Ripoti maalum ni kweli kuna dawa za kuongeza nguvu za kiume?

nelly poul

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
1,276
2,000


UPUNGUFU wa nguvu za kiume umekua ni tatizo kubwa sana nchini, kwa wanaume walio katika ndoa na hata wale ambao bado hawajaoa. Watu wengi wamekuwa wakisumbuka huku na kule katika kutafuta ufumbuzi au tiba ya tatizo hilo, huku wengine wakishikwa na wasiwasi wa maisha yao ya kwenye ndoa au watarajiwa wao. Tatizo la nguvu za kiume limechangia kuvunjika kwa ndoa nyingi, na mahusiano mengi kuharibika.

Hata hivyo kwa wanaume wenye umri mkubwa, upungufu wa nguvu za kiume unaweza usiwe ni tatizo kubwa sana kwani mwili unakuwa umechoka, na hata aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla aliwahi kusema kwamba, umri mkubwa kwa wanaume huchangia tatizo hili.

KINACHOSHANGAZA WENGI
Kitu ambacho kinaweza kukushangaza ni uwepo pia wa vijana wadogo wa kati ya miaka 19 hadi 25 ambao nao wanalalamika kuwa wana tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Gazeti la Uwazi liliamua kufanya utafiti kwa kuzungumza na wadau wa afya ili kuweza kubaini kama ni kweli tatizo hilo lipo na kama kweli kuna dawa ambazo zinaweza kuongeza nguvu za kiume kwa waathirika wa tatizo hilo.

Kwa mujibu wa Mtaalamu wa Lishe, Abdallah Mandai, zipo njia zinazosaidia kurudisha nguvu za kiume zilizokuwa zimepotea kwa kutumia vinjwaji na vyakula. Mandai anasema ni vema kuepuka vinywaji vyote vyenye sukari nyingi kwani ni adui mkubwa sana wa afya yako hasa wakati unataka kurudisha nguvu za kiume. “Kula vyakula asili na nafaka ambazo
hazijakobolewa, kula matunda kwa wingi pamoja na mboga za majani. Utafurahia maisha ya kula vyakula hivyo vya asili na utakuwa imara katika tendo la ndoa,” anasema. Anaongeza: “Tafiti zinaonesha kwamba pombe inakupa hamu au shauku ya kufanya tendo la ndoa lakini inakunyima uwezo wa kufanya tendo hilo, kwani hupunguza kiwango cha maji mwilini, hivyo epuka pombe.

“Hakikisha mwili wako unaupa madini ya msingi kama zinki, chuma, selenium, manganese na vitamini nyingine, kwani madini haya ndiyo yanafanya mwili wako ufanye kazi katika kiwango stahiki. “Madini haya huwezesha kuendesha shughuli za mwili yani ‘enzymes’ kufanya kazi katika kiwango kizuri na kuimarisha mwili wako. Madini haya hupatikana katika mboga, samaki na matunda ya aina mbalimbali.”

Naye Dk. Leopord Mwinuka anasema watu wengi wamelemewa na magonjwa kwa sababu tu mwili haupati damu ya kutosha kwenda sehemu mbalimbali kama vile ubongo, ini na figo ambazo ndiyo sehemu zenye kuufanya mwili wako ufanye kazi katika uhalisia wake. “Sehemu nyeti ya kiume ili isimame kwa uimara, inatakiwa ipate damu ya kutosha. Kufanya mazoezi hupunguza kiwango cha mafuta katika mishipa ya damu na kuiwezesha kupeleka damu ya kutosha katika maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo sehemu hiyo nyeti,” anasema Dk. Mwinuka, ambaye amekuwa akitoa elimu ya afya kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Anashauri kuwa, kunywa maji ya kutosha kila siku, usingoje mpaka kiu ikupate. Mtu mzima anapaswa kunywa maji glasi nane mpaka 10 kwa siku. Maji husaidia kuongeza kiwango cha damu na kuondoa sumu mbalimbali mwilini.

Naye Dk. Godfrey Chale aliyewahi kufanya kazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Temeke anasema, ufanyaji wa tendo la ndoa huwa unahusisha mambo mengi. “Unaweza ukawa umekamilika kiafya lakini ukashindwa kufanya ngono kwa kuwa una msongo wa mawazo. Hakikisha kabla ya kwenda faragha na mpenzi wako, unaituliza akili na usiwaze mambo mengine nje ya tendo unaloenda kulifanya. Hii itakupa muda mzuri wa ubongo wako kupeleka damu ya kutosha katika uume wako.”

Dk. Chale anashauri: “Yeyote anayetumia dawa za kuongeza nguvu zilizothibitishwa kama viagra, ni vyema atumie dozi yake baada ya kushauriwa kitaalamu na pia awe karibu na mwenza wake kwa sababu vinginevyo anaweza kujipa mateso makali ya mwili.

“Watu wenye matatizo ya nguvu za kiume wanapaswa kuonana na daktari, hizo dawa za asili kiukweli zina nguvu sana na mtu akitumia asipopata mwenza kwa wakati huwa ni hatari,” anasema Dk. Chale.

Daktari huyo aliwataja baadhi ya watu ambao wako katika matatizo ya kutokuwa na nguvu za kiume kuwa ni wale wenye magonjwa kama ya kisukari, msongo wa mawazo, shinikizo la damu, tezi dume, watumiaji wa dawa za kulevya na pia wavuta sigara. Anasema njia sahihi ya kuondokana na matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume ni kufanya mazoezi, kula vyakula kwa kuzingatia lishe bora na pia kushiriki mapenzi na wapenzi ambao wanawapenda kwa dhati na siyo kila mpenzi.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
47,232
2,000
Hayo ni matatizo ya ndani, usiombe watu wametoka Tena kwa nguo za kufanana waliitwa mr and mrs kuta zinafucha mengi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom