Ridhwani aibukia Maswa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ridhwani aibukia Maswa!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nyambala, Oct 25, 2010.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Maswa hapakaliki, MGOMBEA WA CCM NAYE AMFUATA SHIBUDA LUPANGO Send to a friend Monday, 25 October 2010 07:20 0diggsdigg

  [​IMG]Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba

  Zulfa Mfinanga, Shinyanga na Frederick Katulanda, Mwanza
  HALI inaonekana kuwa tete kwenye Jimbo la Maswa Magharibi baada ya mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Robert Kisena kukamatwa na kuwekwa mahabusu, siku chache baada ya mgombea wa Chadema, John Shibuda kukamatwa kwa tuhuma za kuhusika kwenye vurugu zilizosababisha kifo cha dereva wa CCM.

  Shibuda, ambaye ameliongoza jimbo hilo kwa tiketi ya CCM kwa kipindi kirefu kabla ya kuhamia Chadema, alikamatwa wiki iliyopita baada ya wafuasi wa chama hicho kupambana na wenzao wa CCM karibu na eneo ambalo Chadema ilikuwa ikiendesha mkutano wake wa kampeni za ubunge, vurugu zilizosababisha Steven Kwilasa Masanja, 26, ambaye alikuwa akimuendesha Kisena, kupoteza maisha.

  Kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga, Daudi Siasi alithibitisha kukamatwa kwa mgombea ubunge huyo wa CCM, ambaye vyombo vya habari viliripoti kuwa siku ya vurugu hizo alikwenda kituo cha polisi na kumshambulia kamanda wa polisi wa wilaya na kumbwaga chini, akimtuhumu kuwa alimwachia huru Shibuda.

  Kukamatwa kwa Kisena kumekuja siku moja tangu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba 'kuweka kambi' wilayani Maswa mkoani Shiyanga kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo la kwanza la aina yake kwenye uchaguzi wa mwaka huu.

  Wakati Manumba akiwa wilayani Maswa kuratibu uchunguzi wa mauaji hayo, katibu mkuu wa CCM, Yusuph Makamba tayari ameshakaririwa na vyombo vya habari akidai kuwa chama chake kina ushahidi wa kimazingira kuwa mgombea huyo wa Chadema alihusika na mauaji hayo ya dereva wa mgombea wa CCM.

  Habari za kipolisi zinasema kuwa Kisena alitiwa nguvuni na polisi jana akihusishwa pia kwenye tukio hilo, lakini taarifa zaidi zinadai kuwa mgombea huyo wa CCM alikamatwa pia kwa tuhuma za kumshambulia kwa mateke kamanda wa polisi wa Wilaya ya Maswa (OCD), Peter Ndunguru.

  "Mgombea huyo (Kisena) ametiwa nguvuni kutokana na mzozo wake na OCD wa Maswa juzi kituoni hapo na kumpiga OCD," alisema Kamanda Siasi, ambaye mwishoni mwa wiki alikaririwa akisema kuwa suala la shambulizi hilo ni la OCD Ndunguru na si Jeshi la Polisi na kufafanua kuwa ofisa wake ndiye aliyetakiwa kuamua au kutoamua kumshtaki mgombea huyo kwa tuhuma hizo za kufanya jinai.

  Akizungumza kwa njia ya simu siku ya tukio, OCD Ndunguru alisema mgombea huyo wa CCM aliyeambatana na viongozi wa chama hicho walifikika polisi na kuuliza mahali alipo Shibuda, lakini kabla ya kujibiwa Kisena alimrukia OCD na kuanza kumshambulia kwa mateke kiasi cha kumuangusha chini.

  “Alinirukia na kunipiga,” alieleza OCD, lakini 'bosi' wake, ambaye ni Kamanda Siasi, akasema kuwa “Suala la Kisena na OCD ni jambo la kawaida kiutendaji na wala siwezi kulizungumzia... kwa sasa hapa ninashughulika na suala zito la mauaji".

  Taarifa zaidi zinasema tayari Jeshi la Polisi limeunda tume ya watu wanne kuchunguza vurugu hizo baina ya wafuasi wa Chadema na CCM ikiongozwa na DCI Manumba ambaye yupo Maswa kuchunguza chanzo cha vurugu hizo zilizosababisha Shibuda kuwekwa rumande hadi leo.

