Ripoti binafsi: Machi 2022 ajali za barabarani zimeua watu 56, Serikali chukueni hatua

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,306
5,452
Leo ni Machi 30, 2022, imesalia siku moja tu kabla ya mwezi huu kufikia tamati, kwa ufupi unaweza kusema huu ni mwezi wa ajali, hiyo ni kutokana na matukio mengi kutoka mikoa tofauti.

Matukio mengi ya ajali yametokea na kusababisha vifo, ulemavu na wengine kujeruhiwa hasa yakihusisha magari na mengine pikipiki.

Nafikiri Serikali ina kitu cha kufanya katika hili, asilimia kubwa ya matukio yaliyotokea ama ni uzembe wa madereva au vyombo vyenyewe vya moto, ni machache yameripotiwa kuhusu miundombinu.

Hiyo inaonyesha wazi kuwa suala la miundombinu halijawa kisingizio ndiyo maana mamlaka husika zimekuwa kimya na kuishia kusema ‘madereva kuwa makini’, hivyo tu.

Unaweza kuniulizia wangefanya nini cha ziada, lakini ukweli ambao naamini Watanzania wengi wanaujua, matrafiki wengi au watu wa usalama wengi wao wapo barabarani kwa ajili ya kutafuta makosa madogomadogo kwa maderva na magari na wengine kuangalia maslahi yao binafsi kuliko usalama.

Mfano mwepesi ni Dar es Salaam, asilimia kubwa ya hao trafiki wanasimamisha magari pasipokuwa na sababu za msingi, ‘WANAONANA’ na dereva au Konda kisha maisha yanaendelea.

Kuna wale ambao unaweza kukuta sehemu kuna foleni au msongamano wa hovyo wa magari, badala ya kutafuta ‘solution’ wao wanakimbilia kuangalia wanaochepuka ili wawaminye wapozwe.

Ndiyo ukweli huo, inasikitisha sana, Rais Samia Hassan Suluhu, najua ajali haina kinga, lakini una kitu cha kuangalia katika idara ya usalama barabarani, ukianza na mamlaka ngazi ya juu, nao watashuka tu hadi chini huku ambapo ndipo kuna ‘uozo mwingi.

Tuangalie takwimu za ajali za magari na bodaboda zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari mwezi huu wa Machi 2022, kumbuka kuwa kuna nyingine nyingi tu zinazotokea mitaani hazijaripotiwa.

Hadi kufikia leo hizo zilizoripotiwa watu 56 wamepoteza maisha kwa ajali, ikiwa na maana kuna watu wengi zaidi wamepoteza maisha kwa ajali na hakuna hatua au tamko la nguvu kuhusu mfululizo wa ajali hizi.

Najua walisoma ripoti kama hii wanachoweza kuamua ni kufanya ni kuwa wakali barabarani kwa mihemko, kisha baada ya muda hazina faida wanaacha biashara inarudi kama kawaida

Machi 16, 2022 (Watu 4)
Watu wanne walifariki dunia na wengine 37 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga ikihusisha magari mawili.

Ilihusisha mabasi madogo ya abiria Toyoya Coast na Toyota Hiace pamoja na watembea kwa miguu.

Machi 18, 2022 (Watu 23)
Maeneo ya Malela Kibaoni Wilayani Mvomero, Morogoro kulitokea ajali ya basi la abiria na lori la mizigo na kusababisha watu 23 kupoteza maisha.

Lori lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) liligongana uso kwa uso na basi la Kampuni ya Ahmeed.

Machi 20, 2022 (Watu 2)
Gari la abiria aina ya Toyota Coaster ilipata ajali na kusababisha vifo vya watu wawili katika eneo la Oilcom, Nanenane Mkoani Morogoro.

Machi 24, 2022 (Watu 2)
Wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari Kivesa Wilayani Handeni Mkoani Tanga walifariki baada ya pikipiki iliyokuwa ikiwapeleka shule kugongana na nyingine, kisha wenyewe kugongwa na lori aina ya Fuso.

