RIPOTI: Gaddafi aliuawa kimakosa

Naona umeanza kutoka povu kwa marehemu. Wewe haujawahi kufika Libya na story sijui za kuhudumiwa kila kitu na Ghadafi umezisoma mtandaoni. Nchi zozote hutangazwa kwa mazuri tu mabaya hufichwa. Ghadafi ni dikteta na sifa mojawapo ya dikteta ni kutaka kuongoza yeye tu (Kung'ang'ania madaraka). Ghadafi yumo kwenye kapu moja na Mugabe, Kurunzinza, Kagame na wengine. Wewe nchi ya watu wote unataka kuongoza wewe tu. Wewe kama nani? Ghadafi alikuwa siyo mtu mzuri kwasababu alikuwa anatengeneza mazingira ya kuongoza yeye tu na kizazi chake na unayoona Libya ni kwasababu ya uongozi mbovu uliuweka na Ghadafi wa kumtegemea mtu mmoja tu. Angekuwa mtu mzuri angekuwa ameshaanda watu wengine wa kuongoza nchi. Ghadafi anajulikana kama dikteta. Kuanza upya siyo ujinga. Kwa wanayopitia watu walibya ndiyo itawafanya nchi iwe ya watu wote na siyo mali ya mtu. Afadhali wameliua maana alitaka ajimilikishe nchi kama yake. Safi sana Marekani kwa kuwaondoa madikteta. Mimi siamini Ghadafi alikuwa mtu mzuri, angekuwa mtu mzuri wanaLibya wasingeshika bunduki kupigana na kiongozi dikteta ambaye hataki kuachia nchi yao.
Kwahiyo sasa hivi watu wanapata mgao wa mauzo ya mafuta kama ilivyo kuwa hapo awali? Sasa hivi wanafunzi wanasoma bure? Sasa hivi huduma za afya ni bure?

Unacho shindwa kuelewa kwann Marekani walimwondoa Gadaff ni mipango/mawazo yake ya kuiunganisha Africa na kuna mkutano mmoja wa AU Gadaf alisema ni lazma umoja wa Africa waanzishe Bank Of Africa kitu ambacho hakikuwapendeza wazungu ndiyo kilicho muondoa uhai wake

Demokrasia inatumia tu kutudidimiza kwenye umaskini, kwanini Malkia wa uingereza hicho kiti wasipewe familia nyingine? Huo siyo udikteta?
 
Angekuwa kiongozi makini angejenga mifumo thabiti ya utawala ktk nchi yake, iweje afe yeye mtu mmoja nchi yote iparaganyike?
Sasa mkuu uoni njia iliyotumika kwamba ni vita,sasa kwenye vita kuna mfumo gani utafanya kazi? Ndio maana mimi nasema walibya ndio wenye makosa wametumia njia isiyo sahihi kuobdoa tatizo.
 
Viongozi wetu ndio kizingiti kikuu
Vitu vyengine tujaribu kufikiria yani matatizo yoooote ya afrika sababu iwe viongozi wetu tu,wenzetu huko watauliza kwani hao viongozi wanatoka wapi na wanachaguliwa na nani? Yani kwamba sie wenyewe raia tupo sawa kabisa ila viongozi tu ndio tatizo!
 
Mnavyozidi kubishana hapa hiyo ndio Devide &Rule yenyewe. Tunapoteza muda kushindanda juu ya uwelewa wa Mambo ya watu ilhali utatuzi wa matatizo yetu wenyewe ni shida kubwa. Mwafrika alisharogwa na Mzungu kiakili. Utumwa tulionao sasa ni hatari kuliko hata ule wa zamani wa kufungwa minyororo. Vijana wanazidi kuwa wajinga kila siku zinavyoongezeka.
 
