Ripoti mpya inasema kuwa zaidi ya nusu (61%) ya wanawake waliuawa na wanaume nchini Uingereza mwaka 2018 ambao walikua ni waume zao

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Ripoti mpya inasema kuwa zaidi ya nusu (61%) ya wanawake waliuawa na wanaume nchini Uingereza mwaka 2018 ambao walikua ni waume zao au waliokua waume zao.

Matokeo ya uchunguzi huo yametokana visa ambavyo vimeshtakiwa au wahusika wamepatikana na hatia.

Sensa ya mauaji ya wanawake, ilifanywa na mwanaharakati wa unyanyasaji Karen Ingala Smith, anadai kwamba wanawake 149 waliuawa na wanaume 147 nchini Uingereza 2018.

Kiwango cha vifo kimeongezeka kwa vifo 10 kutoka kwa ripoti ya mwisho mnamo 2017.

Karen anasema alianza ripoti mwaka 2012 baada ya kusoma kwenye mtandao juu ya msichana ambaye aliuawa na mpezi wake wa kiume.

"Nilianza kutunza rekodi ya majina kujaribu tu na kubaini ni wanawake wangapi na ukweli ni kwamba -tangu wakati huo sijaacha kutunza orodha ya majina yao."

Alieleza ni kwanini anadhani wanawake ndio wenye uwezekano mkubwa wa kukabiliwa na ghasia za nyumbani kuliko wanaume.

"Ni tabia ambazo zinawachochea watoto wadogo wa kike na kium , halafu tunatarajia wanawake wawe wenye kuvutia kwa wanaume, wanafanywa kama vifaa.

"Wanawake wanageuzwa kuwa bidhaa na wanaume kuwa walaji. Na ni mlaji ambaye ana mamlaka kuliko kile wanachokinunua ," aliiambia Radio 1 Newsbeat.

Haki miliki ya pichaKAREN INGALA SMITH
Image caption
Karen alianza sensa ya mauaji ya wanawake wanaouliwa na wame a wapenzi wao mwaka 2012
Karen anasema kwamba kuna ukosefu wa usawa kutokana na kwamba takwimu zilizopo kuhusu mauaji huzingatia idadi ya jumla na sio wanawake wanaouliwa na wanaume, au kwasababu takwimu zao huwa ni za England na Wales pekee huku sensa ya mauaji ya wanawake huwa ni za Uingereza nzima.

Lakini ni muhimu kukumbuka kuwa uchunguzi wake unaangalia tu mauaji ambayo yameshtakiwa au kutolewa hukumu.

Kwa hivyo kuna uwezekano kuwa visa ambavyo havikukupatiwa suluhu ambapo muuaji hakufahamiwa na muathiriwa havikurekodiwa katika uchunguzi huu.

Kamishna wa Tume ya Wahanga wa mauaji ya wanawake, Dame Vera Baird awali aliiambia BBC kuwa idadi ya wanawake waliouliwa na wapenzi wao au waliokua wapenzi wao "haishangazi " lakini "inatisha sana ".

Alisema: "Kwa jina la wanawake hawa tunahitaji kuchukua hatua za haraka za kuingilia kati mapema kuzuwia mauaji haya."

Image caption
Visa vya mauji ya wanawake walio wanaouliwa na wapenzi wao au wame zao pia vimekua vikiripotiwa katika mataifa ya Afrika Mashariki mkiwemo Kenya na Uganda
'Utata wa kuondoka katika mahusiano'

Zaidi ya theluthi ya wahanga 149 walioorodheshwa katika ripoti ya awali walijaribu kuachana na wapenzi wao.

Lakini kuondoka katika mahusino ya mateso si rahisi kila mara.

"Tunafahamu kuwa kumuacha mwanaume anayekutesa ni suala tata na mara nyingi huwa ni hatari," anasema Sandra Horley kutoka shirika la msaada wa wakimbizi wa ndoa.

"La kusikitisha haishangazi kwamba wengi wa wanawake huuawa na wame zao wa sasa au waliokuwa wenzi wao, inatisha.

"Wanawake wanaendelea kuuawa kwa kiuwango hicho na wanaume, wanawaacha watoto bila mama, wazazi bila mabinti zao, familia bila wapendwa wao."

Unaweza pia kuoma:
Kwanini wanawake wanauawa Kenya?
Mwandishi mashuhuri kushtakiwa kwa mauaji Kenya
Mauaji ya wanawake yakithiri Canada
Mauaji ya kupindukia
Ni nusu ya mauaji katika ripoti yaliyoelezewa kama "mauaji ya kupindukia".

Sensa ya mauaji ya wanawake walio katika mahusiano ilielezea hili kama "ghasia ambazo huenda mbali kuliko zile za lazima kusababisha mauaji ya muhanga".

Idadi hii ilikua ni kubwa kwa wanawake wenye umri kati ya 25-34. theluthi mbili ya mauaji 40 katika umri huo yalielezewa kama mauaji ya kupindukia.

Licha ya takwimu hizi, Karen anasema ukomo wa umri ambao sio kigezo kinachosababisha wanawake kuuliwa na wanaume.

"Hakuna jamii moja, umri au kikundi cha kijamii ambacho kimo katika hatari zaidi ya kingine, hakuna mwanamke aliye salama kwa mauaji ya mwanamume ."

