Rip | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rip

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by KakaJambazi, Oct 27, 2010.

 1. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Oct 31. RIP.jpg
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tunakwenda kuuzika Ufisadi usio na Utu wala Ubinadamu chini ya CCM ya KIKwete!

  Nitajieleza Na Nguvu ya umma ya utu iwe nami!:

  Utu ni taasisi pana! Taasisi ambayo ndio uti wa mgongo wa maendeleo ya mtu na jamii yake.

  Alikuwa JK Nyerere peke yake na sasa, Dr W Slaa ... aliyekuwa anadhubutu Kuusemea Utu na kuuweka kama kigezo cha ustawi wa Taifa!

  Bila Utu, ambao ndiyo asili ya Mtu, maendeleo yote hayana maana yoyote! Yanakuwa ni maendeleo ya vitu! Ni utu kwanza...uwe chimbuko la demokrasia na maendeleo ya Taifa.

  Utu ni Uungu ndani mtu, hatuwezi kuusaliti tukabaki salama kama watu... lazima utu kutangulia kila nyanja ya jamii bila hivyo hicho kinachoitwa ustawi, maendeleo na demokrasia vinakuwa havina maana.

  Maendeleo ya Utu ndio yatawale maendeleo na ustawi wa jamii na taifa, na si maendeleo ya vitu bila kuujali, kuujenga na kuuendeleza utu.

  Kitaalam: Utu unanyaushwa, kuharibiwa na kuangamizwa na UFISADI.

  Kiua Utu ni Ufisadi. Kauli mbiu ni Utu Kwanza na Si ufisadi Kwanza.

  Utu unarutubishwa na haki, upendo, maadili ya uongozi bora, kuheshimiana, haki na usawa wa pato la taifa, matumaini, ukweli, ujasiri na si ukatili, uimara wa kusimamia na kutetea sauti ya umma, utambuzi wa dhana nzima ya utu na kuwaongoza watu kuelekea kilele cha utu wao kama ukombozi wa mwandamu.

  Ni Kweli na hakika: CCM na Kikwete wameutupilia mabali Utu ulioasili ya Mtu na kukumbatia kwa kiwango cha kutisha cha Ufisadi. Nani mwenye utu kamili anabishia hili?

  Baada ya CCM na Kikwete kusaliti asili ya mtu, kinachofuatia nchini ni Mgawanyiko na Matabaka kwa Taifa. Mgawanyiko na mtabaka hayo vinazaa Udini, ukabila, kuimarisha, ujinga, dhuluma, maradhi nk. Kisa? Utu umewekwa kando, tumeutwika Ufisadi na sasa tumeisaliti asili yetu kama binaadamu. Na kama utu haupo ...ina maana tunatawaliwa na kinyume cha utu...ambacho ni unyama ndani ya Mtu, yaani ufisadi... Na usiombe kuishi ndani ya jamii au Taifa kama hilo! Nani haoni kiama kinachoweza kufuatia hapo?

  CCM na Kikwete wana Utu na misingi yake ya kujibu hoja hii? Labda kwanza wawafilisi Mafisadi Papa Kumi (Kumi na Moja) waliowekwa hadharani tayari… Vinginevyo wakati wa kuichai nchi ni sasa!

  Kwa kuwa CCM badala ya kupunguza maadui wa ustawi wa maendeleo ya jamii ya watanzania kutoka kuwa wa nne, sasa wanawajenga na kufikia sita. Yaani Ujinga, Maradhi, Umasikini, Ufisadi(Dhuluma), Ukabila na Udini.


  Tunahoji: CCM na Kikwete wanacha kujitetea kwenye hili? Mna Utu na Ubinaadamu wa kuhitaji kuliongoza kwa hekima, utulivu na amani Taifa hili kwa kipindi kingine cha miaka mitano?
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  n chadema wanazikwa jamaa ccm kavaa kijani jamaa
   
 4. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280

  We ushaona wapi vita iko iraki,, afu tanzania tunachimba mahandaki.

  Wafu wanaandaa makaburi yao.
   
 5. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  haaa haaaa chadema mwaka huu ndo mwisho wao
   
 6. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  mwaka 2005, ulikuwa mwisho wa CUF, leo mnafunga ndoa nao (serikali ya Mseto).

  2010 Mwisho wa chadema, Jk anamepaniki anatukana hadharni watu ni majuha.kama wewe ni kocha, Ukiona mcheji mzuri kanza kucheza rafu, anza kutafuata mbadala maana kaisha huyo.
   
 7. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280

  Hata miaka ya myuma ilitabiriwa hivyo, lakini ikawa kinyume.
   
Loading...