Ripoti aliyoiwasilisha shahidi Cpl. Hafidh ilitakiwa kuwasilishwa na Ofisi ya DCI

Unamdanganya Nani na Kwa faida ya Nani? MPELELEZI Mkuu kwenye hii kesi ni Kingai na ameshatoa Investigational evidence mahakamani. Miongoni mwa aliyoulizwa ni kuhusiana na fingerprints na DNA na akasema hakuona haja wala umuhimu wa kuzichukua. Mpaka kesi kuanza kusikilizwa mashahidi na vielelezo vyote vya kesi vinajulikana maana vimeorodheshwa kwenye PH. Mahakama kuu si kama Kwa mjumbe Mkuu.
POLE- subiri watakapo kuja hao mashahidi halafu mawakili wenu wanaharakati waulize maswali
wakili- umebatizwa
shahidi- sijui
wakili- mheshimiwa jaji naomba swali langu lijibiwe
jaji- uliza tena swali lako
BURE KABISA
 
Ninadhani huna facts za kutosha kuhusu alama za vidole. Shahidi wa kwanza alishathibitisha hakikuchukuliwa kwa sababu hazikuwa muhimu!! Jamhuri haiwezi kuleta facts mpya katika hatua hii ya kesi la sivyo itaanza upya! Nadhani unajaribu kutetea jambo usilojua vizuri. Risasi tatu anazodaiwa kuwa nazo Adamoo ni kithibiti. Kinapaswa kuletwa mahakamani. Na kama ulifuatilia maswali ya utetezi, risasi zinazosemwa kutumiwa kupima silaha hazikuwa colour-coded sawa na ile moja iliyobaki!! Hili linaturudisha nyuma kabisa kwenye hati ya mashtaka iliyokuwa na mkanganyiko wa risasi 1 na 3!! Bado hatujasikia kete za madawa ya kulevya. Napo finger prints au blood test kuona kama ni zao au wanatumia haitakuwa muhimu??

Una nadharia za kijinga. Umiliki wa silaha sio rahisi kama unavodhani. Kama iliingia nchini kinyume na taratibu bado unadhani Polisi watajua mmiliki??

Mmezoea maneno ya polisi kutopingwa mahakamani na ndio maana waiba kuku wanafungwa miaka 3 na wezi wa mabilioni miaka miwili kwa “matumizi mabaya ya madaraka”
249480566_565194884480332_932754780607090557_n.jpg
 
POLE- subiri watakapo kuja hao mashahidi halafu mawakili wenu wanaharakati waulize maswali
wakili- umebatizwa
shahidi- sijui
wakili- mheshimiwa jaji naomba swali langu lijibiwe
jaji- uliza tena swali lako
BURE KABISA
Washamba wa hivi Ni mashahidi wa Jamhuri ,In short ni mawakala wa shetani.
 
Duh! Kwa hiyo, Shahidi kathibitisha hiyo Silaha ambayo inafanya Kazi Ni ya nani? Na Kathibitishaje ilhali tumesikia Risasi Ni tofauti na za Silaha yenyewe?
Ndiyo hapo nimekaa kwa kutulia naangalia mchezo....afu wamekamata risasi 3 akatumia 2 kutest kama ni nzima kaleta maganda ambayo hayaendani pia na silaha aliyosema
 
Hyo ni kweli yeye alitumwa tu kufanya kazi halafu atoe majibu Kwa wahusika ila pamoja na yote hata yeye kuna sehemu kama mtaalamu wa uchunguzi amezingua hata kama alipewa barua ya nini afanye ila kwake pia kuna maswahili yanabakia coz kwenye kesi kama hizi inatakiwa utoe fully data kama mtaalamu, Kwa ufupi tu tuache kufanya kazi kimazoea hasa kufuata maagizo ya watu na kuacha utaalamu wetu na miongozo yetu ya kazi inavyotaka
Utaalamu utoke wapi hapa wakati lengo ni kutengeneza sinema ya kesi?
Nchi hii watu wanaudhi sana unatamani papo hapo kizimbani umpige shahidi rungu la kichwa.
 
POLE- subiri watakapo kuja hao mashahidi halafu mawakili wenu wanaharakati waulize maswali
wakili- umebatizwa
shahidi- sijui
wakili- mheshimiwa jaji naomba swali langu lijibiwe
jaji- uliza tena swali lako
BURE KABISA
Comte inabidi ukajisajili kama wakili was nyoongeza upande wa mashitaka ili uhakikishe hasimu wenu anafungwa🏃.
 
