Ripoti ya benki ya Dunia inaonesha Zimbabwe ina nafasi nzuri kwa mazingira ya uwekezaji kuliko Tanzania

Mauritius aliyeshika No. 1 yeye hua anaibiwa nini?

Wanaibiwa pato lao la taifa kupitia Utalii.

Biashara nyingi inashikwa na wageni.

Fungate nyingi na vekesheni hufanyika Mauritius.

Ndo maana hadi sasa katika Afrika Mauritius ndo nchi pekee ambayo huendi karantini ukiingia Ulaya.
 
Alafu unasikia mijitu inapiga kelele huku haina ajira wala kipato cha uhakika, “Magufuli Tano Tena”. Uchafu Mtupu!!!


Huu ni uthibitisho tosha kuwa vyovyote vile ni lazima tuwapumzishe magufuli na CCM yake mwaka huu!!
Angalia huko nyuma uko wazi?
 
Alafu kuna watu wanajifanya Eti tunawazidi kenya!!! Pumbavu
Wakenya wapo mbali sana... Tunatakiwa tujifananishe na kenya na sio Zimbabwe, ndiyo maana hatukui, tunatakiwa tushindane na mshindani, kenya anafanya vizuri, na tukisema kenya atashuka kiuchumi kwasababu ya corona tunajidanganya
 

Mfumuko wa bei sasa hivi Zimbabwe ni asilimia 800.

Kuna upungufu mkubwa wa chakula. madawa, mafuta na fedha haipo kwenye mzunguko.

Umaskini wa wazimbabwe umekuwa sasa ni asilimia 70 ya idadi ya wazimbabwe.

Miezi miwili yaenda sasa kuna mgomo wa manesi na watumishi wa afya wakitaka wapatiwe PPEs na mshahara wao ulipwe kwa dola.

Bila PPEs wagonjwa wa COVID-19 wataendelea kufa na sasa kuna wagonjwa zaidi ya 5000 na vifo 129.

Isitoshe kuweka zaidi chumvi kwenye kidonda waziri wa afya ni Constatino Chiwenga ambae ni mwanajeshi na hana uzoefu wa masuala ya afya.

Mbali ya hayo serikali ya Mnangagwa imekubali kuwalipa wazungu walowezi dola bilioni 3.5 ambao mashamba yao yalichukuliwa na serikali ya Robert Mugabe, ikiwa ni kutimiza masharti ya kuondolewa vikwazo na nchi za kibeberu.

Sasa Zimbabwe itafanikisha vipi haya yote?

Zimbabwe imeamua kutumia amana zake za kigeni kwa kuuza rasilimali zake kama dhahabu, almasi na ardhi iliyoko katika miji yake maarufu.

Hali ni mbaya sana Zimbabwe kwa sasa na nina watu wa karibu kabisa wapo Harare wananipa updates.

Na siku si nyingi utasikia jeshi limemwondoa Mnangagwa maana anae Chiwenga na yupo mwingine jenerali Sibusiso Moyo yuo pembeni anaangalia ustaarabu.

Kama walimwondoa Mugabe na kumweka Mnangagwa basi hawatashindwa kufanya mabadiliko mengine.

Kama wakumbuka uzuri, ni huyu Chiwenga ndie alietangaza mapinduzi baridi kwenye runinga.

By the way, wafahamu Mnangagwa ana utajiri kiasi gani?

Wewe ni mjuzi wa kutafuta hizi taarifa, basi tafuta nani ni wamiliki wa makampuni ya madini yaitwa Sakunda Holdings na Landela Mining Ventures.

Zimbabwe ipo nyuma sana ya Tanzania kwenye uwekezaji na hizo taarifa ni propaganda za kupindisha ukweli halisi.
 
Wanaibiwa pato lao la taifa kupitia Utalii.

Biashara nyingi inashikwa na wageni.

Fungate nyingi na vekesheni hufanyika Mauritius.

Ndo maana hadi sasa katika Afrika Mauritius ndo nchi pekee ambayo huendi karantini ukiingia Ulaya.

Kama ni hivyo basi itabidi FDI yetu iwe zero kabisa,maana haiwezekani mabeberu wakaja kumiliki biashara nyingi kuliko wenyeji,haya mahoteli kama Singita Grunet,Bilila Lodge etc yatakua yanatuibia sana sisi wazalendo.

Khs Mauritius kua nchi pekee ambayo huingii karantini ukiingia ulaya hii ni propaganda ya wazi kabisa.Nchi za Africa zilizoruhusiwa na EU ni Mozambique, Angola, Namibia, Ethiopia, Zambia, Rwanda, Uganda, Egypt, Tunisia, Algeria and Morocco.Na hio Mauritius wala haipo kwny list.

Israel yenyewe imeruhusu nchi 1 tu kutoka Africa kuingia nchini kwao na hautahitaji kuwekwa karantini Ambayo ni Rwanda pekee yake,je hao Rwanda wao wanaibiwa nini na Israel?
 
Hii ndio justification ya kuwafidia mabillion ya dollari.

Hawa Wazungu na mashirika yao wakati mwengine wanazo propoganda za ajabu na kifedhuli.
Jibu swali hayo mashamba ya wazungu zimbabwe waliweza kuyaendesha na kuyahudumia???
 
Back
Top Bottom