Hii ni baada ya waarabu wenzie kumshtukia kuwa anataka yeye ndiye awe bosi wa Arab league
alistahili kwa kwa wengi walikuwa vilaza na wengine wakikubali kudhurumiwa na kupelekeshwa na mataifa tajiri ya ulaya huku wao wakiwa ni matajiri wa mafuta uchumi unaoweza kuwatosheleza na kuwa na nguvu
 
Hii ni baada ya waarabu wenzie kumshtukia kuwa anataka yeye ndiye awe bosi wa Arab league
The guy was selfish and arrogant. Ni vile kitanda usicholalia hujui kunguni wake na tunaongozwa na mihemko. Mtu gani anayejifikiria kuwa yeye anajua yote na hakuna mbadala wake?
 
Nimekwambia hata kila mwezi kuwe kunafanyika uchaguzi na kubadilishwa rais hiyo haitofanya kila raia kupata hiyo nafasi ya urais hivyo lazima tu hiyo nafasi iwe kwa watu wachache tu,sasa iweje raia wa kawaida aingie vitani kisa kiongozi aliyepo madarakani hataki kuwaachie wenzake madaraka? Ndiyo maana nakwambia mara nyingi viongozi wa haya mapambana ya sijui kumtoa kiongozi asiyetaka kuachia madaraka huwa ni wenye uchu wa madaraka au masilahi yao binafsi tunaona akina Museven na wenzie. Huyo Mugabe katolewa na si kwamba alitoka tu mwenyewe.

Mbowe anajiona hana mbadala na watu wanaunga mkono hilo ila watu hao hao ndio hupinga kwa Magufuli kujiona hana mbadala.
We jamaa sijui umeumbwaje! Kwani kuna mtu kasema kila mwananchi kwenye nchi anapaswa kuwa rais? Unaexagerate ili ionekane ni jambo lisilo na manufaa kubadili kiongozi kwa amani. Hizi ndio mimi huziita akili za kuabudu binadamu.

Ndugu yangu, kuchaguliwa kuwa kiongozi haimaanishi wewe ndio una akili sana kuliko watu wote kwenye hilo taifa. Unapofikia kuamini kuwa watu wengine wanapaswa kukusikiliza wewe tu kwa kuwa wewe umekuwa kiongozi huo ni ufinyu wa fikra. Hata hili neno MADARAKA unalopenda kulitumia linanionesha nafsi ya kitumwa, ndio maana mimi hupenda kutumia neno UONGOZI na sio madaraka.

Kuwepo kwa serikali mbadala katika nchi kunaleta tija na msukumo kwa walioshika usukani kufanya vyema zaidi ili waendelee kuwepo kwenye uongozi. Hawa mnaowasujudia kana kwamba hawatakufa ndio tatizo katika hizi nchi zetu. Taifa linapaswa kuwa na VIONGOZI walio tayari tayari kuliendeleza mara aliyepo kwenye uongozi atapomaliza muda wake. Hawa miungu watu, iwe wametolewa na wananchi au MAUTI ni shida sana nyuma yao kwa kuwa hawanaga succession plan.

Yawezekana wengi wenu mnadhani huyu Marehemu Gadaffi alikuwa akigawa fedha zake kwa wananchi...hizo ni fedha za Libya, ni rasilimali za Libya, na ni mali ya Walibya. Angekuwa ameasisi mfumo imara wa uongozi kwa nchi yake, Libya ingeendelea kuwa juu hata baada ya yeye kuondoka. Naamini wewe ni mmoja wa ambao wanadhani ni haki kumiliki bastola ya dhahabu huku akiwagawia fedha anaowataka na kuwanyima anaowataka. Basi hilo ndio lilikuwa anguko lake. Alicha nyufa kwa kulitenga kundi fulani.
 
Hivi umenielewa kweli mkuu? Hakuna nilipopinga kubadili kiongozi ila nachopinga mie ni huko kubadili kiongozi kufanywa ni muhimu sana kiasi cha kuchukua hadi uamuzi wa kuingiza nchi vitani kisa kubadili kiongozi,yani ukaharibu nchi nzima na maelfu ya kufa na kuwa wakimbizi kisa kubadili kiongozi hili ndiyo ambalo mie nalipinga. Hivi leo watanzania tuchukuwe uamuzi wa kuingiza Tz kwenye vita kisa Ccm inang'ang'ania madaraka na haitaki kutoka? Kwako wewe huo ni uamuzi sahihi?

Tatizo lenu katika hili jambo mnamuangalia Gadafi na kuona kakomolewa na si kuangalia athari za uamuzi wa wanazopitia walibya sasa na ndio maana lawama mnamtupia Gadafi tu na wanachi wa Libya mnataka tuone kwamba walilazimika kufanya hivyo kwamba hawakuwa na jinsi.
 
Kuna kundi linawapenda sana mabeberu Kuliko wanavyoipenda Nchi yao

Ila mi Sijawahi kumkubali gadafi alikuwa anamsaidia mla nyama za watu Id amin ili tushindwe vita
Lkn kwa uongozi mathubutu wa Nyerere tulimchapa
Mpaka leo unaamini Idd Amin alikuwa anakula nyama za watu?
 
Hivi umenielewa kweli mkuu? Hakuna nilipopinga kubadili kiongozi ila nachopinga mie ni huko kubadili kiongozi kufanywa ni muhimu sana kiasi cha kuchukua hadi uamuzi wa kuingiza nchi vitani kisa kubadili kiongozi,yani ukaharibu nchi nzima na maelfu ya kufa na kuwa wakimbizi kisa kubadili kiongozi hili ndiyo ambalo mie nalipinga. Hivi leo watanzania tuchukuwe uamuzi wa kuingiza Tz kwenye vita kisa Ccm inang'ang'ania madaraka na haitaki kutoka? Kwako wewe huo ni uamuzi sahihi?

Tatizo lenu katika hili jambo mnamuangalia Gadafi na kuona kakomolewa na si kuangalia athari za uamuzi wa wanazopitia walibya sasa na ndio maana lawama mnamtupia Gadafi tu na wanachi wa Libya mnataka tuone kwamba walilazimika kufanya hivyo kwamba hawakuwa na jinsi.
Hata na wewe nafikiri huelewi kitu kimoja...sio Walibya wote hawakumpenda Gaddaffi. Lakini mnataka tuamini kuwa wote walikuwa wanapewa hizo fedha za bure na elimu na manufaa mengine. Nilikuuliza swali, wale wanaoishi Benghazi kwenye yale mabanda ya makuti ya mitende, wao nao wangekuwa na hofu na kuondokewa na amani?

Kwa nini mnaamini kuwa Walibya ni wajinga sana kiasi kwamba wanaweza tu wakaambiwa na Marekani 'mtoeni huyo' na wao wakaanza fujo? Nikukumbushe kwa mujibu wa maneno yenu kuwa watu wenyewe hao wamelipiwa elimu bure hadi chuo kikuu on which I expect Libya kuwa na graduates wengi kuliko nchi nyingine %wise
 
  • Thanks
Reactions: 365

Aisee! Labda nikuulize ni sababu ipi iliyowafanya walibya kuona bora waingie vitani? Ni kwa sababu ya hao waliyokuwa wanaishi kwenye vibanda au Gadafi hataki kuachia wenzie nafasi ya uongozi ndio sababu ya walibya kuona bora waingize nchi kwenye vita?
 
Usiwaamini wazungu na propaganda zao. Kipimo halisi cha kiongozi bora wa bara hili ni kutokubalika na mataifu ya kibeberu
 
Gaddaffi alipata anachostahili!! Nchi ile kwanza ilijaa ukabila,yaani kama wewe siyo bedui ambalo ndo kabila lake sahau kuhusu keki ya taifa!! Mwisho kabisa akajifanya kama Mungu wa Libya!! yaani yeye ndo ana akili kuliko wote!!

Kama ambavyo yeye mwenyewe aliingia kwa mpindua aliyekuwepo tena kwa vita,na yeye alitoka hivo hivo kwa pinduliwa kwa vita!! Njia aliyotumia kuingia ndo njia aliyotumia kutoka!!

Hii inamaanisha Gddafi alishindwa kusahihisha makosa ya mtangulizi wake!!

Kumbuka viongozi wengi wa Africa wanaficha maovu yao kwenye kichaka cha "maendeleo"
 
Back
Top Bottom