Ripoti: Israel ilimsaidia Saudia Arabia moja kwa moja katika kumuu mwandishi jamal khashogi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Israel ilitoa msaada wa kijasusi kwa Saudia katika mauaji ya Khashoggi
Imebainika kuwa shirika moja la kijasusi la utawala wa Israel lilitoa msaada mkubwa kwa ufalme Saudi Arabia ili kufanikisha mauaji ya mwandishi habari Jamal Khashoggi ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa ufalme huo wa kiimla.
Hayo yamefichuliwa na gazeti la New York Times ambalo limeandika kuwa shirika moja la ujasusi wa mitandaoni la Israel lilitumika katika kufuatilia mawasiliano ya simu ya Khashoggi na kuwakabidhi wakuu wa Saudia taarifa zote za mawasiliano ya mwandishi huyo ambaye aliuawa kinyama. Taarifa zinasema shirika la ujasusi wa mitandaoni la NSO Group la Israel lilinasa mawasiliano yote baina ya simu za mkonono za Khashoggi na mpinzani mwigine wa Saudia aliye uhamishoni. Mawasiliano hayo yalinaswa kwa kutumia programu ya Pegasus ya ujasusi ambayo hubadilisha simu erevu au smartphone ya mlengwa kuwa chombo cha ujasusi. Mpinzani Msaudi anayeishi uhamishoni Canada Omar Abdulaziz sasa amewasilisha mashtaka dhidi ya shirika hilo. Katika mashtaka yake anataka pia kuwepo uchunguzi zaidi kuhusu ushirikiano wa kijasusi baina ya Israel na Saudi Arabia pamoja na tawala zingine za kifalme katika Ghuba ya Uajemi.
Jamal Khashoggi, aliyewahi kuwa msiri na mwandani wa aila ya kifalme inayotawala nchini Saudi Arabia, lakini hatimaye akageuka kuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Aal Saud, aliuliwa na mwili wake kukatwa vipande vipande, alipoingia kwenye jengo la ubalozi mdogo wa nchi hiyo mjini Istanbul, Uturuki mnamo tarehe Pili Oktoba ili kukabidhi hati zake kwa ajili ya mpango wake wa kufunga ndoa.
 
Mauwaji ya Khashogi hayakubaliki kwa namna wala mizania yoyote; ni zaidi ya unyama alitendewa. Kosa lake ni usaliti; huwezi leo ukashirikiana na fulani halafu kesho ukawageuka kutoa siri zao. Hata Uislamu unafundisha anayebadili dini adhabu yake ni kifo maana ulishazijua "siri" zote halafu unageuka! Na hilo kampuni la kizayuni ni la serikali au wafanya biashara?
 
Israel wakijamba mtasema amejamba vizuri hata akifirwa mtasema kafirwa vizuri na kumtesa yesu walimtesa vizuri pia.
ata kama lkn angalia wale watu walivyoboronga hyo misheni alafu eti uamini kuwa israel walikuwa nyuma ya game hilo?
 
Unahitajika ujasusi gani kumfuatilia mtu ambaye ana miadi ya kwenda kwenye moja ya balozi zako kupatiwa haki zake za Kiraia? Wanajua anakuja so watamsubiri tu au wanataka kutuambia kuwa alitekwa?
Serikali ya Saudia imefanya mauaji ya kishenzi na kipumbafu bila msaada kutoka popote pale.
 
Israel wakijamba mtasema amejamba vizuri hata akifirwa mtasema kafirwa vizuri na kumtesa yesu walimtesa vizuri pia.
Astaghfilulah... Astaghfilulah laadhim... Astaghfilulah kama mchanga wa bahari.
 
ata kama lkn angalia wale watu walivyoboronga hyo misheni alafu eti uamini kuwa israel walikuwa nyuma ya game hilo?
Kwani walivyoboronga syria au walivyoboronga wakati wa mapambano yao na Hizbollah ilikuwaje? Naamini ukiambiwa kati ya israel na mungu unampenda nani nadhani utajibu israel
 
Source ni gazeti la marekani, lakin hapa wairan na warusi wa JF wanasita kusema hii ni propaganda za magharibi kwa kuwa ni habar wanayopenda kuisikia
 
Back
Top Bottom