BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,368
- 8,102
Ripoti hiyo ya CAG imeibua hoja nyingi zinazoonyesha matumizi mabaya ya fedha hizo zilizopelekwa kwenye wizara mbalimbali za serikali (Afya, Elimu, Utalii, Maji na Watu wenye Ulemavu). Jumla ya thamani ya hoja zote za ukaguzi zinazoashiria kuwepo kwa matumizi mabaya zinathamani ya Shilingi Bilioni 212.1, sawa na asilimia 17.06 ya fedha zote za mkopo zilitolewa ambazo ni shilingi Trilioni 1.24.
Mgawanyo wa thamani ya hoja za ukaguzi kwa kila wizara ni kama ifuatavyo;
• Wizara ya Afya - Tsh. Bilioni 91
• Wizara ya Elimu - Tsh. ilioni 33.5
• Wizara ya Maji - Tsh. Bilioni 82.8
• Wizara ya Maliasili na Utalii - Tsh. Bilioni 1.2
• Hifadhi ya Jamii (TASAF) - Tsh. Bilioni 1.5
• Wizara ya Maendeleo ya Jamii - Tsh. Milioni 141.
Katika hoja hizi ambazo nyingi zinahusu manunuzi, CAG amebaini kwamba kuna baadhi ya vifaa kama vile Magari kwenye sekta za Afya na Elimu hayakufika hadi tarehe ya ukaguzi. Usimamizi mbovu wa matumizi ya fedha hizi za mkopo unatoa sura kwa namna gani Serikali inashindwa kuwajibika.