Ripoti: Israel ilifanya ujasusi kwa niaba ya Kabila wa DRC

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,175
2,000
Ripoti: Israel ilifanya ujasusi kwa niaba ya Kabila wa DRC

Uchunguzi uliofanywa na kanali moja ya televisheni ya Israel umefichua kuwa, shirika la kijasusi la utawala huo haramu la 'Black Cube' lilikodiwa na aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila kwa ajili ya kufuatilia nyendo za wapinzani na wakosoaji wake.

Televisheni ya Uvda imenukuu mmoja wa majasusi wa zamani wa shirika hilo la Kizayuni ambaye amesema Kabila aliwapa kazi ya kufuatilia mikutano, mikakati na harakati zote za wapinzani na wakosoaji wake.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, mkurugenzi wa shirika binafsi la kijasusi la utawala huo haramu la Black Cube, Dan Zorella alikutana na Kabila mwishoni mwa mwaka 2015, na kikao hicho kilikuwa moja ya vikao vilivyozalisha operesheni iliyopewa jina la 'Coltan' iliyokusudia kukusanya taarifa za kintelijensia kutoka kwa waliokuwa wanapinga na kukosoa utawala wa Kabila kipindi hicho.

Televisheni hiyo ya Kizayuni imeripoti kuwa, Kabila alikodi shirika hilo la kijasusi la Israel ambalo pia linafahamika kama 'Mamluki wa Karne ya 21' kwa ajili ya kuwafuatilia pia watu wa karibu wa familia yake ambao hakuwa na imani nao.

Uamuzi wa Kabila wa kukataa kung'atuka madarakani baada ya kipindi chake cha uongozi kumalizika Disemba 2016 kilichochea maandamano kadhaa ya upinzani na kusababisha makumi ya watu kuuawa mbali na kushajiisha uasi wa makundi yanayobeba silaha katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ilitoa taarifa kadhaa kulaani mauaji na ukandamizaji huo dhidi ya wapinzani uliofanywa na maafisa usalama katika enzi za Kabila.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
49,842
2,000
Mnaotaka mademu wenu mjue wanachiti na nani, fursa iko wazi, nendeni muwaone Israel watawasaidieni
 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
35,393
2,000
Sio rocket science,wizara ya ulinzi ya israel ilinunua kampuni moja staterup ilikuwa ikijihusisha na kuhack mawasiliano Pegasus kama sikosei,sasa hii kampuni huwa inafanya kazi na madictator duniani kuhack mawasiliano ya wapinzani wa tawala mbalimbali,refer kasheshe iliyomkuta khashoggi ya kucharangwa mapanga,chanzo ni hii kampuni kuhack mawasiliano yake akaonekana ana nia ovu dhidi ya ufalme wa saudi,
israel wanakufungia system ya kutrace mawasiliano kwa dola 500,000,kwahiyo sio ajabu kabila kutumia huduma ya hii kampuni kuwapeleleza wapinzani wake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom