Ripoti ya Kamati ya Madini ya Bomani

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,483
2,000
Wajumbe wa Kamati:-
1. Mhe. Jaji Mark Bomani- Mwanasheria Mkuu Mstaafu na Wakili wa Kujitegemea
2.Mhe. John M. Cheyo – Mbunge Bariadi Mashariki
3.Mhe. Iddi M. Simba – Mbunge Mstaafu Ilala
4.Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe – Mbunge Kyela
5.Mhe. Zitto Zuberi Kabwe – Mbunge Kigoma Kaskazini
6.Mhe. Ezekiel M. Maige – Mbunge Msalala
7.Bw. David Tarimo – Mshauri wa Kodi, Kampuni ya PricewaterhouseCoopers
8.Bw. Peter L. Machunde – Mwenyekiti Soko la Hisa la Dar es Salaam
9.Bw. Mugisha G. Kamugisha – Kamishna wa Sera, Wizara ya Fedha na Uchumi
10.Bi. Maria Kejo – Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Katiba na Sheria
11.Bw. Edward D. Kihunrwa – Mkurugenzi Msaidizi, Udhibiti na Usimamizi wa Uendelezaji Mijo,Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
12.Bi. Salome Makange – Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wizara ya Nishati na Madini.


Zaidi soma => ripotiyabomani.pdf
 

Attachments

  • File size
    792.8 KB
    Views
    98

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,410
2,000
Wajumbe wa Kamati:-
1. Mhe. Jaji Mark Bomani- Mwanasheria Mkuu Mstaafu na Wakili wa Kujitegemea
2.Mhe. John M. Cheyo – Mbunge Bariadi Mashariki
3.Mhe. Iddi M. Simba – Mbunge Mstaafu Ilala
4.Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe – Mbunge Kyela
5.Mhe. Zitto Zuberi Kabwe – Mbunge Kigoma Kaskazini
6.Mhe. Ezekiel M. Maige – Mbunge Msalala
7.Bw. David Tarimo – Mshauri wa Kodi, Kampuni ya PricewaterhouseCoopers
8.Bw. Peter L. Machunde – Mwenyekiti Soko la Hisa la Dar es Salaam
9.Bw. Mugisha G. Kamugisha – Kamishna wa Sera, Wizara ya Fedha na Uchumi
10.Bi. Maria Kejo – Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Katiba na Sheria
11.Bw. Edward D. Kihunrwa – Mkurugenzi Msaidizi, Udhibiti na Usimamizi wa Uendelezaji Mijo,Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
12.Bi. Salome Makange – Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wizara ya Nishati na Madini.

Sekretariati yenye wajumbe sita iliteuliwa kusaidia kazi za Kamati:-
1.Bw. Mathias B. Kabunduguru – Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti yaUtumishi wa Umma

2.Bw. Eliakim C. J. Maswi – Kamishna Msaidizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha na Uchumi

3.Bi. Sarah Barahomoka – Mkurugenzi Msaidizi, Uandishi wa Sheria, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

4.Dkt. Medard M. C. Kalemani – Wakili wa Serikali, Wizara ya Nishati na Madini

5.Bw. Shubi J. Byabato – Mjiolojia Mwandamizi, Wizara ya Nishati na Madini

6.Bw. Frank F. M. Lupembe – Afisa Kodi Mkuu, Mamlaka ya Mapato Tanzania.


SURA YA KWANZA
1.1 Utangulizi
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipitisha sera ya Madini mnamo mwaka 1997 kwa lengo la kuhakikisha kuwa sekta ya Madini inachangia ipasavyo katika pato la Taifa. Kufuatia kupitishwa kwa sera hiyo, Serikali iliwasilisha Bungeni Muswada wa Sheria ya Madini na kupitishwa mwaka 1998. Sheria hii ilikusudiwa kuweka misingi ya kisheria ya kufanikisha utekelezaji wa Sera ya Madini.

Takwimu zinaonyesha kuwa shughuli za uchimbaji mkubwa wa madini zimeongezeka kwa kuanzishwa migodi mikubwa sita mipya ya dhahabu kati ya mwaka 1997- 2007. Vile vile kumekuwa na ongezeko la shughuli za uchimbaji wa madini ya vito kama almasi na tanzanite. Aidha shughuli za uchimbaji madini zimeongezeka kutoka wachimbaji wenyeleseni wapatao 2,000 mwaka 1997 na kufikia takribani wachimbaji 7,000 mwaka 2007.Takwimu pia zinaonyesha mchango wa sekta ya madini umeongezeka kutoka 1.7%
mwaka 1997, na kufikia 3.8% mwaka 2006.

