Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,994
- Thread starter
- #41
Labda watu wapate nafasi ya kupitia hizi ripoti ili kusoma na kujiuliza maswali sahihi. NI lazima tukumbuke kuwa ni jukumu letu kupima ushahidi ulioko mbele yetu, kujiuliza maswali sahihi na kuweza kutengeneza mahitimisho ambayo yanaendana na ule ushahidi uliopo. Usikubali tu kauli zilizoko kwenye ripoti hii bila wewe mwenyewe kuona mapengo (gaps) ndani ya ripoti nzima. Vinginevyo utaanza kuimba wimbo wa watawala alimradi wamekupa kibwagizo.