Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

Watu wanafukua bwana acha 2 na wanaweka wazi. Watetezi wa serikali mje muweke mzani sawa kama mtaweza.Tunashukuru wote waliomsakama Tundu Lisu tungeyajuaje haya?
 
Lisu is right. Angalia hukumu za anayeitwa jaji Shangwa, A. hata language aliyotumia unaona kabisa kuwa huyu ana mapungufu hastaili kuwa na mamlaka ya jaji.
 
Tatizo ni kuwa siku bSpika au naibu wake atakaposimama kutoa 'hukumu' utasikia tunaambiwa kuwa "Mheshimiwa Tundu Lissu wala hakutoa ushahidi, yeye ameleta maelezo mareeeeeeefu."
 
Duuuh ndo walitaka kuumbuliwa wao wenyewe....Tundu is very smart.....kama majaji wenyewe ndio hawa Kesi ya Lema na Kesi ya Mahanga ni halali ziamuliwe kihuni vile....any way freedom is coming tommorow
 
Mh. Lissu hii nondo ya ya nguvu kwelikweli! Nadhani kuna watu wakiisoma lazima hapa wajiulize tena juu ya yale wanayoyafanya wakidhani wa-TZ tumelala usingizi! Keep it up my brother Lissu tuko pamoja!
 
Ngoja nikasome sheria kidogo ili nijiridhishe juu ya wale waliokuwa wakimkosoa Lissu katika hotuba yake ya kambi rasmi ya upinzani bungeni na kuwatetea watu hawa, tena kwa maneno makali.

Walifanya hayo kwa mujibu wa kifungu gani cha katiba au sheria za bongoland! Nakwenda pia kufuatilia kama waliyajua haya mapema kabla ya kuanika udhaifu wao bungeni. Nikitoka huko nakuja "kubomoka"!
 
Kuna Mtu anaitwa Werema! eti ndio mwanasheria mkuu wa serikali alafu eti nae ni jaji.. Jamaa kiukweli Sijawahi hata kuhisi tu ni namna gani aliweza kua jaji!
 
Huu muhimili unahujumiwa makusudi na executive, wanaogopa kama kukiwa na strong judiciary system watakabwa sana kwenye madudu yao thats why wanateua wajinga kama Wrema kua jaji Mkuu.

Serikali inajua sasaihvi muhimili mmoja(BUNGE,) hauko upande wao kwa sababu ya nguvu ya upinzani, so ni lazima wahakikishe wanaweka watu wao(wajinga wajinga) huko mahakamani, but what we promise is.2015 is on the corner.

Msishangae hao vibaraka wao wakafungua kesi kesho then wakasema hii issue iko mahakamani ili isijadiliwe coz tayari washashtuka ushahidi unawaumbua.
 
Sasa mbona naona kama vile amehatarisha maisha yake? Au mnasemaje ndugu zangu because he has put everything black and white so that we can know what is happening in this nation.

Halafu Mwanasheria Mkuu anapinga, bungeni alilidanganya bunge tukufu achukuliwe hatua mara moja au kama inawezekana atolewe nje hata kama vikao vimekwisha.

Sasa naamini CDM can lead this nation to our destiny.
 
Kama mahakama zetu ndio zimejaa uozo namna hiyo basi kudai haki yako mahakamani ni kama kucheza kamali.

Asante sana Tundu Lissu kwa kutufungua macho.

Hukumu pekee ya kuaminiwa kwa sasa ni nguvu ya umma.
 
I want to meet Mr Hon Tundu Lissu just to give him HI5 and to congratulate him, also i think he need people to stand with him in Prayers. He has a lot of good things in him.
 
Ni kweli mkuu. Hata ukiangalia kwa makini hiyo taarifa ya Lissu inaashiria kuna suport kubwa ya kitaarifa aliyopatiwa na watu wa ndani kwenye idara ya mahakama.

Usisahau pia kuwa Lissu mwenyewe ni wakili wa mahakama kuu! Kwa hiyo Suport unayoiongelea ndugu yangu hapa si tu ya uswahiba na kuchoshwa kwa majaji kuona tasnia ya sheria IKISIGINWA na watu wenye hulka ya kulipa fadhila kwa vyeo bila kuangalia matakwa ya sheria katika nafasi hizo, bali ndo kero za "viwanja vyake"!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Siku moja nilijiuliza hawa majaji wanateuliwa kwa fujo sana kulikoni? Hasa wanawake,masuali ndani yakawa mengi sana.

Sasa nimegundua kuwa Mh. Rais hajui taratibu zinazotakiwa na hajazisoma kwa hiyo amefanya makosa na sio yeye tu hata waliomtangulia, sasa atatengua?
 
Sasa ndio utaelewa ni kwa nini kesi nyingi Tanzania zimejaa maamuzi yenye utata. Well done Lisu
 
Back
Top Bottom