Machi 26, 2022 (Watu 5)
Watano walifariki kwa ajali Bunju B walipokuwa wakitoka kwenye starehe. Inadaiwa walikuwa wamelewa na wakati wanaingia barabara kubwa ya Bagamoyo Road, Lori la mchanga likawagonga, walikuwa watu sita, mmoja akawa majeruhi.

Machi 27, 2022 (Watu 7)
Eneo la Kidulya Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu gari aina ya Scania liligonga Bajaji katika Barabara ya Bariadi-Maswa na kusababisha vifo vya watu saba na wengine wanane wakijeruhiwa.

Machi 27, 2022 (Watu 5)
Watu watano walifariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa Mkoani Mbeya baada ya Lori la mizigo kufeli breki kwenye mteremko wa Mlima Mbalizi na kuyagonga magari madogo matatu, Bajaji na watembea kwa mguu.

Machi 28, 2022 (Watu 2)
Profesa wa Uchumi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Honest Ngowi pamoja na dereva wake, Innocent Mringi walipoteza maisha kwa kuangukiwa na kontena maeneo ya Mlandizi, Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.

Lori hilo lenye trela lililokuwa likitokea Nchini DRC kwenda Dar es Salaam lilihama upande wake wa barabara na kugonga gari lingine aina ya Noah upande wa pili, kisha kontena kuchomoka na kuangukia gari aina ya Toyota Land Cruizer lililokuwa limembeba Profesa Ngowi.

Machi 28, 2022 (Watu 6)
Watu sita walifariki na wengine kujeruhiwa baada gari aina ya Fuso walilokuwa wakisafiria kutumbukia korongoni eneo la Nyasa (Soni) - Mombo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga. Gari hilo lilikuwa limebeba bidhaa za sokoni kutokea Lushoto kwenda Wilayani Handeni.
 
Viongozi wa jeshi la polisi wameishiwa mbinu, hivyo usitegemee kitu kipya! Yaani mbinu zile zile zilete matokeo tofauti haiwezekani!!eti unawachukua madreva unawapeleka hospital kuwaonyesha majeruhi wa ajari ili waogope!

Hapo cha kufanya mama apangue jeshi zima aweke sura mpya, hao ma RPC, toka miaka na miaka ni kuhamishwa toka hapa nenda pale basi! Yaani RPC apimwe kwa kuangalia, hali ya uharifu mkoani kwake, na kiwango cha ajari za barabarani. Ikishindikana kabisa potelea mbali weka WANAJESHI ndio wasimamie usalama barabarani.
 
Hakuna dereva anayependa apate ajali bali ajali huja pasip kutgmea ama kw uzembe unaotkea njiani au mipango mingne y nguvu za kiroho.
 
Leo ni Machi 30, 2022, imesalia siku moja tu kabla ya mwezi huu kufikia tamati, kwa ufupi unaweza kusema huu ni mwezi wa ajali, hiyo ni kutokana na matukio mengi kutoka mikoa tofauti.

Matukio mengi ya ajali yametokea na kusababisha vifo, ulemavu na wengine kujeruhiwa hasa yakihusisha magari na mengine pikipiki.

Nafikiri Serikali ina kitu cha kufanya katika hili, asilimia kubwa ya matukio yaliyotokea ama ni uzembe wa madereva au vyombo vyenyewe vya moto, ni machache yameripotiwa kuhusu miundombinu.

Hiyo inaonyesha wazi kuwa suala la miundombinu halijawa kisingizio ndiyo maana mamlaka husika zimekuwa kimya na kuishia kusema ‘madereva kuwa makini’, hivyo tu.

Unaweza kuniulizia wangefanya nini cha ziada, lakini ukweli ambao naamini Watanzania wengi wanaujua, matrafiki wengi au watu wa usalama wengi wao wapo barabarani kwa ajili ya kutafuta makosa madogomadogo kwa maderva na magari na wengine kuangalia maslahi yao binafsi kuliko usalama.

Mfano mwepesi ni Dar es Salaam, asilimia kubwa ya hao trafiki wanasimamisha magari pasipokuwa na sababu za msingi, ‘WANAONANA’ na dereva au Konda kisha maisha yanaendelea.

Kuna wale ambao unaweza kukuta sehemu kuna foleni au msongamano wa hovyo wa magari, badala ya kutafuta ‘solution’ wao wanakimbilia kuangalia wanaochepuka ili wawaminye wapozwe.

