Ripoti ya CAG: Deni la Taifa lafikia trilioni 33.5, NEC yamulikwa, Mishahara hewa na Ukwepaji kodi..

Leo tarehe 25 April 2016 repoti ya CAG Alhaj Prof. Mussa Juma Assad, inawasilishwa na kujadiliwa bungeni.

Ripoti hiyo ni ya hesabu za serikali kwa mwaka 2014/2015.

Pamoja na CCM kuhakikisha hatulioni bunge ili kuficha mambo kama haya,lakini baki hapa kupata updates za uwasilishaji.

CAG anaenda kuonesha How public funds were eaten under monitoring and supervision of CCM.CCM is going to be undressed. M/S Lugumi kitu gani,kuna uuzwaji wa nyumba za serikali na uchambuzi wa Thamani ya Fedha ya Miradi ya Barabara 2014/2015,Unajua halmashauri ngapi zimepata Hati Chafu/zenye mashaka?

Haaah haaah,usibadili channel.

Updates:
Spika anaarifu kuwa repoti za PAC na LAAC ambapo CAG husemeamo,hazita wasilishwa,mpaka mda utakapopangwa.Watawasilisha repoti za mawaziri tu.Connect dots.Yaani mtuhumiwa anajiwasilishia hukumu.

Pamoja na umuhimu wa repoti na tukio kwa ujumla, TBC wametoweka baada ya kipindi cha Maswali na Majibu.

Hii ni hujuma kubwa kwa sisi wananchi kushindwa kuona na kusikiliza ni nini msimamizi mkuu wa fedha ameona katika matumizi ya serikali
 

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,227
5,270
Cg37dotWkAA366J.jpg


=========
UPDATES:
=========

Screen Shot 2016-04-25 at 23.15.17.png

=> Ulaji na uzembe vinatajwa kubeba sehemu kubwa ya ripoti hii.

=> Misamaha ya kodi 2014/15 ni asilimia 2 ya pato la taifa kinyume cha asilimia 1

=> Halmashauri 40 hivi ndo zenye hati safi kati ya halmashauri zaidi ya 160

=> Bidhaa a bilioni 9 za kupelekwa nje ziliuzwa hapa hapa nchini. Upigaji huo wa ukwepaji kodi.

=> Bidhaa za bilioni 89 za nje hakuna ushahidi kama zilienda Rwanda, Burundi na Uganda.


=> Rufaa za kodi nyingi mno zimedoda mahakamani na hivyo kuikosesha serikali kodi

=> Deni la Taifa hadi Juni 2015 lilifikia trilioni 33.5. Ndani ya mwaka mmoja lilikua kwa trilioni 7!

=> Malipo kwa deni kwa mwaka ni trilioni 4.

=> Deni na mishahara inamaliza mapato yote ya taifa. CAG anahoji, tutapata wapi pesa za maendeleo?

=> CAG Anataka maduka ya fedha za kigeni yadhibitiwe

=> Vyama vya siasa, kimoja tu kimewasilisha hesabu. Vyama 21 bado, Msajili afiatilie. Hajakitaja chama kilichowasilisha

=> Mishahara hewa katika Taasisi za umma 16 ni Shilingi bilioni 390. Mishahara ambayo haikulipwa na haikurejeshwa hazina ni bilioni 2


=> Sh. Milioni 700 za makato ya watumishi kwa Katavi na Kilimanjaro hayakuwasilishwa kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

=> Sh. Milioni 827 za vifaa vya upigaji kura zilitumika kwa kazi isiyo na tija katika Uchaguzi 2015


=> Nakala 158,003 za Katiba Pendekezwa hazikusambazwa kwa walengwa wakati wa mchakato wa Katiba Mpya

=> Manunuzi yenye thamani ya Sh. Bilioni 27 yalifanywa na Mashirika ya Umma bila ushindani


=> Cheti cha uendeshaji ATC kimeisha muda tangu 2010. ATC ina Wafanyakazi wengi kuliko kazi zilizopo

=> Bidhaa za bilioni 9 za kupelekwa nje ziliuzwa hapahapa nchini. Nia ni kukwepa kodi!

=> Bidhaa za Sh. Bilioni 89 za kwenda nje hakuna ushahidi kama zilienda Rwanda, Burundi na Uganda.


=> CAG ataka UDA irejeshwe serikalini. Mwenyekiti wa Bodi ya UDA, Idd Simba aliwekewa sh. milioni 320 ktk akaunti yake binafsi.

=> Kampuni ya SAAFI inadaiwa Sh. bilioni 17. Hii ni ya mwanasiasa mkongwe, Mzindakaya.


DOWNLOAD ALL REPORTS:
 

Attachments

  • RIPOTI-YA-UKAGUZI-WA-TAARIFA-ZA-FEDHA-ZA-MAMLAKA-ZA-SERIKALI.pdf
    1.4 MB · Views: 135
  • RIPOTI-YA-UKAGUZI-WA-TAARIFA-YA-FEDHA-ZA-SERIKALI-KUU-KWA-MW.pdf
    4.8 MB · Views: 416
  • RIPOTI-YA-JUMLA-YA-UKAGUZI-WA-UFANISI-NA-UKAGUZI-MAALUMU-KWA.pdf
    3.5 MB · Views: 117
  • RIPOTI-YA-UKAGUZI-WA-TAARIFA-ZA-FEDHA-ZA-MAMLAKA-ZA-SERIKALI.pdf
    1.4 MB · Views: 82
  • RIPOTI-KUU-YA-MASHIRIKA-YA-UMMA-KWA-MWAKA-WA-FEDHA-ULIOISHIA.pdf
    1.6 MB · Views: 170
  • RIPOT-KUU-YA-MIRADI-YA-MAENDELEO-KWA-MWAKA-WA-FEDHA-ULIOISHI.pdf
    3 MB · Views: 145
Leo tarehe 25 April 2016 repoti ya CAG Alhaj Prof.Mussa Juma Assad,inawasilishwa na kujadiliwa bungeni.Ripoti hiyo ni ya hesabu za serikali kwa mwaka 2014/2015.Pamoja na CCM kuhakikisha hatulioni bunge ili kuficha mambo kama haya,lakini baki hapa kupata updates za uwasilishaji.CAG anaenda kuonesha How public funds were eaten under monitoring and supervision of CCM.CCM is going to be undressed. M/S Lugumi kitu gani,kuna uuzwaji wa nyumba za serikali na uchambuzi wa Thamani ya Fedha ya Miradi ya Barabara 2014/2015,Unajua halmashauri ngapi zimepata Hati Chafu/zenye mashaka?haaah haaah,usibadili channel
aisee OKW BOBAN SUNZU mbona sijakuona hapa getini Bungeni nimewaona external auiditors wa Bunge pekee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom