FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,416
- 7,828
Habari!
Mwanasayansi wa nyuklia wa Iran aliyeuawa karibu na mji mkuu Tehran mwezi Novemba mwaka 2020, aliuawa kwa bunduki ya otomatiki iliyoingizwa nchini humo na shirika la ujasusi la Israel Mossad ikiwa katika vipande maalumu, kwa mujibu wa ripoti.
Ripoti ya The Jewish Chronicle kutoka nchini Uingereza ikinukuu vyanzo vya kiintelijensia ilieleza [Jumatano] kuwa, shambulizi hilo lilifanywa na timu ya watu zaidi ya 20 wakiwemo raia wa Israel na Iran. Kikosi hicho cha ujasusi kilimshambulia mwanasayansi Mohsen Fakhrizadeh baada ya kuzifuatilia nyendo zake kwa muda wa miezi nane, ripoti ilieleza.
Vyombo vya habari vya Iran viliripoti kuwa Fakhrizadeh alipoteza maisha akiwa hospitalini Novemba 27 mara baada ya kushambuliwa kwa bunduki akiwa katika gari lake. Mara baada ya kifo chake, Iran iliishutumu Israel kuhusika katika shambulio hilo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif akiandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa "kuna viashirio vikubwa vya kuhusika kwa Israel."
Kwa mujibu wa ripoti, Iran "imetathmini kwa siri kwamba itachukua miaka sita" kabla ya kupatikana kwa mbadala wa Fakhrizadeh na kwamba kifo chake "kimeongeza kipindi cha wakati ambao utaichukua Iran kufanikisha bomu la nyuklia kutoka takribani miezi mitatu na nusu hadi miaka miwili."
Ripoti hiyo ilieleza kuwa, bunduki iliyotumika ilikuwa imewekwa katika gari aina ya Nissan (pick-up), ikiendeshwa kutokea mbali (remote) na kikosi cha ujasusi kilichokuwa ardhini kikifuatilia nyendo za mwanasayansi huyo. Bunduki hiyo iliripotiwa kuwa na uzito mkubwa uliotokana na kuunganishwa na bomu maalumu ambalo lililipuka mara baada ya shambulizi ili kupoteza ushahidi.
Pia, ripoti ilisema kuwa, shambulizi hilo lilitekelezwa na "Israeli pekee, bila ya ushiriki wa Marekani" lakini maafisa wa Marekani walipewa kiasi fulani cha taarifa kabla ya utekelezaji wa shambulizi hilo.
Waweza kuipata taarifa hii kupitia vyanzo vifuatavyo:
1) Reuters | Iranian nuclear scientist killed by one-ton automated gun in Israeli hit
2) Al Jazeera | Iranian nuclear scientist killed by Israeli automated gun
3) The Times of Israel | Report: Iranian nuke scientist was killed by Israeli 1-ton automated gun