Ripoti ya EPA Usanii: Ni Mpaka kikao Kijacho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti ya EPA Usanii: Ni Mpaka kikao Kijacho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mafuchila, Feb 13, 2008.

 1. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2008
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Baada ya hekaheka za Richmond Bunge kuendelea na kikao Ijumaa
  Na Waandishi Wetu, Dodoma

  BUNGE linaendelea na kikao chake Ijumaa, baada ya kuahirishwa kutokana na mtikisiko wa kuvunjika Baraza la Mawaziri, uliosababishwa na ripoti ya Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza mchakato wa ushindi wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kwa Kampuni ya Richmond Development ya Houston, Texas, Marekani.

  Spika wa Bunge, Samwel Sitta alisema jana kuwa, bunge litaendelea na shughuli zake kama kawaida kwa kuanza na kipindi cha maswali na majibu, kikifuatiwa na mjadala wa ripoti ya Richmond.

  Alisema bunge haliwezi kuahirishwa kwa sababu ya baraza jipya la mawaziri na kwamba, serikali ni mchakato sio mtu binafsi.

  Sitta alisema, bunge litaahirishwa kesho na haliwezi kuongeza siku kwasababu kuna ujio wa Rais George Bush na kuongeza kuwa, baadhi ya mambo ambayo yalipangwa kuwasilishwa kwenye kikao hiki, yatapangiwa kikao kijacho.

  Kuhusu ripoti ya EPA, alisema iko mikononi mwa serikali ingawa waliiomba itabidi kusubiri kikao kijacho, suala lingine ambalo litasogezwa ni Hoja binafsi ya vitalu vya uwindaji.

  Wakati huo huo, Kambi ya upinzani inatarajia leo kutangaza mabadiliko ya mawaziri vivuli.

  Taarifa zilizopatikana jana, zilisema hatua hiyo inatokana na baadhi ya wizara za serikali kupunguzwa, hali inayowalazimisha na wao kufuata mkondo huo.

  Mwananchi 14/02/2008
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ni tofauti ya mwezi mmoja tu .So wacha waruke ruke mwishowe watanasa kwenye tope sasa ni mwendo mdundo pekee .
   
Loading...