Ripoti: Mwanasayansi wa nyuklia wa Iran aliuawa kwa bunduki ya otomatiki

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
5,416
7,828
Habari!

Mwanasayansi wa nyuklia wa Iran aliyeuawa karibu na mji mkuu Tehran mwezi Novemba mwaka 2020, aliuawa kwa bunduki ya otomatiki iliyoingizwa nchini humo na shirika la ujasusi la Israel Mossad ikiwa katika vipande maalumu, kwa mujibu wa ripoti.

Ripoti ya The Jewish Chronicle kutoka nchini Uingereza ikinukuu vyanzo vya kiintelijensia ilieleza [Jumatano] kuwa, shambulizi hilo lilifanywa na timu ya watu zaidi ya 20 wakiwemo raia wa Israel na Iran. Kikosi hicho cha ujasusi kilimshambulia mwanasayansi Mohsen Fakhrizadeh baada ya kuzifuatilia nyendo zake kwa muda wa miezi nane, ripoti ilieleza.

Vyombo vya habari vya Iran viliripoti kuwa Fakhrizadeh alipoteza maisha akiwa hospitalini Novemba 27 mara baada ya kushambuliwa kwa bunduki akiwa katika gari lake. Mara baada ya kifo chake, Iran iliishutumu Israel kuhusika katika shambulio hilo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif akiandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa "kuna viashirio vikubwa vya kuhusika kwa Israel."

Kwa mujibu wa ripoti, Iran "imetathmini kwa siri kwamba itachukua miaka sita" kabla ya kupatikana kwa mbadala wa Fakhrizadeh na kwamba kifo chake "kimeongeza kipindi cha wakati ambao utaichukua Iran kufanikisha bomu la nyuklia kutoka takribani miezi mitatu na nusu hadi miaka miwili."

Ripoti hiyo ilieleza kuwa, bunduki iliyotumika ilikuwa imewekwa katika gari aina ya Nissan (pick-up), ikiendeshwa kutokea mbali (remote) na kikosi cha ujasusi kilichokuwa ardhini kikifuatilia nyendo za mwanasayansi huyo. Bunduki hiyo iliripotiwa kuwa na uzito mkubwa uliotokana na kuunganishwa na bomu maalumu ambalo lililipuka mara baada ya shambulizi ili kupoteza ushahidi.

Pia, ripoti ilisema kuwa, shambulizi hilo lilitekelezwa na "Israeli pekee, bila ya ushiriki wa Marekani" lakini maafisa wa Marekani walipewa kiasi fulani cha taarifa kabla ya utekelezaji wa shambulizi hilo.

Waweza kuipata taarifa hii kupitia vyanzo vifuatavyo:
1) Reuters | Iranian nuclear scientist killed by one-ton automated gun in Israeli hit
2) Al Jazeera | Iranian nuclear scientist killed by Israeli automated gun
3) The Times of Israel | Report: Iranian nuke scientist was killed by Israeli 1-ton automated gun
 
Iran bado sana kwa Ujasusi.

Na nyinyi mna amini stori hizi za kuchonga,mfano - eti: tathimini ya siri ya Iran inasema itachukwa Iran miaka sita kumpata mwana sayansi mwenye kiwango cha kumfikia marehemu kitaaluma, eti kuuwawa kwake kuta rudisha nyuma Iran miaka sita katika juhudi zake za kuunda bom la nuklia, hizi ndizo stori za kila siku ambazo Israel na like mind wenzake uzi-manufacture kuhadaa Dunia kwa lengo
kujustify ujambazi wake wa kuwalenga wana sayansi wa Iran - killing them in cold blood, halafu baadhi ya watu na akili zao timamu wanaunga mkono ujambazi wa Israel.

Israel na USA hawataki kabisa Iran iwe na uwezo mkubwa wa kisayansi kukaribia au zidi wa kwao, ukiangalia kijuu juu unaweza kufikiri US na Israel wako concern na Iran kumiliki mabom ya Nuklia,ukweli wa mambo Israel na USA hawataki lijitokeze Taifa lolote ndani ya mashariki ya kati lenye uwezo mkubwa kijeshi kuliko Israel, US inataka kuitumia Israel kulinda maslahi yao mashariki ya kati.

