Ripoti ya CAG inasemaje kuhusu bodi ya mikopo (HESLB)

Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
2,125
3,130
Malalamiko yamekuwa mengi kipindi cha karibuni. Tulitegemea CAG apite huko akague na ashauri namna nzuri ya urejeshwaji wa mikopo hiyo.

Ila sijasikia chochote kuhusu bodi hii inayolalamikiwa na wasomi wengi Tanzania. Mheshimiwa Rais muagize tena Kichere apite huku kwa mustakabali mwema wa taifa letu.

"Pamoja tunaweza"
 
Malalamiko yamekuwa mengi kipindi cha karibuni. Tulitegemea CAG apite huko akague na ashauri namna nzuri ya urejeshwaji wa mikopo hiyo. Ila sijasikia chochote kuhusu bodi hii inayolalamikiwa na wasomi wengi Tanzania. Mheshimiwa Rais muagize tena Kichere apite huku kwa mustakabali mwema wa taifa letu.
"Pamoja tunaweza"
mimi nilikua napendekeza tuanzishe lile vagi upyaaa mama anaonekana ni msikivu na anataka kuregebisha nchi ikae sawa atatusikiliza
 
Malalamiko yamekuwa mengi kipindi cha karibuni. Tulitegemea CAG apite huko akague na ashauri namna nzuri ya urejeshwaji wa mikopo hiyo. Ila sijasikia chochote kuhusu bodi hii inayolalamikiwa na wasomi wengi Tanzania. Mheshimiwa Rais muagize tena Kichere apite huku kwa mustakabali mwema wa taifa letu.
"Pamoja tunaweza"
Unakwanga donda bichiiii, utatuumiza kwa kuona damu mbichi.

Mama mama Mama Samia, Raisi wetu, chonde tuhurumie watumishi q. Unakopa 50 unalipa retention 95%.
 
Kwa kifupi "REPORT YA CAG" imeivua nguo za ndani awamu ya Rais Magufuli yote.

Kwenye swala la ATCL kuendeshwa kwa hasara ya Sh Billion 60 kuanzia 2016 - 2021, wakati Rais Magufuli alitengeneza sinema ya kutangaza kwamba shirika linafanya kazi kwa faida na kutengeneza sinema ya kupokea "GAWIO LA SERIKALI" ikulu kutoka kwa shirika la ATCL.

Aibu nliona mimi nlipokua kwenye kilinge cha pombe za kienyeji hapa kijijini nikisikiliza redio, mpaka nlipaliwa na moshi wa kiko changu nlichokua navuta, nikakidondosha.

Rais Samia akiamua kuunda "TUME HURU YA KUCHUNGUZA MAKINIKIA, MIKATABA, MATUMIZI YOTE YA SERIKALI, MANUNUZI YA NDEGE, UCHAGUZI, MIKOPO ILIOCHUKULIWA KISIRI SIRI n.k" basi atamvua nguo Marehemu huko alipo.

Hatari na nusu, sijui tumedanganywa mangapi awamu hio iliopita.
 
Malalamiko yamekuwa mengi kipindi cha karibuni. Tulitegemea CAG apite huko akague na ashauri namna nzuri ya urejeshwaji wa mikopo hiyo. Ila sijasikia chochote kuhusu bodi hii inayolalamikiwa na wasomi wengi Tanzania. Mheshimiwa Rais muagize tena Kichere apite huku kwa mustakabali mwema wa taifa letu.
"Pamoja tunaweza"
Inasema rudisheni madeni yenu..
 
Kwa kifupi "REPORT YA CAG" imeivua nguo za ndani awamu ya Rais Magufuli yote.
Kuna nyumbu wanasingizia eti hasara ya ATCL imetokana na Covid 19, wanasahau Covid imekuja 2020 mwanzoni, ripoti ya CAG imesema miaka 5 iliyopita ina maana hasara imekuwepo kabla ya 2020 ambayo ndio Covid ilianza.

Mwaka 2019 Prof Assad alitumbuliwa kwa kusema ukweli baada ya kuitaja ATCL kuwa miongoni mwa mashirika ya Umma yenye kutia hasara. Prof akafukuzwa kwa kisheria cha Takwimu ambacho uhalali wake umetokana na Katiba
 
Hiyo Bodi ni bora ingeitwa Bodi Kichaa ya Mikopo! Inawaumiza sana wanufaika. Mambo ya rentation fees ni upuuzi tu. Hela hazijakopwa benki, iweje zirudishwe kwa kuangalia thamani ya fedha ya wakati huo?

Huku kila mwezi wakitoa takwimu za kutokuwepo kwa mfumuko wa bei? Kama vipi basi Serikali utulipe na sisi watumishi hiyo rentation fees! Maana ni miaka sita sasa hakuna cha nyongeza ya mishahara au kupandishwa madaraja.
 
mama akitoa statement tu kesho wanaliondoa hilo deni watuache tulipe tulichokopa sio kutupiga waziwazi uzuri spika ndugai alianza nalo japo alikua anamhofia jiwe saizi likipelekwa bungeni linafutiliwa mbali yani niwape siri wabunge kama mnataka kiki ya kutokea anzeni na hili la bodi ya mikopo utakumbukwa milele kuwa umeacha legacy manake unakua umeokoa wengi
 
Tumuombee spika analimudu
 
Mlipokuwa mnatafuna na wachumba hela ya serikali, mlijua hakuna kurudisha🤣🤣🤣
Mlisababisha sie tusio na mkopo wachumba watukatae....
 
Back
Top Bottom