  Taarifa zinasema katika timu hiyo ya uchunguzi, Manumba ameongozana na mmoja wa maafisa waaandamizi wa upelelezi makao makuu ya polisi Dar es Salaam na watashirikiana na mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Shinyanga, Selemani Nyakipande, pamoja na maafisa Idara ya Usalama wa Taifa ambao hata hivyo hawajatajwa.

  Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu juzi, Manumba alisema kuwa amefika kwa ajili ya kusaidia safu ya uchunguzi ili kuhakikisha haki inatendeka na ukweli unabainika.

  “Ndiyo niko Maswa, lakini ndiyo tumeanza uchunguzi... naomba nipewe nafasi ya kufanya kazi; tukikamilisha uchunguzi wetu juu ya jambo hili tutawafahamisheni,” alieleza Manumba.

  Jana Manumba alisema ni mapema mno kuzungumzia tume hiyo na akakiri kuwa yeye ni mmoja wa wajumbe akiongeza kuwa Shibuda na wenzake bado wanashikiliwa na polisi.

  "Sijaunda tume kwa kuwa hata mimi mwenyewe ni mmoja wa watu walio kwenye tume hiyo ndiyo maana nikaja hapa, lakini siwezi kuzungumzia kwa sasa hadi tutakapomaliza kazi; lakini Shibuda bado yupo ndani," alisema Manumba.

  Shibuda pamoja na watuhumiwa wengine 12 alikamatwa Oktoba 21 majira ya saa 10:00 jioni wakituhumiwa kuhusika na tukio la mauaji ya dereva wa gari la mgombea ubunge wa CCM, Robert Simon Kisena katika Kijiji cha Kizungu.

  Taarifa zaidi zinasema kuwa marehemu Kwilasa aliyezaliwa mwaka 1984, amezikwa jana kijijini kwao Badabada, Kata ya Nyalikungu na mazishi yake yalihudhuriwa na mkuu wa mkoa Shinyanga, Dk Yohana Balele, mwenyekiti wa CCM mkoa huo, John Mgeja na katibu wake, mgombea ubunge, Teddy Kasela Bantu na
  Ridhwani Kikwete.

  Hata hivyo, taarifa zilizolifikia gazeti hili wakati tukienda mitamboni zinaeleza kuwa Kisena alionekana kwenye mazishi hayo ya aliyekuwa dereva wake huku polisi wakidai kumuachia huru kwa dhamana baada ya kuhojiwa.

  "Ameachiwa kwa dhamana. Tulimkamata; tukamhoji... dhamana ilikuwa wazi na ametimiza masharti," alisema mkuu wa upelelezi mkoa huo (RCO), Seleman Nyakipande.

  Hata hivyo, Mwananchi ilipotaka kujua sababu za mgombea huyo wa CCM kuachiwa huru mapema tofauti na Shibuda anayeendelea kushikiliwa, Nyakipande alisema "Kisena hawezi kuhusishwa na vurugu zilizotokea kwa sababu alikuwa mbali na tukio."

  Mwananchi ilipohoji kuwa mbona taarifa zinaonyesha kuwa hata Shibuda alikuwa mbali na tukio, RCO huyo alisema: "Tulimkamata Shibuda kwa ajili ya uchunguzi na tutamwachia hivi karibuni."

  Akiwa wilayani Maswa juzi, Makamba alisema: “Kwanza kabla ya yote Chadema walishatangaza kuwa ni lazima watamwaga damu na katika tukio hili kuna ushahidi wa kimazingira kuwa Shibuda anahusika na mauaji hayo... pia kuna ushahidi wa kimazingira kuwa wafuasi wa Chadema wanahusika na mauaji hayo.”

  Vurugu hizo zilitokea Oktoba 21 majira ya saa 10:00 alasiri kwenye eneo lililo mbali na uwanja ambao Shibuda alikuwa akihutubia kijijini Kizungu. Wafuasi wa Chadema waliokuwa wakitangaza kuwepo kwa mkutano huo wa Shibuda kwa kutumia gari la matangazo, walikutana na gari la wafuasi wa CCM wakati wakielekea kwenye mkutano wao na ndipo vurugu kubwa zilipozuka na hatimaye kusababisha kifo.