Israel na washiriki wake ndani ya Iran wamepania kuwamaliza wana sayansi wanuklia wa Iran, wanao tekeleza operation ya kuuwa wana sayansi ni Wairan wenye asili ya Israel wako wengi hawa katika Taifa la Iran, cha ajabu sioni kama Iran imewahi kulishtukia hilo na kuchukuwa hatuwa stahiki.

Cha kujiuliza hapa mbona Israel inao wana sayansi wa nuklia chungu mzima pale Domina jangwani Negev - wanazalisha mambom ya nuklia bila ya kukemewa au kuchukuliwa hatua yoyote, Serikali ya Israel walikataa ku-sign masharti ya umoja wa mataifa unao simamia matumizi bora ya nishati ya nuclear na kukagua vinu vya nuclear ili visizalishe weapon grade plutonium - Israel iligoma kusign masharti hayo na kuendelea kuzalisha mabom, Rais Kennedy alipo injia juu Israel na kusema kwamba lazima vinu vyake vya nuklia vikaguliwe mwaka 1964 kama wanavyo kagua Mataifa mengine - Rais Kennedy aliuwawa Nov,1963 hivyo ukaguzi haukutekelezwa mwaka ulio fuata kutokana na aliye kuwa anashikiza kuuwawa, kuna wanao sema kifo cha Kennedy kilichagiwa na shinikizo la Kennedy la kutaka vinu vya nuklia vya Israel kufanyiwa uchunguzi na shitika la umoja wa Mataifa linalo husika na masuala ya matumizi bora ya nishati za nuclear.

Kuuwawa kwa Rais Kennedy kulifanya Israel ivimbe kichwa sana na ku-defy maazimio yote ya Umoja wa Mataifa linapokuja suala la matumizi ya nuclear, Israel haitaki ihojiwe chochote kuhusu vinu vyake vya nuklia - badala yake Israel na USA wanaigeuzia kibao Iran wanaikalia kooni kuhusu masuala ya nuklia as if wao hawana haki ya kutumia nishati ya nuklia wakati Iran ndio ya pili Duniani kwa wingi wa madini ya Uranium.

Nawashangaa sana waswahili wanao tetea matendo ya kidhalimu ya taifa la Israel dhidi ya wana sayansi/wasomi wa taifa la Iran, wayahudi si watu wema hata kidogo, wao ndio waliwasaidia makaburu kuunda mabom ya nuklia barani Afrika au nyinyi hilo mmelisahau, mnafikiri lengo la makaburu na Israel walitaka kulenga mataifa yapi barani Afrika kama sio frontline states ambayo Tanzania himo, hawa si binadamu wa kutetewa au kuwaonea huruma hata kidogo, binadamu ambao walipanga na makaburu ku-NUKE front line states mnawezaje kuwakingia kifua na kuwaona ni watu wa maana sana - ukweli wa mambo Mayahudi ni binadamu wakatiri by default, msifikiri wanachukiwa huko Ulaya, North America na Latin America bila sababu - kuna tatizo si bure, hayo ni maoni yangu.
 
Nieleze jinsi inavyo endeshwa ww unaye jua.
Hili linakwenda nyuma sana katika historia. Si kitu cha kukifahamu tu kutokana na haya yanayoendelea kwa wakati huu. Isitoshe, ni somo pana sana na linahitaji muda wa kulitafakari na kuelewa.

Nitaweka vidokezo (hints):

Dunia imekuwa ikiendesha kwa nguvu na ushawishi wa kimaslahi. Hili limekuwepo tangu enzi na enzi.

Dunia hii ya sasa pia imeweza kuyakusanya mataifa makubwa, yenye nguvu na ushawishi katika nyanja mbalimbali ili ku-promote maslahi mbalimbali ya pamoja.

