Ripoti ya CAG 2021-2022: Rais Samia ataka baadhi ya mashirika yasiyo na tija kufutwa

kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu leo amepokea ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) pamoja na TAKUKURU. Katika ripoti hiyo CAG aliyataja mashirika 14 yanayoendeshwa kwa hasara ikiwemo TRC, ATCL na NDC. Rais Samia alisema kwa muda baadhi ya makampuni yamekuwa yakiendeshwa kwa hasara lakini hayaingizii serikali chochote ni bora yakafutwa ili kutoendelea kuleta hasara.

"Kuna haja ya kufanya tathimini kama baadhi ya mashirika ya umma yanafaa kuendelea kuwa nayo, yale yanayofaa yaendelee na yasiyo na tija yafutwe. Mashirika mengi yanachuma fedha kutoka serikalini lakini yenyewe haileti fedha serikalini" - Rais Samia Suluhu.

Lakini kwa upande wa TTCL, Rais Samia Suluhu anasema "TTCL na biashara ya simu kusema kweli imewashinda, tujiulize hivi kweli wanaweza kuendelea kufanya biashara ya sekta ya simu, kwanza wao wana mkongo, kwa kufanya biashara ya simu hakuleti mazingira sawa ya ushindani katika biashara hiyo na kampuni nyingine."

FsYZILXXoAE0pLd

 
Ttcl haiwezi kufanikiwa sababu mafisadi papa kutoka CCM ndio wamiliki wa makampuni binafsi yanayoshindania soko. Juzi wamezuia kampuni ya kimarekani liyotaka kuwekeza mtandao wa intaneti wa bei nafuu kwa sababu za kitoto zilizotolewa na mtumishi wa mafisadi Nape Mnauye
 
Back
Top Bottom