Ripoti ya IMF: Uchum wa dunia wazidi kudorora

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,492
9,266
Ripoti mpya ya robo mwaka kuhusu uchumi wa dunia inayotolewa na shirika la Fedha Duniani, IMF, imeonesha ukuaji mdogo wa uchumi kidunia huku ikionya kuhusu vita vya kibiashara, uwezekano wa kukosekana kwa mkataba wa Brexit na changamoto nyingine vinachangia kudorora kwa ukuaji wa uchumi.

Kwenye ripoti yake, IMF inasema kuwa mizozo ya kibiashara imepunguza kasi ya uwekezaji na kudorora kwa sekta ya viwanda, IMF ikitoa wito kwa mataifa kutotumia tozo kumaliza tofauti zao.

IMF sasa inasema uchumi wa dunia umeendelea kukua kwa kasi ndogo ambapo katika mwaka 2019 uchumi wa dunia unatarajiwa utakuwa kwa asilimia 3.2 na asilimia 3.5 kwa mwaka 2020.

Aidha shirika hilo limesema ikiwa hali ya sasa itaendelea kushuhudiwa mfululizo, basi huenda mambo yakawa mabaya zaidi kwa mataifa mengi na hasa yale yanayoendelea.
 
Kwani report yetu inasemaje? Wana ccm njooni huku IMF wametuchokoza tena.
 
CCM haina haja na report ya dunia wao wanamzuka na report ya Tanganyika tu ole wako useme toafauti na mwenyekigoda wao kuhusu zile 7% za ukuaji wa uchumi wa chama chao sorry nchi yao.
 
Back
Top Bottom