Kumbe waliipima silaha ya JWTZ kuona Kama inafanya kazi au haifanyi kazi.
Halafu huyu Shahidi ametupa Jambo jingine leo kama mtuhumiwa alikuwa na kidhibiti amekamatwa nacho labda machungwa mawili ili kujua kweli yalikuwa machungwa mchunguzi au mpelelezi unakula chungwa moja au yote Kisha unasema ni kweli mtuhumiwa alikamatwa na machungwa mawili ila niliyala wakati wa kuchunguza.
Mi nikaona ni kama amesema alikamata machungwa matatu amekula mawili wakati wa uchunguzi na akaja na maganda ya machenza🤔🤔
 
Comte inabidi ukajisajili kama wakili was nyoongeza upande wa mashitaka ili uhakikishe hasimu wenu anafungwa🏃.
Vessel nilifikiri hapa tunajadliana na kubadilishana maoni kumbe wew mwenzangu unatafuta ajira? Mie nina ajira yangu na kazi za kutosha siuhitaji huo uwakili
 
Ninadhani huna facts za kutosha kuhusu alama za vidole. Shahidi wa kwanza alishathibitisha hakikuchukuliwa kwa sababu hazikuwa muhimu!! Jamhuri haiwezi kuleta facts mpya katika hatua hii ya kesi la sivyo itaanza upya! Nadhani unajaribu kutetea jambo usilojua vizuri. Risasi tatu anazodaiwa kuwa nazo Adamoo ni kithibiti. Kinapaswa kuletwa mahakamani. Na kama ulifuatilia maswali ya utetezi, risasi zinazosemwa kutumiwa kupima silaha hazikuwa colour-coded sawa na ile moja iliyobaki!! Hili linaturudisha nyuma kabisa kwenye hati ya mashtaka iliyokuwa na mkanganyiko wa risasi 1 na 3!! Bado hatujasikia kete za madawa ya kulevya. Napo finger prints au blood test kuona kama ni zao au wanatumia haitakuwa muhimu??

Una nadharia za kijinga. Umiliki wa silaha sio rahisi kama unavodhani. Kama iliingia nchini kinyume na taratibu bado unadhani Polisi watajua mmiliki??

Mmezoea maneno ya polisi kutopingwa mahakamani na ndio maana waiba kuku wanafungwa miaka 3 na wezi wa mabilioni miaka miwili kwa “matumizi mabaya ya madaraka”
Ukweli kwenye hili Kingai alitegwa na akakubali mtego kwamb hawakuchukua alama za vidole.

Itakumbukwa kwamba Adamoo alidai kuwa hiyo pistol siyo yake maana yake hakuishika na kwahiyo vidole vyake haviwezi kuwa kwenye hiyo pistol.

Pia ukifuatilia ushahidi wa Kingai alitaja jina la Pistol ambalo ni tofauti na report ya Hafidh. Kama utakumbuka Kibatala alipompa Hafidh pistol na kumtaka asome jina kwenye kitako ambacho kilikuwa na lebel Luger which you can't miss it ukiwa mpelelezi.

Na pia Hafidh kuna sehemu katika kuhojiwa kwake alijibu kwa kumtaja Adamoo
 
Hivi
Mtu wa kuwa link yupo- lakini kwa ujuaji wa mawakili wa utetezi walitumia nguvu nyingi kwa jambo dogo.
Shahidi namba 3 kilichomuleta ni kuthibitisha uzima wa silaha basi na alifanya hivyo.
Nafikiri atakuja shahidi atakae unganisha hiyo silaha na ADAMOO- kumbuka mpaka sasa hivi upande wa mashitaka haujagusa alama za vidole.
Atakauja shahidi mwingine wa kuonyesha umiliki wa hiyo silaha- hapo patamu.
Hivi unaelewa ulichoandika? Hiyo Silaha ilitakiwa ifanyiwa Finger Print ili kubaini mmiliki wa hiyo Silaha Kama kweli ni Adamoo. Uchunguzi wa Finger Print haukufanyika. Sasa huyo unayesema atakuja kuilink hiyo Silaha na Adamoo atatumia njia gani ?
 
Sijui ni kutokuelewa protocols ama ndio business as usual? Ripoti ya uchunguzi wa silaha ilipaswa kuwasilishwa na walioomba uchunguzi huo, sio na aliyechunguza. Mchunguzi kwanza hata alikuwa hana haja, na kama angehitajika basi yeye alipaswa kuleta uthibitisho wa barua ya maombi kutoka ofisi ya DCI.

Ofisi ya DCI ndiyo ilipaswa kuja na hii ripoti kama backup ya kuthibitisha kwamba hawa watuhumiwa walikuwa wanapanga kuwadhuru viongozi kwa hiyo silaha ambayo sasa imethibitishwa kuwa inafanya kazi.