  Kamanda Siasi aliwaambia waandishi kuwa wafuasi wa CCM walipofika eneo hilo waliteremka kwa ajili ya kukojoa na baadaye gari la Chadema lilisimama na wafuasi hao wakaanza kushambuliana.

  Kamanda Siasi alisema kuwa mbali na kuuawa kwa dereva huyo, wafuasi wengine wanne wa CCM waliokuwa kwenye gari hilo aina ya Toyota Hilux Surf, walijeruhiwa katika mapambano hayo na kuwataja kuwa ni Msaada Mangulu mwenye umri wa miaka 33, Sita Mashara, 32, Alexernder Edward, 43, pamoja na William Simon, 32, ambaye ni mdogo wa mgombea huyo wa CCM na kwamba hali zao zinaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na kuruhusiwa kutoka Hospitali ya Wilaya ya Maswa.

  Kutokana na vurugu hizo, Shibuda ambaye alikuwa akiendelea na mkutano wake, alifuatwa na maofisa wa polisi na kuwekwa chini ya ulinzi na hadi jana alikuwa akiendelea kushikiliwa kwa mahojiano.

  Akizungumzia tukio hilo, Shibuda alisema alidai kuwa kushikiliwa kwake kunatokana na maagizo ya CCM kwa vile wanataka kutumia njia hiyo kummaliza kisiasa licha ya kuwa wanatambua kuwa wakati tukio hilo alikuwa jukwaa akiendelea na kampeni.

  Alisema kushikiliwa kwake kunaonyesha ni jinsi gani ambavyo jeshi hilo linatumiwa na CCM kumkandamiza kwa kuwa eneo alilokuwa akihutubia yeye lilikuwa mbali na eneo la tukio, lakini amepata taarifa kutoka kwa baadhi ya maofisa wa polisi kuwa wamepewa maelekezo na vigogo wa juu wa CCM kuwa asiachiwe
   
 2. awesome

  awesome Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiki kibwn mdogo kimekosa kazi az kufanya, kujipendekeza kwenye matukio kama vifo ili aonekane anajali jamii kweli kumbe wana lao jambo na baba ake/family.
   
 3. T

  The King JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amehudhuria vifo vingapi vya Watanzania vile? Wana wasiwasi wa kupoteza jimbo vinginevyo asingetia mguu maswa. Mara ya mwisho alifika Maswa mwaka gani vile?
   
 4. g

  glojos88 Member

  #4
  Oct 25, 2010
  Joined: Jul 31, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtaka Haki ameshauri kuchunguzwa vizuri jambo hili kwani kuna dalili mbaya.
  Makamba laikuwa huko pia, kwa nini naye asisaidie polisi pia? Kwani ameanza kueleza na ushahidi wa mazingira. Akamatwe aeleze vizuri sana.
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  mgombea wa ccm ana makosa, shibuda anahujumiwa.....
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  This tells u ni namna gani politicking ya bongo isivyokuwa na adabu, huyu dogo hajui kwamba historia inamuhesabu!
   
 7. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Naona CCM wameshindwa kutawala nchi kwa haki na sheria. Uonevu wa jinsi hiyo huzaa chuki na kutoweka kwa amani. Nashindwa kuwaelewa hawa CCM. Hivi wanatumia akili zao za kichwani au akili zao ni makamasi ya puani? Mimi nazidi kuichukia sana CCM na kadi yao nitawarudishia rasmi.
   
 8. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vigumu kujua nani anaongoza nchi hii, JK au Riz1? Nisaidie! maana OCDs, RPCs wako chini ya haka kaduduwasha!
   
 9. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Baba na mwanaaa wanaimba na kuchezaaa
   
 10. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Makamba aliwahi kutoa maneno ya dharau dhidi ya Mh Sibuda wakati alipoondoka CCM. Nadhani Sibuda na Makamba hawakuwa wanaiva ndio maana Makamba anataka kutumia hiyo nafasi kama kete kummaliza adui yake.

  CCM ya Makamba na serikali ya Kikwete ni utawala wa kidhalimu. Na mzee Makamba ni adui mkubwa wa nchi hii na pia ni agent wa shetani mwenyewe. Wanataka kuharibu nchi yetu yenye amani na upendano.

  Hata hivyo, utawala wa kidhalimu hauwezi kusimama hata ukilindwa kwa bunduki na mizinga. Hauwezi kudumu hata kama waganga na walozi watatumia nguvu za giza kuupigania. Utawala utaporomoka ghafla na watu watashangaa.
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hapo kinachotafutwa ni huruma ya wananchi - basi!
   
