Ripoti kamati ya 'Mzee Ruksa' kuanikwa bungeni Oktoba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti kamati ya 'Mzee Ruksa' kuanikwa bungeni Oktoba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Sep 24, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kwani iliundwa na Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (Nec), kufuatilia mienendo ya wabunge wanaoishambulia serikali kwa ufisadi.


  Na inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake katika mkutano wa 17 wa Bunge unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Oktoba mwaka huu.

  Uchunguzi wa kutoka vyanzo mbalimbali vya uhakika wa habari ulifanyika na kubaini kwamba, ripoti hiyo itatolewa mwishoni wa juma la kwanza la mkutano huo unaoanza Oktoba 27.

  Kwa mujibu wa vyanzo hivyo na habari zake kudhibitishwa na maafisa kadhaa wa bunge na wajumbe wa Nec.

  Kwnai ripoti hiyo itatolewa kwa wabunge wa CCM wakiwa Kamati ya wabunge wa Chama hicho ambayo kwa kawaida hukutana katika ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma.

  Afisa mmoja mwandamizi wa Bunge ambaye jina lake kapuni hakuwa kimya alisema, ripoti hiyo itatolewa mwishoni mwa juma kati ya tarehe 30 na 31 Oktoba.

  Alisema anachojua kamati hiyo itatoa taarifa yake mwishoni mwa juma la kwanza la mkutano ujao wa Bunge. Kwa mantiki hiyo inaweza kuwa kati ya Oktoba 30 na Oktoba 31.

  Kamati hiyo imesheheni wajumbe wapatao watatu ambao ni Alhaj Ali Hassan Mwinyi, spika wa zamani, Pius Msekwa na Waziri wa zamani, Abdurahman Kinana iliundwa na Nec Agosti 18, mwaka huu.

  Mbali na majukumu hayo, kamati ilipewa kazi ya kuhakikisha wabunge hao wa CCM na Wawakilishi wa Chama hicho katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wanarudi katika nidhamu ya Chama kwa kuacha malumbano yasiyokuwa ya msingi.

  "Bunge limeanza kuwa kama mchezo wa (kikundi cha televisheni cha vichekesho, (The Comedy) ," alisema katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, John Chiligati alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kikao hicho.
  http://www.darhotwire.com/home/news/2009/09/22/ripoti_kamati_ya_mzee_ruksa_kuanikwa_bungeni_oktoba_.html
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii ripoti ianikwe bungeni, kwani ni bunge ndo liliomba ifanywe?
   
Loading...