Miongoni mwa malalamiko ya wananchi ni pamoja na hali inayoonekana ya sekta ya madini kutochangia vya kutosha katika maendeleo ya nchi hasa ya kiuchumi na kijamii. Pia imeonekana kuwa mikataba ya madini inapendelea zaidi makampuni makubwa ya uwekezaji katika madini, huku kukiwepo na usiri mkubwa wa mikataba hiyo. Katika siku za karibuni, malalamiko makubwa zaidi yamekuwa juu ya mfumo wa kodi ambapo kumekuwa na hisia kuwa kampuni za madini hazilipi kodi kiasi cha kutosha,huku kampuni zote zinazojishughulisha na uchimbaji wa dhahabu na almasi zikidai hazijapata mapato yanayostahili kulipa kodi. Aidha, kumekuwa na lawama kuhusiana na wananchi waliohamishwa kutoka maeneo yao ya asili ili kupisha uchimbaji mkubwa kutolipwa fidia ya ardhi zao. Pia wananchi wanaotoka wilaya zenye migodi wanalalamika kutopata sehemu ya mrahaba licha ya maisha yao kuathiriwa na shughuli za uchimbaji wa madini katika maeneo yao.

Baadhi ya kero za wananchi ni pamoja na zile za mazingira ambapo inasemekana kuwa mazingira yanaharibiwa sana. Vile vile wafanyakazi wa kitanzania katika migodi wanalalamika athari za kiafya wanazopata na ujira mdogo kulinganisha na wafanyakazi wageni.

Baadhi ya wananchi wanalalamikia udhaifu katika usimamizi wa sekta, yakiwemo masuala ya usafirishaji wa mchanga wa dhahabu nje ya nchi, kuchenjuliwa na kutotolewa kwa taarifa sahihi za gharama za uwekezaji na uzalishaji. Vile vile kumekuwapo malalamiko makubwa ya wananchi kwamba viongozi wao wanafaidika binafsi kutoka kwa wawekezaji, zikiwemo tuhuma za rushwa katika mikataba.

1.2 Kuundwa kwa Kamati
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Jakaya Mrisho Kikwete aliona umuhimu wa kutathmini upya mfumo wa usimamizi wa sekta ya madini kwa mapana zaidi ili kunufaisha taifa pamoja na wawekezaji. Rais alionyesha dhamira hiyo katika hotuba yake ya kwanza kulizindua Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

Aidha, Mheshimiwa Rais alirudia kauli yake wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, tarehe 3 Novemba, 2007 mjini Dodoma. Tarehe 12 Novemba 2007, Rais aliteua Kamati aliyoahidi na kuipa miezi mitatu
kukamilisha kazi yake.

1.3 Majukumu ya Kamati
Kamati hii ilipewa majukumu yafuatayo: -
1. Kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zinazohusu migodi mikubwa;
2. Kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini;
3. Kupitia mfumo wa usimamizi unaofanywa na Serikali katika shughuli za uchimbaji mkubwa;
4. Kuchambua na kuainisha haki na wajibu wa mwekezaji na mwenye mali (Serikali);
5. Kukutana na Tanzania Chamber of Minerals and Energy” na wadau wengine ili kupata maoni yao;
6. Kutoa taarifa yenye mapendekezo.
7. Kupitia taarifa mbalimbali za Kamati zilizotangulia kuhusu sekta ya madini
8. Kumualika mtu yeyote mwenye utaalamu katika sekta ya madini ili kupata maoni yake; na
9. Kushauri juu ya mambo mengine yoyote yanayohusu sekta ya madini ambayo kamati itaona yanafaa.

1.4 Muundo wa Taarifa ya Kamati
Taarifa hiyo ina sura sita. Sura ya kwanza inahusu utangulizi. Sura ya Pili inaeleza hali halisi ya sekta ya madini; Sura ya tatu inaeleza maoni ya wadau mbalimbali; Sura ya nne inahusu uzoefu wa nchi nyingine katika kusimamia shughuli za madini; Sura ya tano inatoa tathmini, maoni na mapendekezo
ya kamati; na Sura ya sita ni Hitimisho.

Taarifa hii fupi ya kamati inaainisha baadhi tu ya mambo muhimu yaliyoko katika taarifa halisi ya kamati ya Rais kuishauri Serikali kuhusu usimamizi wa sekta ya madini.