Maana yake ni kuwa, maslahi ya taifa lolote lile ndio msingi mkuu wa ushirikiano ama uhusiano wa kimataifa. Kila taifa hujaribu kuhalalisha matendo yake kupitia msingi huu wa maslahi yake ya kitaifa.

Kwa utafiti wa kina, tabia za mataifa mbalimbali huwa determined na maslahi mbalimbali ya mataifa hayo kimataifa, aidha maslahi binafsi kitaifa ama yale ya pamoja na mataifa mengine.

Pale linapotokea tishio linaloweza kuleta athari hasi katika maslahi kadha wa kadha ya pamoja, limekuwa ni jambo la kawaida sana mataifa makubwa [yenye ushawishi katika masuala mbalimbali] ama dunia kwa ujumla kuungana ama kushirikiana ili kupinga ama kulithibiti tishio hilo.

Tunafahamu kuwa kuna baadhi ya mataifa makubwa yenye uhasama hususani katika masuala ya kisiasa na kidiplomasia, lakini kwa utafiti wa kina, kuna muunganiko na ushirika wa namna moja ama nyingine katika masuala mengineyo yenye maslahi ya pande zote kwa mataifa hayo.

Nimedokeza kuhusiana na maslahi ya kitaifa:
Kumekuwa na ukinzani ama upinzani mkubwa sana pale linapokuja suala la maslahi ya kitaifa na yale ya kimataifa ama ya dunia kwa ujumla.

Taifa linaweza kuwa na maslahi yake ya kitaifa lakini maslahi hayo yakawa tishio kwa maslahi ya mataifa mengine ama dunia kwa ujumla. Hili limekuwepo tangu zamani sana kama ambavyo nimekwisha kusema hapo awali.

Mifano ni mingi sana kuhusiana na hili:
Tukirejea katika historia wakati wa Adolf Hitler, sera zake za upanuzi (expansionism) zilitajwa kama "maslahi ya kitaifa" ya Ujerumani kwa wakati ule. Lakini, maslahi haya yalitazamwa na mataifa mengine duniani kama tishio ama uhalifu mkubwa.

Matendo ya uvamizi wa kijeshi wa taifa moja dhidi ya taifa ama mataifa mengine yamekuwa yakifanyika tangu zamani sana kwa jina hili la "maslahi ya kitaifa". Sera za namna hii ama zinazofanana na hizi zipo mpaka sasa.

Mataifa makubwa, yenye ushawishi mkubwa katika masuala ya kijeshi na kiuchumi kama vile Marekani, China pamoja na Urusi yamekuwa na tabia au mienendo fulani ndani na nje ya mipaka yao ili kulinda maslahi yao. Tabia hizi na mienendo hii yaweza kuonekana kuwa ni halali kwa baadhi ya watu huku ikionekana kama uhalifu kwa wengine.

Operesheni kubwa za kijeshi za Marekani nje ya mipaka yake zimekuwepo miaka na miaka katika historia ya taifa hilo kwa jina la "kulinda maslahi ya kitaifa". Urusi nayo hali kadhalika. Operesheni hizi zimekuwa zikionekana kama tishio kwa maslahi ya mataifa mengine mbalimbali duniani.

Kumekuwa na migogoro ya kimpaka kati ya China na mataifa mengine, huku ikitamkwa kwa jina maarufu la "kupigania maslahi ya kitaifa" kwa upande wa China. Maslahi haya ya kitaifa ya China ni tishio kubwa kwa usalama wa mataifa mengine ambayo nayo yanalazimika kuingilia kati kupigania maslahi yao.

Mfano: China na India katika kipindi hiki. Pia katika historia, kati ya China na uliokuwa Umoja wa Kisovieti.

Mashariki ya kati pia kumekuwepo na migogoro ya kimaslahi kati ya mataifa mbalimbali; Israel dhidi ya Iran, nchi za Ghuba dhidi ya Iran n.k. Mfano; Iran inautazama uwepo wa Israel na utawala wake kama tishio kwa maslahi yake katika Mashariki ya Kati.