 12. asam.thegunner

  asam.thegunner Member

  #12
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi ndio siasa za chuki ambazo inabidi tuzikemee. Kuna tatizo gani Riziwani kuhudhuria hayo mazishi? Yeye ni mwana ccm na ana uongozi ndani ya ccm sasa tatizo liko wapi akihudhuria? Kwan kuna mtu ana idadi ya misiba ambayo Ridhiwan kahudhuria? Tuwe wastaarabu sio kila Jamaa analofanya ni tabu kwa wengine. Sioni sababu yeyote ya kuhoji Riziwani kuhudhuria.
   
 13. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Habari nilizozipata ni kuwa mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Maswa Magharibi bwana Robert Kisena ameachiwa huru kwa dhamana (Mwananchi, 25 Octoba 2010,u.k 1 & 4).
  Kinachoniumiza kichwa hapa ni suala la Shibuda,kwa nini mbaka leo wanaendelea kumshikilia,anakosa gani?.Taarifa tulizozipata ni kumba wakati tukio la mauaji,lilipotokea yeye alikuwa anaendelea na mkutano wa kampeni,hivyo hakuwepo eneo la tukio,kwa lugha raisi hakutekeleza mauaji,sasa kwa nini wanaendelea kumshikilia?huu ni uonezi na anashikiliwa ili kumzoofisha kisiasa.Ridhwani ni lazima apatikane maeneo hayo,kwa kuwa huyo ni mtaalamu wa kupandikiza chuki!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 14. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  ingekuwa nchi za magharibi polisi amepigwa na mwanasiasa basi huyo mwanasiasa lazima angesimamishwa na chama chake na angekuwa anasubiria kwenda jela.
  huyu the so called bosi badala ya kumtetea mfanyakazi mwenzako unaweka uoga, stupi...d
   
 15. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Inaonesha wazi kuwa wakifanikiwa kutuibia kura, huyu dogo , baba yake na mama yake jinsi watakavyokaa jikoni kwao na kugawa vyeo kwa maboi zao!!
   
 16. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Sheria inasemaje kwa wale wanao ijua vyema?

  Shibuda alikiuwa jukwaani akihutubia wananchi je inakuwaje anahusishwa na tuhuma za kuwavamia wanaCCM kupigwa mpaka kupelekea kifo cha mwana CCM?
  Chadema nao watuambie nani alitoa amri ya kuwa fuata wale wana CCM na kuwapiga?

   
 17. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani hii iwe kama ni Marekani du! Inabidi kwanza mgombea asimamishwe, pili mkuu wa chama aoombe radhi na taratibu za jela kuanza mara moja in court. Hata sisi tunaweza haya, na hii inaonyesha pia sababu nyingine kwa nini CCM na JK hawatakiwi kuchaguliwa.
   
 18. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  The History is being re-written!

  Shibuda atatolewa rumande kwa nguvu ya wananchi!
   
 19. M

  Mgosingwa Member

  #19
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiki ni kitendo cha kusikitisha mno, hii imetengenezwa katika mazingira ya kumdhoofisha Shibuda katika kampeni kwani inaonyesha sisiem wana hali mbaya wanatumia tukio hili kama mtaji kwao, lakini tumwangalie huyu bwana Riz1 alichofuata kule si msiba bali kupandikiza chuki tu. Huyu ni miongoni mwa vijana ambao hawaifikirii kabisa Tanzania kama ni nchi ya watu anafikiri baba yake ataishi milele. Ngoja ukombozi wa mtanzania utakapotimia tarehe 31/10/2010 ndipo atajua kuwa wenye nchi ni raia wazalendo wa Tanzania. NAOMBA WOTE TUKAPIGE NA KULINDA KURA ZETU ILI TUMWEKE KITINI MKOMBOZI WA WANYONGE WA TANZANIA.
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Huu ni utovu wa adabu na nidhamu uliotukuka!Kumpiga Mkuu wa polisi aliyevaa crown ni sawasawa na kuipiga Jamhuri!Sipati picha ingekuwa vipi kama mtu wa upinzani angempiga Mkuu huyu , ingeonekana ni jambo la kawaida?
   
Loading...