Chanzo: BBC Swahili
1582283084778.png
 
Wadau,
Ripoti mpya inasema kuwa zaidi ya nusu (61%) ya wanawake waliuawa na wanaume nchini Uingereza mwaka 2018 ambao walikua ni waume zao au waliokua waume zao. Matokeo ya uchunguzi huo yametokana visa ambavyo vimeshtakiwa au wahusika wamepatikana na hatia.
image-2.jpg

Sensa ya mauaji ya wanawake, ilifanywa na mwanaharakati wa unyanyasaji Karen Ingala Smith, anadai kwamba wanawake 149 waliuawa na wanaume 147 nchini Uingereza 2018.

Kiwango cha vifo kimeongezeka kwa vifo 10 kutoka kwa ripoti ya mwisho mnamo 2017.

Karen anasema alianza ripoti mwaka 2012 baada ya kusoma kwenye mtandao juu ya msichana ambaye aliuawa na mpezi wake wa kiume.

“Nilianza kutunza rekodi ya majina kujaribu tu na kubaini ni wanawake wangapi na ukweli ni kwamba -tangu wakati huo sijaacha kutunza orodha ya majina yao.”

Alieleza ni kwanini anadhani wanawake ndio wenye uwezekano mkubwa wa kukabiliwa na ghasia za nyumbani kuliko wanaume.

“Ni tabia ambazo zinawachochea watoto wadogo wa kike na kium , halafu tunatarajia wanawake wawe wenye kuvutia kwa wanaume, wanafanywa kama vifaa.

“Wanawake wanageuzwa kuwa bidhaa na wanaume kuwa walaji. Na ni mlaji ambaye ana mamlaka kuliko kile wanachokinunua ,” aliiambia Radio 1 Newsbeat.

Picture of Karen
Karen alianza sensa ya mauaji ya wanawake wanaouliwa na wame a wapenzi wao mwaka 2012
Karen anasema kwamba kuna ukosefu wa usawa kutokana na kwamba takwimu zilizopo kuhusu mauaji huzingatia idadi ya jumla na sio wanawake wanaouliwa na wanaume, au kwasababu takwimu zao huwa ni za England na Wales pekee huku sensa ya mauaji ya wanawake huwa ni za Uingereza nzima.

Lakini ni muhimu kukumbuka kuwa uchunguzi wake unaangalia tu mauaji ambayo yameshtakiwa au kutolewa hukumu.

Kwa hivyo kuna uwezekano kuwa visa ambavyo havikukupatiwa suluhu ambapo muuaji hakufahamiwa na muathiriwa havikurekodiwa katika uchunguzi huu.

Kamishna wa Tume ya Wahanga wa mauaji ya wanawake, Dame Vera Baird awali aliiambia BBC kuwa idadi ya wanawake waliouliwa na wapenzi wao au waliokua wapenzi wao “haishangazi ” lakini “inatisha sana “.

Alisema: “Kwa jina la wanawake hawa tunahitaji kuchukua hatua za haraka za kuingilia kati mapema kuzuwia mauaji haya.”

mauaji ya wanawake
Visa vya mauji ya wanawake walio wanaouliwa na wapenzi wao au wame zao pia vimekua vikiripotiwa katika mataifa ya Afrika Mashariki mkiwemo Kenya na Uganda
‘Utata wa kuondoka katika mahusiano‘

Zaidi ya theluthi ya wahanga 149 walioorodheshwa katika ripoti ya awali walijaribu kuachana na wapenzi wao. Lakini kuondoka katika mahusino ya mateso si rahisi kila mara.

“Tunafahamu kuwa kumuacha mwanaume anayekutesa ni suala tata na mara nyingi huwa ni hatari,” anasema Sandra Horley kutoka shirika la msaada wa wakimbizi wa ndoa. “La kusikitisha haishangazi kwamba wengi wa wanawake huuawa na wame zao wa sasa au waliokuwa wenzi wao, inatisha.

“Wanawake wanaendelea kuuawa kwa kiuwango hicho na wanaume, wanawaacha watoto bila mama, wazazi bila mabinti zao, familia bila wapendwa wao.”

Ni nusu ya mauaji katika ripoti yaliyoelezewa kama “mauaji ya kupindukia”. Sensa ya mauaji ya wanawake walio katika mahusiano ilielezea hili kama “ghasia ambazo huenda mbali kuliko zile za lazima kusababisha mauaji ya muhanga”.

Idadi hii ilikua ni kubwa kwa wanawake wenye umri kati ya 25-34. theluthi mbili ya mauaji 40 katika umri huo yalielezewa kama mauaji ya kupindukia. Licha ya takwimu hizi, Karen anasema ukomo wa umri ambao sio kigezo kinachosababisha wanawake kuuliwa na wanaume.

1582282730040.png
unnamed-1.jpg
Violent young man threatening his girlfriend with his fist outdoors

“Hakuna jamii moja, umri au kikundi cha kijamii ambacho kimo katika hatari zaidi ya kingine, hakuna mwanamke aliye salama kwa mauaji ya mwanamume .”

Chanzo BBC

Na bado itaongezeka tu hata duniani kote. Maana hali si shwari kabisa!

Kwasasa mwanamke ukiolewa tu, heri utulie tu. Mambo ya kuanza usaliti nje ni hatari kubwa inayowakabiri ke kote duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom