Ripoti ya CAG 2017/2018: Makampuni ya Kijapan ya Kuuza Magari yaliyotumika yamewaibia Watanzania TZS 21Bil

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,455
29,134
Kwema Wakuu,

Kwa mujibu wa Report ya CAG, makampuni haya yalipaswa kutoza US$ 150 kama ada ya ukaguzi lakini yamekuwa yakitoza kuanzia US$ 300 na kuendelea kiasi cha kupelekea Watanzania kuibiwa kiasi cha TZS 21Bil kwa miaka miwili tu.

Makampuni hayo ni SBT, Autorec, TradeCarView, Befoward na Real Motors. Ameilaumu pia Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa wizi huu.

1070425
 
Haya makampuni hukagua kule kwa niaba ya TBS ambao ndio wasimamizi wa maswala ya ubora hapa nchini.

Hii bei iliyozidishwa watakuwa wanajua tu, na wameamua kupiga kimya tuibiwe sababu labda na wao wana maslahi.
 
Tutapataje pesa yetu....just kidding

Wauza Maharishi toka Japan Dealers ndani ya Tz wanatuibia sana

Kwanza wanapunguza mileage pili wanakuwekea ushuru mkuuubwa. Bei ya magari ishuke sana

Sina hamu na hawa watu wapemba waarabu sijui wahindi ni wezi tu.

Show rooms nyingi ni za kitapeli
 
Hii inspection fee nayo ni aina flani ya urasimu tu na njia ya kukusanya hela, sidhan kma kuna gari ishawahi kukataliwa kwny inspection ya TBS baada ya kulipia ushuru wa TRA. Hakuna weledi wa ukaguzi ni process tu.

Mtu umenunua gari mpya kutoka nje ikifika hapa TZ inakaguliwa nini? Nchi yetu haina hata sheria za CO2 emissions.

Ukirudi huku mtaani kuna malori mikangafu hata haifai kuwa barabarani, haya ndo risky kwa wananchi na mazingira watukagulie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tutapataje pesa yetu....just kidding
Wauza Maharishi toka Japan Dealers ndani ya Tz wanatuibia sana
Kwanza wanapunguza mileage pili wanakuwekea ushuru mkuuubwa
Bei ya magari ishuke sana
Sina hamu na hawa watu wapemba waarabu sijui wahindi ni wezi tu
Show rooms nyingi ni za kitapeli
Kuipata hela yetu ni kuwaambia watukagulie bure mpaka ile 21Bil irudi kisha wateja waliokua walipe Kule tuwaambie walipe huku
 
Hata kama tunapigwa bado ni rahisi ukiagiza direct kupitia haya makampuni kuliko kununua kwa wabongo wenzetu
 
Back
Top Bottom