Ripoti ya Hali ya Uchumi Tanzania: Benki ya Dunia yapendekeza mfumo wa ncha 3 kupambana na COVID-19 na Mporomoko wa Uchumi

Sisi tuko uchumi wa kati, hayo matakwimu yao ya kibeberu wabaki nayo huko, sisi tuko vizuri wanatuobea wivu tu.

Au nasema uongo ndugu zangu
Hata hizo habari za uchumi wa Kati no kwa mujibu wa takwimu za beberu
 
Njia tuliyoamua kufuata kupambana na corona iliangalia zaidi kula yetu ya leo na si kesho. Sema tu sisi ni wazuri kwenye finger pointing, eti wewe upo short sighted
 
Nilivyoona comments zimekuwa chache hapa nikajua Uchumi umepanda....ambayo ni habari mbaya kwa kundi B!

Ukisikia uchumi umekua haina maana ni habari njema, kinachoangaliwa ni ukuaji wake kama upo positive ama negative

kabla ya 2015, uchumi ulikua kwa asilimia 6 na point zake means kama tulitaka kujiona tumeendelea ilipaswa tuingie kwe 7% kuendelea, mbali na hapo uchumi umekua in decreasing rates yaani negatively (mfano asilimia 5.9 ya 2019 ).

Hiki kitu kiuchumi si kitu cha kushangiliwa haswa kwa nchi iliyo na room kubwa ya ukuaji kama wetu
 
Naona kama swali la kama Tanzania kufikia uchumi wa kati je tumefikia malengo ya dira ya maendeleo ya 2025 limepotezewa.

kiufupi amejibu technically ili kuliepuka ila nakumbuka Kikwete aliliongelea katika speech yake kwenye msiba wa Mzee Mkapa .

Makadirio ya pato la mtu mmoja mmoja kulinganisha na pato la taifa (Per capital income) kama kigezo kikubwa, tayari lilikuwa limefikia pazuri kwa nchi kupewa status ya "lower middle income nation" toka mzee Kikwete alipoliacha..

Hivyo, ili kupima kama tupo vizuri kufikia malengo ya 2025 chini ya utawala huu, haitoangaliwa "status" ya nchi tuliyopewa bali kiwango cha Per capital Income kilichoongezeka toka 2015 v/s Target yetu v/s Ukuaji wa tawala zilizopita.

Hii ndio njia sahihi ya kupima peformance ya sasa, zilizobaki ni kelele ambazo sidhani kama zitaendana na uhalisia
 
Serikali ingeanza kutoa taarifa za maambukizi na vifo vitokanavyo na COVID 19 hii ingesaidia kujua hali halisi ya athari zitokanzo na janga hili.

Pia kutoa taarifa sahihi kuhusu hali halisi ya kiuchumi kuliko kuwaambia wananchi kuwa uchumi wetu umekua kwa kasi huku hali ya maisha ya mwananchi ikizidi kuporomoka.

Naona ipo haja ya serikali kupitia upya baadhi ya misimamo yake na kuibadili ili kisaidia wananchi kuepukana na janga la Corona na pia kuisaidia nchi iimarike kiuchumi.
Kwan ripoti ya WHO au WORD BANK?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je mwenendo wetu wa sasa katika sera na matendo ya kiuchumi haifuti hayo ya nyuma tuliyoyafanya kutufikisha hapa tulipo?
 
kiufupi amejibu technically ili kuliepuka ila nakumbuka Kikwete aliliongelea katika speech yake kwenye msiba wa Mzee Mkapa .

Makadirio ya pato la mtu mmoja mmoja kulinganisha na pato la taifa (Per capital income) kama kigezo kikubwa, tayari lilikuwa limefikia pazuri kwa nchi kupewa status ya "lower middle income nation" toka mzee Kikwete alipoliacha..

Hivyo, ili kupima kama tupo vizuri kufikia malengo ya 2025 chini ya utawala huu, haitoangaliwa "status" ya nchi tuliyopewa bali kiwango cha Per capital Income kilichoongezeka toka 2015 v/s Target yetu v/s Ukuaji wa tawala zilizopita.

Hii ndio njia sahihi ya kupima peformance ya sasa, zilizobaki ni kelele ambazo sidhani kama zitaendana na uhalisia
Mkuu kama sijakosea lengo letu ni dola 3000 naomba mchango wako
 
Sekta zilizochangia katika ukuaji wa uchumi.
1. Madini
2.Uwekezaji katika miundombinu
3. Huduma za fedha na mawasiliano.
4. Usafirishaji wa bidhaa.

Sekta hizi zinatumia mitaji mikubwa na idadi ya rasilimali watu katika sekta hizo ni ndogo kwasababu ya kutumia teknolojia ya mitambo zaidi.

Utalii umeshuka kwa mujibu wa ripoti. Kilimo kinachangia sehemu ndogo sana ukilinganisha na idadi ya watu walio katika sekta hiyo.

Mada fikirishi sana hii. Nangoja wadau waje tujadili.
 
Mkuu kama sijakosea lengo letu ni dola 3000 naomba mchango wako

tupo 1080 $ kwa 2020 na ukuaji wake ni chini ya asilimia 6 hivyo, sidhani kama kufikia 2025 tutakuwa tumefika hata nusu ya target iliyowekwa. Labda uchumi ukue kwa double digits (juu ya asilimia 10) kitu ambacho sioni kikitokea anytime soon unless mambo yabadilike
 
Sekta zilizochangia katika ukuaji wa uchumi.
1. Madini
2.Uwekezaji katika miundombinu
3. Huduma za fedha na mawasiliano.
4. Usafirishaji wa bidhaa.

Sekta hizi zinatumia mitaji mikubwa na idadi ya rasilimali watu katika sekta hizo ni ndogo kwasababu ya kutumia teknolojia ya mitambo zaidi.

Utalii umeshuka kwa mujibu wa ripoti. Kilimo kinachangia sehemu ndogo sana ukilinganisha na idadi ya watu walio katika sekta hiyo.

Mada fikirishi sana hii. Nangoja wadau waje tujadili.
Hapa hautawaona wachangiaji wengi. Karanga nakuomba utoe neno hapa. Waalike na wengine
 
Back
Top Bottom