SURA YA PILI
2.1 Hali halisi ya Sekta ya Madini
Katika Sura hii kamati inazungumzia kuhusu rasilimali ya madini na mchango wake katika maendeleo ya taifa, ambapo wameonyesha kulingana na kanzi data (data base) ya Wizara ya Nishati na Madini. Madini yanayoweza kupatikana nchini Tanzania yamegawanyika katika makundi matano:- Kundi la jamii ya madini ya metali linalojumuisha dhahabu, chuma, níkel, shaba, kobalti
na fedha; kundi la jamii ya vito linalojumuisha almasi, tanzanite, yakuti, garnets na lulu; kundi la jamii ya madini ya viwandani linalojumuisha chokaa, magadi soda, jasi, chumvi na fosfeti; madini yanayozalisha nishati kama makaa ya mawe na uranium; na madini ya ujenzi kama vile kokoto, mchanga na madini kwa ajili ya terazo. Mchanganuo wa hazina ya madini iliyothibitishwa nchini umeoneshwa katika jedwali Na.1 kama
ifuatavyo:-
Jedwali Na.1: Hazina ya Madini iliyothibitika
AINA YA MADINI
KIASI
Dhahabu
Tani 2,222
Nikeli
Tani milioni 209
Shaba
Tani milioni 13.65
Chuma (Iron Ore)
Tani milioni 103.0
Almasi
Karati milioni 50.9
Tanzanite
Tani 12.60
Limestone
Tani milioni 313.0
Magadi soda (soda ash)
Tani milioni 109
Jasi (gypsum)
Tani milioni 3.0
Fosfeti (Phosphate)
Tani milioni 577.04
Makaa ya mawe
Tani milioni 911.0
Chanzo: Geological survey of Tanzania, 2007
Pamoja na kuwepo hazina hii kubwa, Mchango wa sekta hii katika uchumi wa taifa na maendeleo
ya jamii unaonekana kutokidhi matarajio ya wananchi ikilinganishwa na sekta nyingine za uchumi.
Kwenye mapitio ya sera ya madini imeonekana kuwa kufuatia umuhimu wa sekta ya madini Serikali
ilipitisha Sera ya Madini ya Mwaka 1997. Madhumuni ya sera hii ni pamoja na kuchochea utafutaji na
uendelezaji wa uchimbaji madini, kuboresha uchimbaji mdogo wa madini na kupunguza umaskini,
kuimarisha miundombinu ya kijamii na kiuchumi, kuingiza fedha za kigeni na mapato kwa serikali,
kukuza na kuiendeleza Tanzania kuwa kituo cha vito katika Afrika na kuhimiza usalama na uhifadhi
wa mazingira.
Mwaka 1998, Serikali ilitunga sheria mpya ya madini na kuifanyia marekebisho Sheria ya Fedha za
Kigeni (The foreign Exchange Act, 1992) ili kukidhi mahitaji ya sekta ya madini na kuzingatia Sera
ya Madini ya 1997.
Ili kutekeleza sera hii sheria za kodi zimeweka vivutio mbalimbali kama ifuatavyo:-
2.1.1.
Kodi ya Mapato
Sheria ya kodi ya mapato ambayo ndiyo inatumika hivi sasa katika utozaji wa kodi ya
mapato ina vifungu maalum vinavyohusu utozaji wa kodi kwenye sekta ya madini.
Vifungu hivi ni kama kifungu cha 15(3) ambacho kinaruhusu fedha zinazokadiriwa
kwa ajili ya kuhuisha mazingira kukombolewa na kampuni baada ya kutekeleza
masharti. Kifungu cha 83(1)(a) kinazitaka kampuni kukata kodi ya zuio (witholding tax)
kutoka kwenye malipo yaliyofanywa kwa ajili ya huduma za menejimenti za kitaalamu
zilizotolewa kwa kampuni.
Hata hivyo baadhi ya vipengele vilivyokuwemo kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato ya 1973
iliyofutwa bado vinaendelea kutumika katika ukadiriaji wa kodi ya mapato kwa ajili ya
kampuni za madini. Kifungu Na. 145 cha Sheria ya Kodi ya Mapato ya 2004 kinaruhusu
kutumika kwa sehemu ya tatu ya jedwali la pili la sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka
1973 iliyofutwa.
Vipengele muhimu vinavyohusu utozaji wa kodi ya mapato na bado vinatumika ni pamoja
na:-
I.
Unafuu wa 100% wa gharama za uwekezaji katika ukokotoaji wa mapato
yanayotozwa kodi kwa mwaka huo.

