RIO & RC (Arusha) - Aidha hamkula KIAPO ama mmeamua KUMDHALILISHA Rais!

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Aug 29, 2011
412
90
Kwenu Mulongo & Namomba;

Hili liko wazi kabisa kwa kuzingatia ile Sheria No. 8 ya 1962 {CAP.266} kwa watumishi wa umma wa kada yenu kwamba kiapo ni kitu cha kwanza kabla utumishi wenu haujaanza kwa nafasi ambayo mnakwenda kuitumikia. Kifungu cha 12 cha Sheria hiyo (Oath of Secrecy) ndicho kilichonigusa sana manake Mulongo kifungu hicho unawajibika kwacho.

Nimeshtushwa na majibu ya Mulongo kwenye vyombo vya habari jana kwamba ati yeye si muhifadhi nyaraka ilihali kwa nafasi aliyonayo yeye (kama Mwakilishi wa Raisi na Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa Mkoa) anapaswa kuwa Muhifadhi Mkuu wa Kwanza wa Nyaraka za Serikali na uzembe huo usimfanye ajitoe katika hili. Hakika hatutashangazwa keshokutwa kusikia Raisi kadhuriwa akiwa katika himaya ya Mulongo kwa uzembe wa namna hii. Mwlaimu angekuwepo Mulongo na Namomba leo sijui mgekuwa wapi. Nyaraka kugongwa neno SIRI kwa maana ya kawaida ni kumfikia mlengwa hasa kinyume na hapo itakuwa si aibu kwa mtumaji au mtumiwaji bali kwa Serikali nzima.

Katika hili ama wahusika wamechoshwa na aliye watuma ama makundi yamewafanya kumdhalilisha aliyewatuma ama kwao kiapo hakina tija.......
 
Unachemsha!

Back
Top Bottom