Rihanna Ataka Hukumu ya Kutowasiliana na Chris Brown Ifutwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rihanna Ataka Hukumu ya Kutowasiliana na Chris Brown Ifutwe

Discussion in 'Celebrities Forum' started by MziziMkavu, Sep 12, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Mwanamuziki wa Marekani, Rihanna aliyetamba sana na wimbo wake "Umbrella" ameripotiwa kuwa ana hasira na amehuzunishwa sana na uamuzi wa mahakama kumuamuru mpenzi wake wa zamani Chris Brown akae nae mbali na wala asijaribu kuwasiliana naye.

  Chris Brown alihukumiwa jumanne iliyopita kutumikia kifungo cha nje cha miaka mitano kufuatia tukio la mwezi februari mwaka huu ambapo Chris Brown alimshushia kipigo cha nguvu Rihanna na kuiharibu sura yake.

  Chris Brown mwenye umri wa miaka 20, alihukumiwa pia kufanya kazi ngumu za kuitumikia jamii kama vile kufagia barabara na kukata nyasi katika jimbo la Virginia.

  Mbali na adhabu hizo, Chris Brown aliamriwa asijaribu kuwasiliana na Rihanna kwa simu wala kwa kumtumia mtu mwingine katika kipindi chote cha kifungo chake cha nje cha miaka mitano.

  Alitakiwa pia asimsogelee Rihanna kwa umbali usiopungua mita 90 lakini kama wote watakutana kwenye shughuli za muziki basi wanatakiwa wasikaribiane kwa umbali usiopungua mita 9.

  Hata hivyo, kwa mujibu wa vyombo vya habari, Rihanna amekuwa katika jitihada za kuitaka mahakama ifute uamuzi wake wa kumkataza Chris Brown kumsogelea au kuwasiliana naye.

  "Wakati Rihanna alipoambiwa na mwanasheria wake kuwa jaji amekataa kufuta uamuzi huo, alionekana mwenye huzuni sana" alisema mdau mmoja wa karibu wa Rihanna akiongea na jarida moja la Uingereza.

  "Alianza kuwapigia simu rafiki zake na kusema ni uamuzi gani wa kipuuzi umechukuliwa, Chris hawezi kumpiga na kumjeruhi kwa mara nyingine, Rihanna alionekana ni mwenye hasira sana".

  http://www.nifahamishe.com/entertainment.aspx?NewsID=3004790
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu huyu hakimu hataki hawa vijana wawe pamoja tena na sijui kama imeshatolewa hukumu ndefu kama hii kwa wapendanao ambao bado wanataka kuendeleza penzi leo. Pamoja na yaliyotokea wote bado wanapendana lakini kuwatenganisha kwa miaka mitano ni kipindi kikubwa mno ambacho sijui kama wote wataweza kukivumilia.

  Je, uamuzi huu wa mahakama uko applicable hata nje ya Marekani au ni Marekani tu (kwa mfano wote waamue kuhamia nchi nyingine mpaka baada ya miaka mitano) ? Je, Riri akiamua 'kumtembelea' Chris nyumbani kwake (US) je, anaweza kuadhibiwa na mahakama?
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ndio maana wapenzi au hata spouses kabla ya kupelekana mahakamani inabidi kufikiria sana unataka nini sasa na hata kesho.Unaweza ukawa leo una hasira sana ukataka dola ikusaidie..ujue dola haitakusaidia nusunusu.Kwa hili la Rihanna na Chris - wakiamua kuhamia nchi nyingine sioni ni vipi hukumu hiyo itafanyika.Systems zinaweza kuwa tofauti kabisa.Ndio tuelewe tunapoona wapendanao wenye kufanyiana ubaya wa kila aina hawapelekeni mahamani ni kukwepa situatioins kama hizi.
   
 4. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Haka kasichana nahisi kana asili ya ule mkoa Bongo ambao wanawake wasipopigwa na waume zao wanaona kama vile hawapendwi.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160

  Binadamu mara nyingi tunafanya matendo ya kinyama tunapokuwa na hasira, na bahati mbaya zaidi huwa hatukubali kuishi na consenquences simply because we forget easily. Kama Rihanna angeulizwa that Chris afanyiwe nini, si ajabu angesema anyongwe kabisaa...

  I just feel sorry for the two, but once you blow the whistle, be ready for whatever!!!

  sipendi domestic violence, lakini pia sipendi ku-publicize matatizo ndani ya mapenzi, kwani mara nyingi huzaa negatives kuliko positives
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  KKN ulikuwa wapi siku zote hizi? Nafurahi kukuona tena jamvini. Kupenda kubaya jamani kabinti bado kanampenda sana Chris ndiyo maana sasa kanakuwa kama kamechanganyikiwa, lakini hakimu naye kutoa hukumu ndefu kiasi hicho ni kama kuwakomoa vijana hawa. Tuone kama wataweza kuvumilia hiyo miaka mitano au kila mmoja atashika 50 zake na kibaya zaidi wote matendo yao hufuatiliwa sana na vyombo vya habari.
   
 7. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Nipo BAK, siku hizi nimeamua kuwa msomaji tu, tuna waleta habari wengi sana humu hadi ukiingia hujui usome thread gani na uache ipi but about 70% ni pumba tu, JF imepoteza utamu wake bana ndo maana siku hizi hainipagawishi kihiiiiiiiivyo. Mambo mengine?
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  KKN nilidhani niko pekee yangu mwenye dhana kama hiyo Mkuu, kumbe tuko wengi halafu ustaarabu uliokuwepo umetoweka kabisa kutukanana na kuleta mijadala inayojenga uhasama hasa ya kidini ndiyo kumepamba moto.

  Mambo mengine poa kabisa. TV leo ina mambo kibao nawaangalia MANU sasa hivi, baadaye nitamwaagalia Tiger Woods akifanya vitu vyake na jioni nitamwangalia Serena akimsimamisha former # 1 Kim Clijster from belgium katika semi final ya US Open, lakini baada ya mechi ya MANU nitatoka kidogo kwenda kufanya manunuzi. Haya Jumamosi njema Mkuu.
   
 9. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Sounds super mkuu, mi niko mzigo naugulia maumivu ya kichapo cha City, masaa yenyewe hayaendi, swaumu nayo inakaba kichizi. Enjoy your evening.
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Goli 4 ni nyingi mno du! Mzee ulipotea sana ama ni mambo ya kampeni 2010?
   
 11. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2009
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wana hela hawa kama wanataka kuonana wapande ndege waende Canada au Mexico.
   
 12. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Mi sio mwanasiasa Masa, boksi zimenikaba tu mkuu.
   
Loading...