Ndio maana huyu shaidi wa jana alishindwa kuwalink watuhumiwa na uchunguzi wake sababu ripoti ya uchunguzi wake ilipaswa kuwasilishwa na walioomba huo uchunguzi.

Hakuwa hata shahidi, kwa hiyo mie nishachoka haya mambo
 
Mtu wa kuwa link yupo- lakini kwa ujuaji wa mawakili wa utetezi walitumia nguvu nyingi kwa jambo dogo.
Shahidi namba 3 kilichomuleta ni kuthibitisha uzima wa silaha basi na alifanya hivyo.
Nafikiri atakuja shahidi atakae unganisha hiyo silaha na ADAMOO- kumbuka mpaka sasa hivi upande wa mashitaka haujagusa alama za vidole.
Atakauja shahidi mwingine wa kuonyesha umiliki wa hiyo silaha- hapo patamu.
Mkuu naona unapulizia kinyesi pafyumu!
 
Then what? Mimi nikikamatwa na bastola ambayo sina umiliki nayo ndiyo kumaanisha nimekuwa gaidi ama nataka kumdhuru kiongozi?

Kwa nini usinishitaki kwa kosa la kumiliki silaha kinyume na sheria ambalo ni objective, then unanishitaki kwa kosa la kutaka kudhuru ambalo ni subjective?
Huo ni one piece of evidence, kwamba silaha ilikuwa nzima.

Hukumu hutolewa kwa kuangalia udhahidi wote uliowasilishwa
 
Sijui ni kutokuelewa protocols ama ndio business as usual? Ripoti ya uchunguzi wa silaha ilipaswa kuwasilishwa na walioomba uchunguzi huo, sio na aliyechunguza. Mchunguzi kwanza hata alikuwa hana haja, na kama angehitajika basi yeye alipaswa kuleta uthibitisho wa barua ya maombi kutoka ofisi ya DCI.

Ofisi ya DCI ndiyo ilipaswa kuja na hii ripoti kama backup ya kuthibitisha kwamba hawa watuhumiwa walikuwa wanapanga kuwadhuru viongozi kwa hiyo silaha ambayo sasa imethibitishwa kuwa inafanya kazi.

Ndio maana huyu shaidi wa jana alishindwa kuwalink watuhumiwa na uchunguzi wake sababu ripoti ya uchunguzi wake ilipaswa kuwasilishwa na walioomba huo uchunguzi.
Jiongezee maarifa juu ya uwasilishaji wa ripoti za kitaalamu za uchunguzi
 
Hivi

Hivi unaelewa ulichoandika? Hiyo Silaha ilitakiwa ifanyiwa Finger Print ili kubaini mmiliki wa hiyo Silaha Kama kweli ni Adamoo. Uchunguzi wa Finger Print haukufanyika. Sasa huyo unayesema atakuja kuilink hiyo Silaha na Adamoo atatumia njia gani ?
Jamaa hajui kitu chochote kuhusu vidhibiti. Vitu walivyokutwa navyo washitakiwa vinapaswa kufikishwa mahakamani kama ushahidi na ushahidi usio na shaka. Finger prints zilikuwa muhimu sana kuchukuliwa!! Tests za kinachosemwa bila aibu kuwa ni madawa vilipaswa kufanyiwa vipimo na chombo chenye mamlaka. Matokeo yake wanasema walitumia risasi ambazo ni kidhibiti kupima kama silaha inafanya kazi. Ndio kusema maabara ya upimaji haina risasi za kupimia silaha? Je kama mshitakiwa angekamatwa bila risasi hata moja, uzima wa silaha hiyo usingepimwa kwa namna nyingine yoyote?? Hii fact itawasumbua kama hakimu atakuwa fair!! Hata kama walikuwa na madawa, je inaonesha walishika madawa hayo, je ni watumiaji? Kama si watumiaji lakini ni wauzaji - kuna namna wameonesha kwenye simu zao zilizodukuliwa kama wanafanya biashara hiyo?? Makosa ya tofauti za taarifa kuhusu silaha yataleta shida, information pieces lazima ziwe complete. Na haziko complete!

Kesi hii inafumbua watu macho. Maneno ya polisi yametumika sana kuhukumu watu - inapokuja polisi kupambana na wanasheria, matokeo ya kesi nyingi yamekuwa polisi wasivotarajia. Unapoleta mashahidi ni lazima wote waondoe shaka katika shitaka. Mmoja tu akiweka shaka, basi kesi nzima inakuwa sio timilifu. Upande wa mashitaka umefanikiwa sana kuongeza shaka badala ya kuzipunguza!!
 
Nyaraka nyingi wanazokuja nazo hawa mashahidi zilipaswa kuletwa na ofisi ya DPP au DCI.

PERIOD!!!

Screenshot_20211112-144305.jpg
 
Back
Top Bottom