Ripoti ya Haki za Binadamu: Haki za kiraia na kisiasa 2024 zilikumbwa na changamoto kama vurugu za wananchi, mauaji yasiyo ya kisheria nk

Ripoti ya Haki za Binadamu: Haki za kiraia na kisiasa 2024 zilikumbwa na changamoto kama vurugu za wananchi, mauaji yasiyo ya kisheria nk

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,153
Reaction score
15,425
Haki za kiraia na kisiasa nchini Tanzania mwaka 2024 zilikumbwa na changamoto mbalimbali zikiwemo vurugu za wananchi, mauaji yasiyo ya kisheria, mauaji yanayochochewa na imani za kishirikina, mauaji ya wenza wa karibu, kutoweka kwa watu, na adhabu ya kifo.

Pia kulikuwepo ukatili dhidi ya wanawake, watoto na makundi mengine, pamoja na changamoto katika usalama wa binafsi, upatikanaji wa haki, na mfumo wa haki ya jinai.

Haki ya kuishi iliathiriwa kwa kiwango kikubwa. Takwimu zinaonyesha matukio 500 ya vurugu za wananchi kila mwaka, ambapo 95% hutokea Tanzania Bara.

Tangu 2020, LHRC imeripoti matukio 36 ya mauaji yasiyo ya kisheria, huku matukio hayo yakipungua kidogo hadi 6 mwaka 2024.

Pia, matukio 12 ya mauaji yanayohusishwa na imani za kishirikina yaliripotiwa mwaka huo, wengi wa waathirika wakiwa wanawake.

Zaidi ya hayo, mashambulizi dhidi ya watu wenye ualbino yaliibuka tena baada ya ukimya wa mwaka mmoja, likiwemo tukio baya la kuuawa kwa mtoto wa miaka 2, Asimwe Novath, huko Kagera.

Hukumu 10 za kifo zilitolewa na Mahakama Kuu mwaka huo, na wafungwa zaidi ya 700 wanaendelea kusubiri kunyongwa.

Mauaji ya wenza wa karibu yalipungua hadi matukio 41, huku wanawake wakiathirika zaidi (88%).

Aidha, matukio 63 ya kutoweka yaliripotiwa katika mikoa mbalimbali.

Ingawa ajali za barabarani zimepungua kidogo, zaidi ya watu 500 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na ajali hizi, nyingi zikitokana na uzembe wa madereva.

Changamoto hizi zote zinaathiri kwa kiasi kikubwa haki za msingi za raia nchini.
 
Back
Top Bottom