Ripoti ya CAG Prof. Assad, mtihani mzito kwa Raisi, Bunge na Katiba

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,225
2,000
RIPOTI ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ipo njia moja kuelekea Bunge la Jamhuri ya Muungano, lakini je, itafikishwa? Na ikifikishwa itasomwa? Halafu ikishasomwa?

Ripoti hiyo ipo kwenye kituo cha kwanza (kwa Rais John Magufuli), kituo chake cha pili ni Bungeni. Lakini ripoti hiyo imeandaliwa na Prof. Mussa Assad, mkuu wa taasisi hiyo (CAG) ambaye bunge limegoma kufanya kazi naye.

Hapa ndipo hoja ya Dk. Benson Bagonza, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Doyosisi ya Karagwe inaibuka, "Kama Rais Magufuli ataipeleka ripoti hiyo bungeni, atakuwa amelipuuza Bunge na kama hatoipeleka atakuwa amevunja Katiba ya Nchi".

Prof. Assad anatambua hilo, naye tayari ametoa tahadhari kwamba, mgogoro unaweza kuwa mkubwa kutokana na uamuzi wa Bunge kumtenga huku ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2017/18 ikiwa tayari imeandaliwa.

Ndani ya siku saba, baada ya bunge kuanza kuketi tarehe 2 Aprili 2019, ripoti hiyo inapaswa kufikishwa bungeni na kusomwa.

Job Ndugai, Spika wa Bunge, jana tarehe 4 Aprili 2019 alisema kuwa, Ripoti ya CAG ya mwaka 2017/18 haijafika mikononi mwake, kwa lugha nyingine ni kwamba, "Bado ipo Ikulu"

Ni kwa kuwa, Prof. Assad alisema tayari ameshaikabidhi ripoti hiyo kwa Rais Magufuli na kwamba, kinachosubiriwa kwa sasa ni kuwasilishwa bungeni kama inavyoelekezwa na Katiba na sheria za nchi.

Ni kwa mujibu wa Ibara ya 143(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ambapo inamtaka CAG kuwasilisha kwa Rais kila taarifa atakayotoa.

Kwa mujibu wa ibara hiyo, baada ya Rais kupokea taarifa hiyo, atawaagiza watu wanaohusika wawasilishe taarifa hiyo kwenye mkutano wa kwanza wa Bunge, utakaofanyika baada ya rais kupokea taarifa hiyo.

Na kuwa, ripoti hiyo itapaswa iwasilishwe katika mkutano huo kabla ya kupita siku saba tangu siku kikao cha bunge kilipoanza.

Maana yake ni kwamba, ripoti ya CAG inapaswa kuwasilishwa bungeni kabla ya Alhamisi ya wiki ijayo.

Spika Ndugai alikutana na waandishi wa habari jana ambapo miongoni mwa maswali aliyoulizwa, ni kwamba, ameishapokea ripoti ya CAG ya mwaka 2017/18 iliyosainiwa na Prof. Assad?
“Bado” ndivyo alivyojibu na kwamba, haoni sababu ya kueleza kama mhimili huo wa kutunga sheria utapokea ripoti hiyo na kuifanyia kazi ama la!

Hata hivyo Spika Ndugai alisisitiza kwamba, Bunge halifanyi kazi na Prof. Assad na kwamba,halijakataa kufanya kazi na Ofisi ya CAG.

Spika Ndugai anasema, walikwazwa kwa kauli ya Prof. Assad kwamba, Bunge ni dhaifu wakati Bunge hilo ndio linashirikiana naye kwa kiwango kikubwa na ofisi yake inashiriki katika utekelezaji wa shughuli za chombo hicho cha kutunga sheria.

Jumanne wiki hii, Bunge lilipitisha azimio la kutofanya kazi na Prof. Assad baada ya Kamati yake ya Kudumu ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwasilisha taarifa kuhusu shauri dhidi yake kwamba, alilidharau bunge.

Lakini je, Ripoti ya Ukaguzi ya mwaka 2017/18 iliyosainiwa na Prof. Assad itafikishwa bungeni? Itafanyiwa kazi na Bunge licha ya kutangaza kumtenga?

.......
Je, Raisi ataipeleka ikiwa na saini ya Prof. Assad? Isipopokelewa itakuwaje? Atairudisha ofisi ya CAG ili isainiwe na mtu mwingine?(sheria inaruhusu?) Siku 7 zikiisha ikiwa ni bilabila?

THE CALCULATED SERIES ON AIR! STAY TUNED FOR THE NEXT EPISODE.
 
The Humble Dreamer

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
7,270
2,000
Hii vita ni kali sana. Assad yupo sahihi na kinachoonekana mapema ni kua hata Jiwe mwenyew itakua kamwekea kifua spika mana si kwa kujidai huko na kauli zake na jiwe atakua mnafiki.
 
kanabyule

JF-Expert Member
Dec 5, 2016
386
500
Kumbuka kuwa Prof Assad na CAG ni vitu viwili tofauti.
Sishabikii mtifuaono uliopo, lkn endapo bunge litakataa kupokea na kusoma taarifa hiyo kutakuwa na sababu zaidi ya kukataa kufanya kazi na Prof. Assad.
Ni vyema ujue pia taarifa hiyo huandaliwa na watumishi mamia kama sio maelfu waliopo ofisi kuu, na ofisi za Kanda nchini. Majumuisho yake huwasilishwa makao na kuandaliwa kitaalamu, kisha kupitiwa na jopo maalum kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa mkuu wa taasisi hiyo ili aiwasilishe kwa Mkulu.