Iran nayo inapo-promote maslahi yake katika masuala ya kiimani, pia katika kufadhili makundi ya wapiganaji na uasi katika mataifa mengine kwa jina la "maslahi ya kitaifa" huonekana kama tishio kwa maslahi ya mataifa mengine bila kusahau yale yenye imani kinzani. Hivyo, si ajabu kuona mataifa haya yakishirikiana katika kupinga ama kuthibiti tishio la maslahi yao ya pamoja.

Mifano ni mingi! Dunia imekuwa ikiendeshwa ama ikijiendesha na itaendelea hivyo katika msingi wa maslahi huku yale ya wengi ama wenye nguvu na ushawishi yakiendelea kutamalaki.
 
Hili linakwenda nyuma sana katika historia. Si kitu cha kukifahamu tu kutokana na haya yanayoendelea kwa wakati huu. Isitoshe, ni somo pana sana na linahitaji muda wa kulitafakari na kuelewa.
Mkuu hilo nalijua sana tu ya kwamba mataifa yote huwa yanahalalisha uharifu yaliyo ufanya kwa kisingizio cha maslahi ya kitaifa na hata hiyo Iran ikiwemo.

Ila swali linakuja kwa nn Israel na Marekani wanapo halalisha mauaji wanayo yafanya kwa jina la masilahi ya mataifa yao nyinyi mnaona ni sawa na kuwasifia , ila Iran aki fanya kwa ajili ya kulinda masilahi yake mnamuona mbaya na kumpa kila aina ya jina baya?
 
Mkuu hilo nalijua sana tu ya kwamba mataifa yote huwa yanahalalisha uharifu yaliyo ufanya kwa kisingizio cha maslahi ya kitaifa na hata hiyo Iran ikiwemo.
Ila swali linakuja kwa nn Israel na Marekani wanapo halalisha mauaji wanayo yafanya kwa jina la masilahi ya mataifa yao nyinyi mnaona ni sawa na kuwasifia , ila Iran aki fanya kwa ajili ya kulinda masilahi yake mnamuona mbaya na kumpa kila aina ya jina baya?

What a splendid question!! Be blessed.
 
Mkuu hilo nalijua sana tu ya kwamba mataifa yote huwa yanahalalisha uharifu yaliyo ufanya kwa kisingizio cha maslahi ya kitaifa na hata hiyo Iran ikiwemo.
Ila swali linakuja kwa nn Israel na Marekani wanapo halalisha mauaji wanayo yafanya kwa jina la masilahi ya mataifa yao nyinyi mnaona ni sawa na kuwasifia , ila Iran aki fanya kwa ajili ya kulinda masilahi yake mnamuona mbaya na kumpa kila aina ya jina baya?
Mimi sijamsifia yeyote hapa.

Isitoshe, kama unafahamu kuhusiana na kile nilichokieleza, iweje uulize swali la namna hii? Umeielewa kweli concept niliyoieleza kwenye post yangu iliyopita?
 
Na nyinyi mna amini stori hizi za kuchonga,mfano - eti: tathimini ya siri ya Iran inasema itachukwa Iran miaka sita kumpata mwana sayansi mwenye kiwango cha kumfikia marehemu kitaaluma, eti kuuwawa kwake kuta rudisha nyuma Iran miaka sita katika juhudi zake za kuunda bom la nuklia, hizi ndizo stori za kila siku ambazo Israel na like mind wenzake uzi-manufacture kuhadaa Dunia kwa lengo.
Umetumia mtizamo wa kihistoria kuwahukumu Waisrael, ila mtizamo huu umeangalia upande mmoja. Historia inaonyesha kuwa Persia iliwahi kuwa taifa kubwa na lilisumbua sana na hata kuteka maeneo ya dola za karibu.

Matumizi ya Uranium kwa Israel siyo tishio kwa nchi jirani kwani licha ya kusemekana kuwa ana nukes, bado Iran amekuwa akitoa vitisho vya kumfuta kwenye ramani ya dunia.
 
Back
Top Bottom