Ripoti ya CAG ina kitu tusichokijua kuhusu ESCROW?

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,562
2,000
"Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali iliombwa na Katibu wa Bunge na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kufanya ukaguzi maalum wa Akaunti ya Tegeta Escrow. Tunapenda kuwajulisha Umma taarifa kuhusu mwelekeo wa ukaguzi huo. Tafadhali pakua kiambatanisho cha taarifa kamili kuhusu suala hilo kwenye link hii2014 IPTL Press Release WORD" - Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) [16 Oktoba 2014]

"Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali CAG - Prof MUSSA JUMA ASSAD, ameahidi kufanya marejeo katika Ripoti ya ofisi yake kuhusu Akaunti ya TEGETA ESCROW ambayo iliibua mjadala mzito Katika Mkutano wa Kumi na sita na Kumi na saba wa bunge wiki iliyopita mjini DODOMA.Prof ASSAD ameeleza hayo mjini ARUSHA baada ya kufungua Mkutano wa Bodi ya wahasibu NBAA ambapo amesema katika ripoti hiyo ya TEGETA ESCROW kuna mambo machache yanayohitaji kufanyiwa kazi" - Shirika la Utangazaji TanzaniA (TBC) [5 Desemba 2014]

"Kufuatia kupokea nyaraka hizo, Rais Kikwete ameelekeza kuwa Ripoti ya CAG iwekwe hadharani kwa ajili ya umma kuweza kuisoma na kujua nini hasa kimesemwa na kupendekezwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Rais Kikwete ameelekeza kuwa Ripoti hiyo itangazwe kwenye magazeti yanayosomwa na watu wengi na kwenye mitandao ya kijamii, ili Ripoti hiyo iweze kupatikana kwa Watanzania wengi" - Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais [9 Desemba 2014]

"Ikulu imeagiza Taarifa ya CAG ichapwe kwenye magazeti, jambo ambalo halijapata kutokea huko nyuma kwani sio mara ya kwanza PAC kutumia Taarifa ya CAG kuwajibishana" - Ukurasa wa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) [12 Desemba 2014]
 

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Hili swali hata mimi ninajiuliza sana lakini sina jibu.

Ni ajabu kwenye suala nyeti ambalo limepigiwa kelele kuanzia 1990's ndani na nje ya nchi lakini mpaka ninaandika comment yangu, hakuna repoti ya CAG kwenye public domain ukiondoa wabunge na pia ofisi ya Rais.

Tunaambiwa hata kwenye sheria za TAKUKURU, repoti yao hapewi Rais wa nchi bali anakabidhiwa moja kwa moja DPP kufanya uamuzi wake ambao hata Rais hana uwezo wa kuupinga!

Something smells fishy!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom