka watu waandike ivyo bila uwoga na pia ujumbe umeshafika ila yote haya ni watu kumchoka na kumshusha heshima yake.
   
 9. sexologist

  sexologist JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 2,296
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 135
  Ni kweli hilo bango la kumwambia JK auze mke wake wengi hawakulipenda.. Kabla ya maandamano kuanza polisi walilikamata lakini baadae walimrudishia jamaa.. Nadhani waliamini ni hisia na mawazo binafsi ya huyo ndugu.. Na hli linachangiwa na hali halisi ya maisha.. Mpaka vijana wanakosa busara na hekma.. Tusiwalaumu! By the way Dr. Slaa hakuwepo, alikuwa Mbowe tu.. Na pia isingekuwa rahisi kwa viongozi wa CDM kusoma mabango yote.. TUSIWALAUMU JAMANI.
   
 10. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hizo zote ni kelele za mlango ambazo hazimzuii mwenye nyumba kupa usingizi tena ule usingizi mwololo.

  baada ya kashfa, kejeli, uchochezi katika mabango na maneno ya viongozi wa Chadema mwisho wake ilikuwaje?????

  Sisi tunasisitiza amani tu na si vinginevyo.

  Poleni sana Chadema
   
 11. m

  mams JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2011
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Watu wa aina hiyo wapo kila Chama. Mwaka jana kwenye Mkutano pale Jangwani Hadija Kopa mbele ya Kikwete alitoa single kumkashfu Dr Slaa eti Rais gani awe kwani alienda bafuni akaanguka akienda Ikulu si atafia huko! Wengi walishangilia na hata wangeguna tuu ingetosha, lakini lol!
   
 12. M

  Magezi JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  mtu yeyote mwenye akili timamu kama HM Hafif hawezi kumshanglilia kikwete....
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Labda amani unayoizungumzia ni ile ya kitandani.....vinginevyo umefulia
   
 14. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hafif uelewa wako hafifu kama jina lako mwenyewe sasa naanza kuamini majina yana reflect tabia za watu. Maana naona na wewe unaongea mipasho kama role model wako JK, eti kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala, kwa taarifa yako jk halali, si umesikia juzi kwenye hotuba yake alivyokuwa anatia huruma, na kama analala pamoja na kelele zote hizo basi ana walakini, acheni kumtia ujinga mwambieni aamke asikilize shida za watz ndio kazi aliyoitaka mpaka akaiba kura zetu. Mwambie aanzishe maandamano halafu tuhesabu watu wataohudhuria, lakini hawezi maana hata midahalo alikimbia wakati wa kampeni, aliulizwa kwa nini tz ni maskini akasema hata yeye anashangaa, muulize mtoto wa darasa la kwanza swali hilo leo atakujibu bilaa kusita, atakwambia ni ufisadi. Ndugu yangu vipi bwana
   
 15. j

  jerry monny Member

  #15
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanatakiwa waende mombasa wakatafute hiyo hela yakuwalipa dowans.sisi hatulipi tumegoma.
   
Loading...