marveljt
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 1,503
- 1,479
Wanajukwaa kwema?
Kwa mujibu wa taarifa za CAG ni ukweli uliopo kuwa kuna tatizo kubwa sana serikalini. Kwa matamshi ya mkuu wa serikali ambayo kila leo analalamika ni dhahiri kwamba mchwa bado wapo na wanatafuna sana hazina.
Haiwezekani leo tunaenda mwaka wa pili bado patokee ufisadi wa zaidi ya trilion 2. Lazima ukiwa kama kiongozi ujitafakari mapema. Hata kama ni wanao wanadokoa nyumbani na kutoa vitisho lakini udokozi ukaendelea jua kuna tatizo kubwa. Ingekuwa ni mimi ningefanya moja kati ya haya
1. Kufumua mfumo mzima serikalini na kuwafikisha wahusika wote mahakamani. Hapa hata wewe kiongozi hupaswi kuwa na makandokando wala kuangalia mtu.
2. Kuachia madaraka kutokana na jopo unaloliongoza haliendani na wewe na hutaweza kufaulu.huwezi kuongoza nchi mwenyewe kama hupati sapoti.
Rais Magufuli ukiweza usiangalie hao haijalishi mmetoka barabara moja,mmelala kitanda kimojo au la. Hiyo ni dharau sana. Hawawezi kufanya ufisadi ukawaacha ili hali wewe unapinga ufisadi.
Bunge linawajibu mkubwa kwani ndiyo wapitisha bajeti,toeni oda wahusika wapigwe ndani kwanza. Mkipitisha bajeti na kulinyamazia hili maana yake mmekubali kuwa pamoja na hao mafisadi