Ndiyo ukweli huo, inasikitisha sana, Rais Samia Hassan Suluhu, najua ajali haina kinga, lakini una kitu cha kuangalia katika idara ya usalama barabarani, ukianza na mamlaka ngazi ya juu, nao watashuka tu hadi chini huku ambapo ndipo kuna ‘uozo mwingi.

Tuangalie takwimu za ajali za magari na bodaboda zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari mwezi huu wa Machi 2022, kumbuka kuwa kuna nyingine nyingi tu zinazotokea mitaani hazijaripotiwa.

Hadi kufikia leo hizo zilizoripotiwa watu 56 wamepoteza maisha kwa ajali, ikiwa na maana kuna watu wengi zaidi wamepoteza maisha kwa ajali na hakuna hatua au tamko la nguvu kuhusu mfululizo wa ajali hizi.

Najua walisoma ripoti kama hii wanachoweza kuamua ni kufanya ni kuwa wakali barabarani kwa mihemko, kisha baada ya muda hazina faida wanaacha biashara inarudi kama kawaida

Machi 16, 2022 (Watu 4)
Watu wanne walifariki dunia na wengine 37 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga ikihusisha magari mawili.

Ilihusisha mabasi madogo ya abiria Toyoya Coast na Toyota Hiace pamoja na watembea kwa miguu.

Machi 18, 2022 (Watu 23)
Maeneo ya Malela Kibaoni Wilayani Mvomero, Morogoro kulitokea ajali ya basi la abiria na lori la mizigo na kusababisha watu 23 kupoteza maisha.

Lori lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) liligongana uso kwa uso na basi la Kampuni ya Ahmeed.

Machi 20, 2022 (Watu 2)
Gari la abiria aina ya Toyota Coaster ilipata ajali na kusababisha vifo vya watu wawili katika eneo la Oilcom, Nanenane Mkoani Morogoro.

Machi 24, 2022 (Watu 2)
Wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari Kivesa Wilayani Handeni Mkoani Tanga walifariki baada ya pikipiki iliyokuwa ikiwapeleka shule kugongana na nyingine, kisha wenyewe kugongwa na lori aina ya Fuso.

Machi 26, 2022 (Watu 5)
Watano walifariki kwa ajali Bunju B walipokuwa wakitoka kwenye starehe. Inadaiwa walikuwa wamelewa na wakati wanaingia barabara kubwa ya Bagamoyo Road, Lori la mchanga likawagonga, walikuwa watu sita, mmoja akawa majeruhi.

Machi 27, 2022 (Watu 7)
Eneo la Kidulya Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu gari aina ya Scania liligonga Bajaji katika Barabara ya Bariadi-Maswa na kusababisha vifo vya watu saba na wengine wanane wakijeruhiwa.

Machi 27, 2022 (Watu 5)
Watu watano walifariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa Mkoani Mbeya baada ya Lori la mizigo kufeli breki kwenye mteremko wa Mlima Mbalizi na kuyagonga magari madogo matatu, Bajaji na watembea kwa mguu.

Machi 28, 2022 (Watu 2)
Profesa wa Uchumi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Honest Ngowi pamoja na dereva wake, Innocent Mringi walipoteza maisha kwa kuangukiwa na kontena maeneo ya Mlandizi, Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.

Lori hilo lenye trela lililokuwa likitokea Nchini DRC kwenda Dar es Salaam lilihama upande wake wa barabara na kugonga gari lingine aina ya Noah upande wa pili, kisha kontena kuchomoka na kuangukia gari aina ya Toyota Land Cruizer lililokuwa limembeba Profesa Ngowi.

Machi 28, 2022 (Watu 6)
Watu sita walifariki na wengine kujeruhiwa baada gari aina ya Fuso walilokuwa wakisafiria kutumbukia korongoni eneo la Nyasa (Soni) - Mombo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga. Gari hilo lilikuwa limebeba bidhaa za sokoni kutokea Lushoto kwenda Wilayani Handeni.
Nitakuwa wa mwisho kuamini kama Rais Samia ataendelea na Urais baada ya 2025
 
Back
Top Bottom