Hapo sijaelezea ama kuugua na kulazwa ama kufariki/kufa.

Kwa hiyo dhana ya kutokupokelewa na kutokuwasilishwa bungeni sioni kama inamantiki yo yote hapa.
RIPOTI ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ipo njia moja kuelekea Bunge la Jamhuri ya Muungano, lakini je, itafikishwa? Na ikifikishwa itasomwa? Halafu ikishasomwa?
RIPOTI ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ipo njia moja kuelekea Bunge la Jamhuri ya Muungano, lakini je, itafikishwa? Na ikifikishwa itasomwa? Halafu ikishasomwa?

Ripoti hiyo ipo kwenye kituo cha kwanza (kwa Rais John Magufuli), kituo chake cha pili ni Bungeni. Lakini ripoti hiyo imeandaliwa na Prof. Mussa Assad, mkuu wa taasisi hiyo (CAG) ambaye bunge limegoma kufanya kazi naye.

Hapa ndipo hoja ya Dk. Benson Bagonza, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Doyosisi ya Karagwe inaibuka, "Kama Rais Magufuli ataipeleka ripoti hiyo bungeni, atakuwa amelipuuza Bunge na kama hatoipeleka atakuwa amevunja Katiba ya Nchi".

Prof. Assad anatambua hilo, naye tayari ametoa tahadhari kwamba, mgogoro unaweza kuwa mkubwa kutokana na uamuzi wa Bunge kumtenga huku ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2017/18 ikiwa tayari imeandaliwa.

Ndani ya siku saba, baada ya bunge kuanza kuketi tarehe 2 Aprili 2019, ripoti hiyo inapaswa kufikishwa bungeni na kusomwa.

Job Ndugai, Spika wa Bunge, jana tarehe 4 Aprili 2019 alisema kuwa, Ripoti ya CAG ya mwaka 2017/18 haijafika mikononi mwake, kwa lugha nyingine ni kwamba, "Bado ipo Ikulu"

Ni kwa kuwa, Prof. Assad alisema tayari ameshaikabidhi ripoti hiyo kwa Rais Magufuli na kwamba, kinachosubiriwa kwa sasa ni kuwasilishwa bungeni kama inavyoelekezwa na Katiba na sheria za nchi.

Ni kwa mujibu wa Ibara ya 143(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ambapo inamtaka CAG kuwasilisha kwa Rais kila taarifa atakayotoa.

Kwa mujibu wa ibara hiyo, baada ya Rais kupokea taarifa hiyo, atawaagiza watu wanaohusika wawasilishe taarifa hiyo kwenye mkutano wa kwanza wa Bunge, utakaofanyika baada ya rais kupokea taarifa hiyo.

Na kuwa, ripoti hiyo itapaswa iwasilishwe katika mkutano huo kabla ya kupita siku saba tangu siku kikao cha bunge kilipoanza.

Maana yake ni kwamba, ripoti ya CAG inapaswa kuwasilishwa bungeni kabla ya Alhamisi ya wiki ijayo.

Spika Ndugai alikutana na waandishi wa habari jana ambapo miongoni mwa maswali aliyoulizwa, ni kwamba, ameishapokea ripoti ya CAG ya mwaka 2017/18 iliyosainiwa na Prof. Assad?
“Bado” ndivyo alivyojibu na kwamba, haoni sababu ya kueleza kama mhimili huo wa kutunga sheria utapokea ripoti hiyo na kuifanyia kazi ama la!

Hata hivyo Spika Ndugai alisisitiza kwamba, Bunge halifanyi kazi na Prof. Assad na kwamba,halijakataa kufanya kazi na Ofisi ya CAG.

Spika Ndugai anasema, walikwazwa kwa kauli ya Prof. Assad kwamba, Bunge ni dhaifu wakati Bunge hilo ndio linashirikiana naye kwa kiwango kikubwa na ofisi yake inashiriki katika utekelezaji wa shughuli za chombo hicho cha kutunga sheria.

Jumanne wiki hii, Bunge lilipitisha azimio la kutofanya kazi na Prof. Assad baada ya Kamati yake ya Kudumu ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwasilisha taarifa kuhusu shauri dhidi yake kwamba, alilidharau bunge.

Lakini je, Ripoti ya Ukaguzi ya mwaka 2017/18 iliyosainiwa na Prof. Assad itafikishwa bungeni? Itafanyiwa kazi na Bunge licha ya kutangaza kumtenga?

.......
Je, Raisi ataipeleka ikiwa na saini ya Prof. Assad? Isipopokelewa itakuwaje? Atairudisha ofisi ya CAG ili isainiwe na mtu mwingine?(sheria inaruhusu?) Siku 7 zikiisha ikiwa ni bilabila?

THE CALCULATED SERIES ON AIR! STAY TUNED FOR THE NEXT EPISODE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom