Ripoti: China inafanya mazoezi ya kushambulia vituo vya Marekani na washirika

S V Surovikin

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
13,590
32,672
Kuna uwezekano kuwa jeshi la China linafanya mazoezi
ya kushambuia vituo vya Marekani na vya washirika
huko Pacific, kwa mujibu kwa makao makuu ya ulinzi
ya Marekani.
Ripoti ya kila mwaka kwa Congress inasema kuwa
China inaongeza uwezo wake wa kupeleka ndege za
kivita kwenye visiwa vyake vya baharini.
Manowari ya Marekani yapita karibu na visiwa vya
Uchina
Ripoti hiyo inazungumzia kuongezeka uwezo wa
kijeshi wa China ikiwemo bajeti kubwa ya dola bilioni
190, thuluthi ya ile ya Marekani.
China bado hijazungumzia ripoti hiyo.
Ni mambo pia yako kwenye ripoti hiyo?
Onyo kuhusu mashambulizi ya angani ni moja ya
malengo ya kijeshi na kiuchumi ya China.
"Kwa miaka mitatua iliyopita PLA [People's Liberation
Army] limepanua maeneo yake ya kufanyia mazoezi
bahrini, na kupata ujuzi wa maeneo muhimu ya
baharini na kuna uwezekazo kuwa linafanya mazoezi
kushambulia vituo vya Marekani na vya washirika,"
ripoti hiyo ilisema.
Marekani yaionya China kuhusu visiwa bandia
baharini
Inaendelea kusema kuwa haijulikani ni kipi China
inataka kudhibitisha kwa kufanya mazoezi kama hayo.
"PLA huenda linataka kuonyesha kuwa lina uwezo wa
kushambulia Marekani na vikosi washirika kwenye
kambi za jeshi magharibi mwa bahari ya Pacific
ikiwemo Guam," ripoti hiyo iliongeza.
Ripoti hiyo inasema kuwa China inapanga vikosi
vyake "kupigana na kushinda".
"Lengo na mabadiliko haya ni kubuni kikosi hatari
kinachozunguka ambacho kitakuwa nguzu ya
oparesheni zake," kwa mujibu wa ripiti hiyo.
Marekani: China 'inawatishia majirani zake'
Bajeti ya jeshi la China inatarajiwa kuingezeka hadi
dola bilioni 240 katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Maeneo yenye misuko suko ni yapi?
Marekani ina wasi wasi kuhusu kuendelea kukua kwa
China huko Pacific ambapo Marekani bado ina
ushawishi mkubwa.
China yazindua manowari mpya ya kijeshi
Kati maeneo ambapo mvutano upo ni kusini mwa
bahari ya China ambalo ni eneo linalodaiwa na China
na nchi zingine.
Jeshi la Marekani mra nyingi hujaribi kuonyesha
kuwepo uhuru kwa kutumia eneo hilo kwa kupitisha
ndege zake kusini mwa bahari ya China.
China imekuwa ikapanua kile kinachoonekana kuwa
vituo vya kijeshi kwenye visiwa eneo hilo, na imepeleka
ndege zake huko wakati ikifanya mazoezi.
Eneo lingine ni Taiwan, ambalo linatajwa na China
kama mkoa wake uliojitenga.
Taiwan kuunda manowari zake kujilinda dhidi ya
Uchina
Ndege za China zazuia ndege ya Marekani
Ripoti hii inaonya kuwa China huenda inapanga
mikakati ya kuichukua kwa nguvu Taiwan.
Marekani ilikataa uhusiano wake na Taiwan mwaka
1979 lakini inadumisha ule wa kisiasa na kiusalama
hatua ambayo ineighadhabisha China.
Marekani pia inaendelea kudumisha uhusiano wake
mkubwa wa kijeshi na Japan ambayo ina tofauti zake
na China na pia Ufilipino.
Misukosuko isiyokuwa ya kijeshi inaendelea, China na
Marekani zimetangaza ushuru kwa bidha za mwingine.
 
hahaaa mwisho wa enzi" kama nawaona vile " Russia .iran " uturuki" N.corea wanavyo nyapia nyapia""... USA apigwe tu" tumechoka kuona akizidi kuwaamulia wenzie namna ya kuishi"...
 
Tatizo ni hawa wanaomzunguka na kumshauri Trump nawaza kama kuna miscalculation wanaweza ifanya kuhusu Maeneo ya Pacific na Middle East
Mkuu nakwambia hakuna mwenye uwezo wa kuanzisha ujinga kule.
Kama vita itaanza kule Pasifiki inamaanisha mataifa matatu makubwa kiuchumi duniani ndiyo yatakuwa vitani (Marekan, Uchina na Japani). Hivi unadhani Trump na Xi hawalijui hili ???? (Hakuna anayetaka vita)


Vita inaweza ikatokea lakini siyo kwa Uchina kuivamia Marekani au Marekani kuivamia Uchina.
Historia inatufundisha vita zote za dunia huwa hazianzi na taifa moja kubwa kuvamia taifa jingine kubwa.
Ila utakuta vijisababu vya kijinga-jinga tu: Mara Archduke kauwawa huko Serbia mwaka 1914 au Mara Hitler kavamia Poland.
 
China ina watu karibia bilioni moja na laki mbili, hawaitegemei Marekani kufanya biashara. Wana simu zao, magari yao na kila kitu chao. Marekani na watu wake million 300 asipofanya biashara na mchina inakula kwake.
Sio billion 1 na laki mbili mkuu.

Ni billion 1 na millions 200+
 
China has never been in war in modern world
Vietnam war
Sino-vietnam war
Sino-indian war
Korean civil war
Huelewi ukisemacho
It should be ' sijui nikiandikacho'. But it's a proven fact, only thing the US can do to China is tariffs, imposing sanctions on China will only hurt America and being the world economy power house America know this that's why it never happened as China is the world's largest consumer. Have you ever heard of sanctions against China? Just FYI China introduced new tariffs on American products ( not even Russia could do this). Fanya usome mjomba usije kichwa kichwa utakula za uso.
 
Kwa hali kama hiii mchina bado sana kwa mzungu anatakiwa atumie akili na muda wa miaka kama 1,000 kumfika mzungu wa USA, sio kwa aibu hiii.
Wazungu wa USA wapo mbali sana ktk mambo mengi mpaka wazungu wa Europe wanawashangaaa sio kwa uwezo ule na ndio Maana Trump akizisema baadhi ya nchi zinanyamaza, Maana haziitaji kubishana wakati zinaelewa project za USA sio za mchezo mchezo. Mfano Germany alivyoambiwa kuhusu kuchangia ktk NATO amekaa kimiya, anaelewa ulinzi anaolindwa na USA. Lakini China ndio ivyo wakati mwingine akubali kwamba kapitwa na USA.
We would want to make America Great Again
 
Back
Top Bottom