Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha

Ni zama zipi mambo yalikua hayaendi? Au hizo zama zilizosemwa kua zilikua za kifisadi, mambo yalikua hayaendi?!
Kuna mambo mengi sana yanafikirisha kwenye hili sakata jipya la ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu kuibua madudu mengi ambayo serikali iliyokuwa chini ya hayati JPM yamejitokeza...
 
Katiba mpya inaitajika kwa sasa kuliko wakati mwingine wowote.
Yeyote atakayeizuiya huyo ndio adui wa maendeleo ya Tanzania
 
Siku ya leo sijui tuuiteje huko; Mbaya? Au nzuri sana?

Ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali inayoendelea kusomwa muda huu si kwamba tu inawaweka CCM na watetezi wa mwendazake kwenye wakati mgumu sana, lakini tayari imechefua wananchi wengi kwa kiwango kisichomithilika...
Wasalaam

Ama baada ya salam!

Ripoti ya CAG miaka mitano ya Rais Kikwete 2010-215 inasemaje?.

Kwani CAG alisema nini kuhusu mzee mkapa miaka mitano ya mwisho?

Au ndugu mavi ya kale huwa hayatoi harufu?

Iwe iwavyo Magufuli keshakufa. Kazikwa na kama hawakumpiga sindando huenda kashaoza.

Ila Tanzania bado ipo. Imara sina hakika! Na kila uchwao wake zetu wanabeba mimba na wengine wanajifungua na hawa wanaikaribishwa katika ardhi hii hawana sehemu nyingine ya kupaita nyumbani isipokua hapa.

KAMA TUMEAMUA KUISHI YALIYOPITA SAWA! ILA TUJUE KUPEVUKA NI KUIFIKIRIA KESHO...
 
Binadam akili zetu zinawaza tofauti sana, yaani sana! Ngoja niishie hapa!
 
Kwa ushahidi wa ripoti hii ya CAG Magufuli alikuwa ni kiongozi populist ambae alikuwa ni mwizi,fisadi na mzembe wa mali za uma aliekuwa anajificha kwenye chaka la siasa za propaganda.
 
Mleta uzi hujamsoma CAG deni la taifa limekuwa sana jamaa kakopa mno alafu akija jukwaani eti anatudanganya kuwa tunajenga kwa pesa zetu wenyewe.jamaa alikuwa noma
 
Kuna mambo mengi sana yanafikirisha kwenye hili sakata jipya la ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu kuibua madudu mengi ambayo serikali iliyokuwa chini ya hayati JPM yamejitokeza...
Mbunge wa ccm akikutwa na tuhuma au ufisadi ni nini hatuna ya ubunge wake? Mfano kibwangala na prof Adolf Mkenda?
 
Ukitumia report ya CAG kukamata mwizi ama kuamini ulaji mkubwa then ngumu kukusaidia

CAG ana deal na audit queries ambazo sio necessarily wizi...

Ndio maana wanapewa muda kutoa majibu ya hoja za ukaguzi

Nimekuwekea mfano wa maelezo ya hoja huwa zinapanguliwa kwakuwa most of it ni accounting errors na sio wizi...

Tukana boss ...
Yaaani mataga bwana.... nyie si ndo mlikua mnasema Mwendazake kafyekelea mbali ufisadi? Kuna ndege imelala aiport toka 2015 ila mnatoa pesa za maintanance. Mnanunua na nyingine... unataka kuniambia alikua hajui? Yaani wizara zifanye ubadhirifu halafu asijue wakati kina Aika walikula buku 20 za wamachinga wanatakiwa kuzilipa
Screenshot_20210408-180035_Samsung%20Internet.jpg
 
Kuna mambo mengi sana yanafikirisha kwenye hili sakata jipya la ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu kuibua madudu mengi ambayo serikali iliyokuwa chini ya hayati JPM yamejitokeza...
CAG ametajwa kwenye katiba ya nchi na kuwa haingiliwi na mhimili wowote katika kufanya kazi zake za kukagua matumizi ya fedha za umma

Nashangaa mtu tuliyepewa kikatiba atusaidie kujua fedha zetu zinatumikaje ndio huyo tunamsimanga tena!

Nani katuroga? Ushabiki?
 
Mada ya 2018

Awamu ya tano imetupa pembeni utaratibu wa zabuni na sasa inaamua na kufanya manunuzi au kuingia mikataba wenyewe kwa amri toka juu...

Rejea hii itatukumbusha siku za usoni na hasa kwa Miradi hii.

1. Uwanja wa ndege chato
2. Vitambulisho vya utaifa
3. Fly overs
4. Bombadier
5. Tenda za ujenzi za TBA n.k
6. SGR
7. Bwawa la umeme

Kwa kumalizia tuu.... nimeandika hayo nikiwa full detailed. Kuna vitu duniani havichiki navyo ni Jua mwezi na ukweli.

MUDA NI HAKIMU WA YOTE!!

Credit kwako Lusungo
Akija mwingine mambo ni Hays Hays kuibua madudu ya Samoa pia.Naye atadai kuwa tulichezewa mno
 
Magu aamshwe aeleze kwaa nini alitudanganya
aaaaaa apatikane wa kwenda kuugonga mlango wa kaburi aje atueleze huu upigaji wa kiwango cha standard geji ilikuwaje akimalize arudi usingizi wake, au akiamka atampiga biti naye CAG atachomoa kitabu cha pili na kusema hii ripoti ya kwanza ilikuwa feki ngojeni niwasilishe upya
 
CAG analeta audit queries sio wizi.
Anatoa accounting errors na sio ufisadi.

Wahusika wanatoa viambatanisho muhimu na kujibu tuhuma za kikaguzi..

Yatakayokosa majibu ndio huwa tuhuma kamili na wahusika kushtakiwa

Angalia attachment ya kinachotokea baada ya report
Nipambanie nini?
Kuna mwaka ambao CAG hajawahi kuleta haya mambo?
Screenshot_20210408-180035_Samsung%20Internet.jpg
 
Hela nyingi za utekelezaji wa miradi ya mwendazake ilikua haipati baraka za bunge
Hivyo hatujui ni sh ngapi zilikua zinaenda...
Shida ni kwamba jamaa alikuwa hataki mambo ya michakato! Ukiwa na falsafa ya kutotaka michakato lazima uhusishwe na wizi! Kimsingi yeye anajua hela ipo na anataka kukamilisha jambo flani kwa maslahi mapana ya taifa😸 ila kupitia mijadala ya bunge hela zingetoka vile vile japo kwa kelele nyingi! Hayo ndio mzee hakuyataka.
 
Kwanza Tanzania haijawahi kupata Rais ambaye sio mzalendo kama yupo mtaje.

Pili toka Rais Mkapa mpaka leo hakuna siku mambo yalisimama. Tofauti ni vipaumbele huyu anajali ukweli na uwazi, huyu demokrasia huyu ujenzi wa miundo mbinu.

Kila awamu ndani ya nchi hii ilijenga miundo mbinu ya kimkakati kwa nafasi yake, pamoja na ujenzi huo kamwe hawakuwahi kujenga kwa gharama ya jasho la watumishi wa umma. Hawakuwahi kujenga kwa gharama ya umoja wa taifa letu, hawajawahi kujenga kwa gharama ya maisha ya vijana wa nchi hii.

Unaposema miradi ilikuwa inaenda inatakiwa useme kwa gharama ya nani? Hakuna nyongeza ya mshahara kwa watumishi wa umma kwa miaka 5 mfululizo hakuna ajira kwa vijana na biashara nyingi zimekufa katika awamu ya tano.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom