Ripoti ya CPJ: Kwa mwaka 2019 hadi kufikia Desemba 01 Waandishi wa Habari 250 walikuwa wamefungwa sehemu mbalimbali Ulimwenguni

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Idadi hiyo ni kwa mujibu wa Kamati ya Kutetea Waandishi wa Habari kupitia ripoti yake ya mwisho wa mwaka huku ikibainisha kuwa mwaka 2018 idadi hiyo ilikuwa Waandishi 255

China ni ya kwanza kwa kufunga Wanahabari 48 ndani ya mwaka huu huku Uturuki ikiwa nafasi ya pili ikiwa imefunga Wanahabari 47, Saudi Arabia 26, Misri 26, Eritrea 16, Vietnam 12 na Iran 11

Ripoti hiyo imeeleza kuwa idadi ya Waandishi waliofungwa China imeongezeka tangu pale Rais Xi Jinping alipoimarisha udhibiti wake wa kisiasa nchini humo

China imekuwa ya kwanza kwa mwaka huu na kuipita Uturuki ambayo katika ripoti ya mwaka jana ilikuwa imefunga Waandishi wa Habari 68

Aidha, idadi ya Waandishi wa Habari waliofungwa kutokana na kuandika "Habari za Uongo" imeongezeka kutoka 28 mwaka jana hadi 30 mwaka huu

2.PNG

Kujua zaidi, tembelea China, Turkey, Saudi Arabia, Egypt are world's worst jailers of journalists
*****

For the fourth consecutive year, at least 250 journalists are imprisoned globally as authoritarians like Xi Jinping, Recep Tayyip Erdoğan, Mohammed bin Salman, and Abdel Fattah el-Sisi show no signs of letting up on the critical media

China has imprisoned at least 48 journalists so far in 2019, more than any other country, displacing Turkey as the most oppressive place for the profession, a report by the Committee to Protect Journalists (CPJ) has said.

The report, released on Wednesday, noted that the number has "steadily increased since President Xi Jinping consolidated political control" in the Communist-ruled country.

"A crackdown in Xinjiang province - where a million members of [the] Muslim ethnic group have been sent to internment camps - has led to the arrests of dozens of journalists, including some apparently jailed for journalistic activity years earlier," the report said.

Besides China, Turkey, Saudi Arabia and Egypt are among the world's worst jailers of journalists, followed by Eritrea, Vietnam and Iran.

At least 250 journalists have been imprisoned for their work across the world as of December 1. According to the CPJ, a majority of jailed journalists faced anti-state charges.

However, the number of them charged with "fake news" rose to 30, compared with 28 last year, and one in 2012. Earlier this year, Russia and Singapore also introduced controversial anti-fake news laws.

Turkey, the second-worst country on the list, closed down more than 100 news outlets and imprisoned 47 journalists in 2019.

Instability and recent protests in the Middle East also led to a rise in the number of journalists jailed in the region.

Saudi Arabia arrested 26 journalists in 2019, putting it at par with Egypt as the world's third-worst jailer.

In Saudi Arabia, no charges have been disclosed in 18 of the cases, the CPJ report said. The watchdog said it is concerned over reports of "beating, burning and starving political prisoners, including four journalists".

In sub-Saharan Africa, of the 39 journalists jailed, 16 were in Eritrea, "where most have not been heard from for nearly two decades". Cameroon was the second-worst in the region.

In Asia, Vietnam was listed as the second-worst country after China, with 12 journalists jailed, while in the Americas, three journalists were put behind bars.

"The record number of journalists jailed for their work in recent years is a cause for alarm," said Courtney Radsch, CPJ's advocacy director. "Each one represents a case of censorship, not to mention a human being deprived of their rights."


To know more: China, Turkey, Saudi Arabia, Egypt are world's worst jailers of journalists
 
Idadi ya wanahabari wanaotupwa jela imefikia 250 kote duniani huku wengi wao wakizuiliwa nchini China. Kamata kamata ya wanahabari hao inafanywa na serikali zinazolenga kukandamizia uhuru wa vyombo vya habari

Kalamu, kitabu na vifaa vya mwanahabari haviko tena salama. Kwa mujibu wa ripoti ya kamati ya kuwalinda wanahabari iliyo na makao yake mjini New York, Marekani - CPJ, mataifa ambayo yametajwa kuwa hatari na yenye mazingira magumu ya kufanyia kazi kwa waandishi wa habari ni Uturuki, Saudia Arabia, Misri, Eritrea, Vietnam na Iran.
1576132080531.png


Wengi wa wale ambao wanahudumu vifungo gerezani wanakabaliwa na mashtaka ya kuipinga serikali ama tuhuma za kuandika habari za uongo. Kamati hiyo ya CPJ imesema kuwa imewahesabu waandishi wa habari wasiopungua 48 waliofungwa nchini China, idadi hiyo ikiwa mmoja zaidi ya mwaka 2018 wakati ambapo Rais Xi Jinping anaongeza juhudi za kudhibiti vyombo vya habari.

Takwimu hizo za CPJ zimeiweka China mbele ya Uturuki, ambayo iliwafunga waandishi wa habari 47 ikiwa ndiyo idadi kubwa kufungwa nchini humo katika muda wa miaka mitatu iliyopita, huku Saudia Arabia na Misri zikiwa katika nafasi ya tatu duniani kwa kuwafunga wanahabari 26 kila mmoja.

Mwandishi wa habari wa Reuters nchini Myanmar akiwa chini ya ulinzi
Nchini Saudia Arabia, hakuna mashtaka yoyote yaliyofunguliwa dhidi ya wanahabari 18 walioko kizuizini huku CPJ ikionesha wasiwasi kuhusu mateso wanayopitia wanahabari hao yakiwemo kupigwa, kuchomwa moto, na kunyimwa chakula.

Licha ya idadi ya waandishi wa habari waliofungwa nchini Uturuki kupungua kutoka 68 ya mwaka uliopita hadi 47 mwaka huu, haimaanishi kuwa hali ya utendajikazi nchini humo kwa wanahabari imeimarika, ripoti ya CPJ imesema.

Ripoji ya CPJ inaongeza kuwa juhudi za rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan zimefanikiwa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari hasa kuzima wanahabari wanaoandika habari za ukosoaji wa serikali.

CPJ imesema kuwa serikali ya Uturuki imefunga zaidi ya vituo 100 vya habari na kuwabandikia mashtaka ya ugaidi wafanyakazi kwenye vituo hivyo. Hatua hiyo imewakosesha kazi wanahabari wengi na imetafsiriwa kama mbinu ya kuwatisha.

Ripoti ya CPJ pia imesema utawala wa kimabavu, ukosefu wa utulivu na maandamano ambayo yamekuwa yakifanyika katika eneo la Mashariki ya kati kumesababisha ongezeko la idadi ya wanahabari waliofungwa katika eneo hilo.

Wanaharakati wanaotetea haki za wanahabari wanahoji kuwa idadi ya wanahabari 250 waliofungwa bado iko juu na yenye kutia hofu japokuwa idadi hiyo iko chini tofauti na wanahabari 255 waliofungwa mwaka 2018 na 273 mwaka 2016.

Chanzo: DW Swahili
 
Madikteta hawawezi kuwa na amani, tunaona masaibu yanayomkuta Al Bashir leo.
 
Back
Top Bottom