II. Unafuu wa ziada ya 15% ya gharama za uwekezaji. Kampuni zenye mikataba na
serikali kwa ajili ya uwekezaji katika migodi (Mining Development Agreements
MDAs- Mikataba ya uendelezaji machimbo ya madini)
, iliyosainiwa kabla ya tarehe 1
Julai, 2001 zinaruhusiwa kukomboa ziada ya 15% ya gharama ya uwekezaji katika
migodi. Unafuu huu wa ziada hutolewa kila mwaka.
Athari kubwa ya kipengele hicho ni kampuni za madini kuchukua muda mrefu
kabla ya kuanza kulipa kodi au kutolipa kabisa na hivyo kuinyima Serikali mapato
yake.

III.
Unafuu wa kodi unaotolewa katika ukokotoaji wa mapato ya kampuni za madini
zinazoruhusiwa kukomboa gharama zote za uwekezaji na uendeshaji wa miradi
yote wanayoendesha bila kujali kama miradi yote wanayoendesha inachangia katika
mapato ya mwaka husika. Kwa utaratibu huo hakuna “ring fencing” kwa msingi wa
mgodi kwa mgodi.

IV.
Viwango vya kodi zuio (withholding taxes) vinavyotumika kwa kampuni
zisizokuwa na MDAs au zile zilizoingia MDAs baada ya tarehe 1 Julai 2001 ni
vile vilivyoainishwa kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004. Viwango vya kodi ya zuio vinavyotumika ni vya sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 1973iliyofutwa. Aidha, katika baadhi ya maeneo, viwango vilivyoainishwa kwenye Sheriaya Kodi ya Mapato ya mwaka 1973 havitumiki.
 

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,410
2,000
Hii ripoti naona kama ingezingatiwa basi haya yote yasingetokea. Tuna la kujifunza hapa kupitia ripoti za Jaji Bomani na hizi mbili za Magufuli.
 

KWEZISHO

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,530
2,000
Kumbe Dkt. Medard M. C. Kalemani alikuwa ni Wakili wa Serikali, Wizara ya Nishati na Madini!
 
  • Thanks
Reactions: Gut

Mp Kalix2

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
5,946
2,000
Wajumbe wa Kamati:-
1. Mhe. Jaji Mark Bomani- Mwanasheria Mkuu Mstaafu na Wakili wa Kujitegemea
2.Mhe. John M. Cheyo – Mbunge Bariadi Mashariki
3.Mhe. Iddi M. Simba – Mbunge Mstaafu Ilala
4.Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe – Mbunge Kyela
5.Mhe. Zitto Zuberi Kabwe – Mbunge Kigoma Kaskazini
6.Mhe. Ezekiel M. Maige – Mbunge Msalala
7.Bw. David Tarimo – Mshauri wa Kodi, Kampuni ya PricewaterhouseCoopers
8.Bw. Peter L. Machunde – Mwenyekiti Soko la Hisa la Dar es Salaam
9.Bw. Mugisha G. Kamugisha – Kamishna wa Sera, Wizara ya Fedha na Uchumi
10.Bi. Maria Kejo – Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Katiba na Sheria
11.Bw. Edward D. Kihunrwa – Mkurugenzi Msaidizi, Udhibiti na Usimamizi wa Uendelezaji Mijo,Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
12.Bi. Salome Makange – Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wizara ya Nishati na Madini.


Zaidi soma => ripotiyabomani.pdf

Kweli Kikulacho kinguoni mwakoMinerals: Many in hot soup
The list also includes former deputy AGs, Felix Mrema and Sazi Salula as well as the heads of the contracts department, Maria Kejo and Julius Malaba.

“ I hereby direct intelligence and security officials to summon all the individuals who have been mentioned in this report and interrogate them, as a preamble to taking appropriate legal actions,’’ he said.
 

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,410
2,000
Kumbe Dkt. Medard M. C. Kalemani alikuwa ni Wakili wa Serikali, Wizara ya Nishati na Madini!
Hakika mkuu, mikataba yote ya kifisadi atakuwa amehusika kwa namna moja au nyingine. Sema ni mteule wa Rais na Mwanachato.
 

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,287
2,000
Huyo Maria Kejo ndie Maria Ndossi?
JK alikuwa akinishangaza sana! Kwenye kashfa, huwa alikuwa akiunda Tume, halafu hiyo tume inajumuisha wanaolalamikiwa na wanaolalamika. Mwishowe wanamalizana wenyewe humo humo. Mfano hii ya madini Zitto aliwekwa, na huyo Mery Ndossy Kejo, Iddi Simba. Tulimshauri Zitto asikubali uteuzi kwenye hiyo kamati kama kweli haitaleta mabadiliko yoyote. Lakini wapi, naskia tu walipiga mkwanja wa hataree
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom